|
YANAYO HUSU JANABA NA KUINGILIANA MUME NA MKE KATIKA MCHANA WA RAMADHANI |
|
Suala: Samahat Shk Ahmed: nini neno (jawabu) lenu kwa aliye lala kabla ya sala ya ishaa na hajashituka isipokuwa baada ya kuchomoza al-fajiri (jua), na alipo amka amekuta kwenye nguo yake janaba (manii). Nini juu yake (hukumu yake)? |
|
Jawabu: Juu yake ni kufanya haraka kwenda kukoga janaba, kutokana na hadithi ya Mtume (SAW): (Atakae amka na janaba, basi ame amka hakufunga), kisha atekeleze sala ya faridha ya ishaa na al-fajiri baada ya kumaliza kukoga janaba hata baada ya kutoka (kuchomoza) jua, na lenye nguvu ni kuwa hailipi hiyo siku kwa sababu ameamka na janaba bila ya kukusudia, na janaba si kitu kikubwa kama kula, hali ya kuwa kula bila ya kukusudia hakubatilishi saumu. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)
|
|
Suala: Mtu ametia shaka kuwa yeye ameota kwa kutuko manii baada ya al-fajiri na kutoka (kuchomoza) kwa jua, na mwingine ameota kwa kutoka manii mchana wa ramadhani, na akachelewesha kukoga janaba mpaka yaka kauka manii yaliyo ingia kwenye nguo yake, katika hali hizi mbili ipi inayo batilisha (haribu) saumu? |
|
Jawabu: Atakae ota al-fajiri akchelewesha kukoga janaba kwa makusudi na yeye amefunga basi saumu yake imebatilika, na inamlazimikia kuilipa hiyo siku, kwa sababu hukumu ya wakati wa mchana inakusanya nyakati za baada ya al-fajiri mpaka usiku, na pia atakae ota usiku na akachelewesha kukoga janaba kwa makusudi usiku na aka amka anajanaba ina muajibikia kuilipa siku hiyo. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)
|
| Suala: Mwanamke ametaka kukoga janaba katika mwezi wa ramadhani, lakini amesikia adhana ya al-fajiri na yeye ana anza kujimwagia maji mwilini mwake, na bado hajamaliza kukoga janaba mwili mzima. Nini inamlazimikia afanye? |
|
Jawabu: Wameruhusu baadhi ya wanavyuoni, kuwa
haimlazimikii kuilipa hiyo siku ikiwa amewahi kuosha kichwa chake na utou
wake kabla ya kutoka al-fajiri, na ikiwa hajawahi kuvikosha hivyo vitu
viwili (kichwa na utupu wake), basi alipe hiyo siku.
(Mwenyezi Mungu
ndie mjuzi wa kila kitu)
|
| Suala: Kijana mdogo amefika umri wa miaka kumi na nne, ameota kwa kutokwa na manii katika siku ya mwanzo ya ramadhani. Kutokana na ujahili wake na kutokuwa na maarifa kuwa yeye ameshakuwa (mukalaf) anahisabiwa na Mwenyezi Mungu hajafunga hiyo siku na ramadhani nzima isipokuwa kafunga siku tatu za mwanzo tu, kama watoto wenzake katika mtaa wao. Nini hukumu yake? |
|
Jawabu: Ilikuwa ni juu yake afunge, na kwa ajili
yeye amefungua basi ni juu yake aulipe mwezi mzima wa ramadhani, na juu ya
hayo atekeleze kafara nako
ni kuachia uhuru mtumwa,
ukiwa hujapata mtumwa, ufunge miezi miwili kwa pamoja (mfululizo), ukiwa
huwezi kufunga miezi miwili kwa pamoja , basi ulishe maskini sitini. Na
juu ya yote hayo atubu kwa Mwenyezi mungu kwa alilo fanya (alilo tenda)
(Mwenyezi
Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)
|
| Suala: Nini neno (jawabu) lenu kwa aliyefunga kafara ya miezi miwili kwa pamoja, aka amka katika siku moja hizo na janaba, akalala kwa kutia nia kuwa atakoga janaba kabla ya sala ya al-fajiri, akapitikiwa mpaka ika adhini sala ya al-fajiri. Je ailipe hii siku? Je ailipe hiyo siku baada ya hiyo miezi miwili kwa wakati maalumu? |
| Jawabu: Ndio juu yake kuilipa hiyo siku, na ailipe pale tu akimaliza kufunga hiyo miezi miwili. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu) |
| Suala: Mume amemuingilia (amelala na) mkewe, kabla ya adhana ya al-fajiri, na akamka katika wa huo wa al-fajiri huku hajakoga janaba? |
|
Jawabu:
Akiamka na janaba kwa kwa
kuwa na khiyari inamlazimikia kuilipa hiyo siku, na akiwa si kwa khiyari
yake, lakini ameshituka kutoka usingizini akajikuta ana janaba, basi
afanye haraka kwenda kukoga janaba na hana juu yake isipokuwa hilotu. (Mwenyezi
Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).
|
| Suala: Nini neno (jawabu) lenu kwa aliye funga siku tatu kisha akakuta kwenye nguo yake janaba na yeye hajui lini imeingia janaba? |
|
Jawabu: Akikuta mtu janaba katika nguo yake na
hajui lini imeingia, basi ajaalie kuwa janaba hiyo imeingia katika kulala
kwake mara ya mwisho, na alipe sala alizosali baada ya kuamka katika
kulala kwake mara ya mwisho. Ama saumu ulamaa wamesema: Ailipe siku hiyo
ikiwa umepita mchana mzima na yeye hajui kuwa ana janaba, na wakasema
ikiwa utapita wakati mrefu kuliko huo mchana mzima walau (hata) baadhi
yake, na haya maneno yote ya Ulamaa yanatokana na hadithi sahihi juu ya
Mtume (SAW) : (Atakae amka na janaba, basi ame amka hakufunga. Na akajibu Shk Ahmed jawabu jingine: kwa ajili wewe umepita mrefu zaidi ya mchana na wewe una janaba, basi ilipe saumu ya hiyo siku. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu) |