YANAYOHARIBU SAUMU

 

Suala: Mtu ameingiwa na mwiba kwenye macho yake. Na Doctor akamuamrisha atie dawa ya maji ya macho (eye drops) kila muda wa masaa mawili na huku amefunga.nini juu yake?

Jawabu: Jicho limewasiliana na koho (tumbo) ikiwa hiyo dawa ni ya maji, kwa hiyo nina ona alipe hizo siku baada ya kupona. Inshaallah. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Je dawa ya macho inavunja (inatengua) saumu? Nini afanye ambae hawezi kufunga?

Jawabu: Mishipa ya macho inafika mpaka ndani ya koho (koo), ikiwa amehisi uchungu wa dawa kwenye koho lake basi alipe siku alizotia dawa kwenye jicho lake. Na akishindwa kufunga kwa ajili ya maradhi haya tegemewi kupona au kwa kuwa mzee, basi ni juu yake kulisha maskini mmoja juu ya kila siku aliyofungua. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).

 

Suala: Je inajuzu kutumia dawa ambazo hazitii nguvu mwili wakati mtu yuko katika saumu, hali ya kuwa anahisi utamu au uchungu wa hiyo dawa kwenye koo (koho) lake?

Jawabu: Ikiwa kutumia dawa hiyo ni kwa kula au kunywa au kwa njia inayo fanana na hizo kama kutia matone ya dawa (Dreep) kwa kutumia njia inayofikisha tumboni au kooni (koho) basi hayo yanavunja(yana funguza) saumu. Na ikiwa ni dawa inayotiwa katika mwili (mfano: Marham au dawa ya ngozi) au shindano inayopigwa juu ya ngozi basi haibatilishi saumu. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Nini hukumu ya saumu ya mtu ikiwa ameingiwa kwenye Koo (tumbo) lake kitu ambacho si chakula, kama vile kumeza sindano au kipande kidogo cha karatasi?

Jawabu: Neno la Ulamma wote ni kuwa, kitu ambacho si chakula kinaharibu saumu kama chakula, na vitu hivyo ni mfano wa chuma, nywele, ngozi na karatasi. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Atakae ingiwa katika koo lake na mbu, na huku amefunga jee saumu yake inavunjika (inabatilika)?
Jawabu: Haija vunjika (haija batilika) kwa ajili hajakusudia kumeza huyo mbu. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Nini hukumu ya mtu kumeza kilichotoka kwenye kichwa chake (makohozi, makamasi) katika mchana wa mwezi wa ramadhani ikiwa hawezi kukitoa kwa njia ya mdomo wake, pia kumeza kilichotoka kwenye kifua (matapishi, kucheuwa)?

Jawabu: Akiwa amemeza kwa kusudi kati ya hayo yaliyotajwa, basi saumu yake imebatilika, na ikiwa ni nnje ya uwezo wake na makusudio yake basi saumu yake haija haribika. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Atakaemeza makamasi na huku amefunga, je saumu yake inaharibika (inabatilika)?

Jawabu: Ikiwa ameyameza bila ya kukusudia basi haina neno. Na ikiwa kakusudia kwa makusudi basi ailipe siku hiyo. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Je kucheuwa (kutapika) kuna haribu (kunabatilisha) saumu, na khasa macheuwo(chakula) yakitoka kwenye tumbo?

Jawabu: kucheuwa (kutapika) hakuharibu saumu, isipokuwa akirejesha yule mwenye kucheuwa (kutapika) ndani ya tumbo lake kitu katika hayo macheuwo (matapishi), baada ya kuwa na uwezo wa kuyazuia yasirudi ndani. Hii ni kwa alicheuwa (aliyetapika) bila ya kujitapisha yeye mwenyewe, ama aliye cheuwa (aliyetapika) kwa kujitapisha yeye mwenyewe, katika kuharibika saumu yake kuna khilafu baina ya wanavyuoni. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Nini hukumu ya kutumia dawa (tahmil) inayotiwa chini ya utupu wa nyuma (sharaj) au utupu wa mwanake wa mbele (mihbal)?

Jawabu: Ama kwa kutumia njia ya utupu wa mbele wa mwanamke hakuna shaka kuwa kunaharibu saumu. Ama kwa kutumia njia ya utupu wa nyuma ikiwa inafikisha ndani ya tumbo basi inabatilisha saumu kwa manemo ya Ulamma wengi, wakaenda baadhi ya watu wenye elimu kuwa kutumia dawa kwa njia hizi si kama mtu kula chakula au kunywa maji, kwani mtu hawezi kula au kunywa kwa kutumia njia hizo mbili zilizotajwa kabla, na hawajakuta la kukataza kutumia njia hizo. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

MAASI NA MADHAMBI:

Suala: Mwanamume amefanya Zina na mwanamke katika usiku wa mwezi wa ramadhani na si mchana wa ramadhani, je hilo lina athiri (haribu) saumu yake?

Jawabu: Ndio, Kwani saumu yake ina athirika kwa ajili saumu yake inakuwa hai kubaliwi na wala amali zake hazi kubaliwi, kwa sababu Mwenyezi Mungu anasema: (Hakika Mwenyezi Mungu anakubali amali na wanaomuogopa (wanao mcha)). Na jambo hili la kuzini si kitu chochote katika (kumcha) kumuogopa Mwenyezi Mungu, lakini akitubu juu ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu anakubali amali zake na ana mrejeshea ujira wake (thawabu zake). (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Nini hukumu ya aliyedanganya kwa kufanya mzaha, katika mchana wa ramadhani?

Jawabu: Kudanganya ni katika madhambi makubwa, ikiwa kwa hima au kwa mzaha, kwani yamekuja makatazo makali juu ya kudanganya, na nafsi ya kudanganya ni kufanya mzaha, kwani Mtume (SAW) anasema: (Ole wake mwenye kuzungumzisha watu kwa kudanganya ili awachekeshe ole wake, ole wake). Na atakae fanya hivyo na alipe saumu ya siku hiyo, na juu yake atubu kwa Mwenyezi Mungu kwa alilofanya. Na wala halipi kafara, kwa ajili kafara ni kama mpaka unajulikana kwa jambo lenye kutatanisha (Shubuhaat). (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Nini neno (jawabu) lenu katika saumu ya mtu anae funga ramadhani katika nchi za Ulaya (nje), na yeye anaona wanawake wanavyokwenda uchi na machafu mbalimbali?

Jawabu: Mtu anae funga ramadhani katika nchi za Ulaya (nje), au nchi yeyote yenye mambo machafu, akiona huo uchafu ana takikana ainamishe macho yake (asitizame) na amuogope Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ata mkubalia.  (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Je inajuzu kuimba katika mwezi wa ramadhani bila ya vyombo vya music?
Jawabu: Nyimbo katika ramadhani na miezi mingine yote ni haramu, kwa ajili nyimbo ndio inayokaribisha kufanya zina, na ni mazumari (zumari) ya mashetani. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Je saumu inaharibika kwa kuona uchi wa mtoto?
Jawabu: Saumu haiharibiki kwa jambo hilo isipokuwa mwenye kufunga saumu akikusudia kutizama kwa matamanio. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Tumejua kuwa kuvaa nguo ndefu mpaka ikapita vifundo vya miguu (Isbaal) kwa mwanamume kuwa kuna haribu sala. Nini hukumu ya saumu na Hajj kwa mwanamume mwenye kuvaa nguo ndefu kwa makusudi?

Jawabu: Ama kuhusu saumu ikiwa ameshikilia (amekusudia) kuvaa nguo ndefu kwa makusudi ndani ya saumu yake, basi hamna shaka kuwa saumu yake imebatilika, kwa kushikilia kwake kufanya madhambi makubwa ndani ya saumu. Ama Hajj atakae vaa nguo (ihram) ndefu, basi inamlazimikia achinje mnyama. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Vijana wako katika saumu na wanatizama michezo na film za mwezi wa  ramadhani asubuhi na jioni (usiku). Nini hukumu ya saumu yao?

Jawabu: Watubu kwa Mwenyezi Mungu, na kuna khilafu kuhusu kulipa saumu yao, kutokana na khilafu kuwa je maasi yanavunja saumu. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Mtu hasali muda wa mwaka mzima isipokuwa katika mwezi wa ramadhani. Nini neno lenu juu yake?

Jawabu: Atakae wacha sala za faridha anakuwa ametengwa (ameekwa mbali) na Mwenyezi Mungu kama ilivyokuja katika hadithi za Mtume (SAW). Na haku saidii kitu kufunga na kusali katika mwezi wa ramadhani. Kwani dini ya kiislamu haina mapatano na wala Mwenyezi Mungu haikubali nusu nusu. Na mwezi wa ramadhani yanafutwa madhambi kwa yule aliye jikaribisha kwa Mwenyezi Mungu si kwa yule aliye shikilia kufanya madhambi makubwa kama kuacha kusali na mengineo katika mambo ya wajib (faridha), kwani kushikilia madhambi madogo yanaatabirika (yanachukulika-yanahesabika) kuwa ni madhambi makubwa, kwa hiyo vipi kushikilia kuacha nguzo katika nguzo za uislam. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Je kukata ndevu katika mwezi wa ramadhani kuna batilisha saumu?

Jawabu: Kuhusu jambo hili kuna khilafu, kuna Ulamaa wanao sema kuwa maasi yeyote yanafunja (yanabatilisha) saumu. Wanasema: Saumu inabatilika kwa kukata ndevu katika mchana wa ramadhani. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Nini hukumu ya mwanamke aliyemsema (aliye msengenya) mwanamke mwenzake ambae ni dhalimu na muhini wakati wa ghadhabu, hali ya kuwa amefunga. Nini inabidi afanye?

Jawabu: Mtu dhaalim anae julikana waziwazi kwa dhuluma zake, ni kuwa hapana neno kumsengenya kwa dalili ya hadithi ya Mtume (SAW), na saumu ya aliyemsengenya huyo mwanake haija haribika. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Je kudanganya kwa dharura kuna haribu saumu?
Jawabu: Ikiwa ni kwa kuondosha madhara, basi saumu hai haribiki. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Mwanzo wa mwenzi wa ramadhani, nilitizama kwa makini paka na huku wanaingiliana mpaka nikaingia matamanio katika nafsi yangu, nini hukumu ya jambo hili?

Jawabu: Kutizama kwa matamanio wanyama waki ingiliana wenyewe kwa wenyewe ni maasi, ikiwa yame kutoka manii basi saumu yako imebatilika. Na juu yako kuilipa hiyo siku na utubu na utekeleze kafara nako ni kuachia uhuru mtumwa, ukiwa hujapata mtumwa, ufunge miezi miwili kwa pamoja (mfululizo), ukiwa huwezi kufunga miezi miwili kwa pamoja, basi ulishe sitini maskini. Na ikiwa manii hayaja kutoka basi ni juu yako kuilipa hiyo siku. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Nini hukumu ya aliyepunguza ndevu zake katika mchana wa ramadhani?
Jawabu: Kwa mlango wa kuchukua Ihtiyaatt (hadhari), inatakikana ailipe siku yake. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Mwanafunzi amefunga kulipa siku zilizompita katika ramadhani iliyopita, akafutari (akafungua) asubuhi ili ashirikiane na wenzake katika kwenda matembezi (picknick) Muscat, nini hukumu ya kufungua kwake kwani yeye ni jahili (hajui) ya mambo haya?

Jawabu: Kutokana na kuwa yeye hajui (jahili) hukumu ya jambo hilo, na amefungua kwa ajili ya safari, hana hukumu nyingine isipokuwa kuilipa siku hiyo. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Nimejichezea utupu wangu mpaka nika toka manii katika mchana wa mwezi wa ramadhani?

Jawabu: Ni juu yako kutubu kwa Mwenyezi Mungu, na kuilipa siku hiyo na kutekeleza kafara nako ni kuachia uhuru mtumwa, ukiwa hujapata mtumwa, ufunge miezi miwili kwa pamoja (mfululizo), ukiwa huwezi kufunga miezi miwili kwa pamoja , basi ulishe sitini maskini. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Je kuchezea utupu wa uume (mwanamume), kwa kupata ladha bila ya kutoka  manii, kuna haribu saumu?
Jawabu: Ndio, jambo hilo lina haribu saumu, kwa ajili ni kufanya maasi na ndio njia ya kutoka manii na ndio hadafu ya kufanya jimaa (kulala na mwanamke). (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)