|
|
UMUHIMU WA KUHUDHURIA VIKAO VYA DINI |
Alhamdulilah
Rabil Aalamin. Baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na Kumtakia rehma bwana
Mtume Muhammad S.A.W. na kuwatakia radhi Masahaba zake wote na waliowafuata
kwa wema hadi siku ya malipo.
Amma
Baad:
Katika fadhila kubwa anazozipata Muislamu
pale anapokusanyika na wenzake wakasomeshana mambo ya Dini yao na
kuelimishana kimaarifa wakapata faida katika kikao chao. Kasema Allah katika
Suratil Kahf Aya ya:
(واصبر
نفسك مع الذين يدعون ربهم بالغداة والعشي يريدون وجهه ولا تعد عيناك عنهم تريد
زينة الحياة الدنيا)
(Na
isubirishe nafsi yako pamoja na wanaomuomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni,
hali ya kuwa wanataka radhi yake. Wala macho yako yasiwaruke kwa kutaka
pambo la maisha ya dunia.)
Kwa hivyo wajibu wa kila Muislamu kuhudhuria
vikao kama hivi vya kuelimishana mambo ya Dini. Alhamdulilah ndugu zenu
wamejitolea kuwaelimisha wenziwao kwa kile walichonacho, wajibu wetu
kuhimizana kuja kusoma, kwani kutafuta elimu ni fardhi kwa kila Muislamu
kama alivyotueleza Bwana Mtume S.A.W.
Na fadhila kubwa huzipata kila mwenye
kuhudhuria vikao vya elimu, Allah Subhanahu Wataala humpa mja wake zawadi
nzuri amabazo hazipatikani katika vikao vyengine. Kasema Mtume S.A.W katika
Hadithi iliyotolewa na Imam Muslim.
)وما
اجتمع قوم في بيت من بيوت الله يتلون كتاب الله،
ويتدارسونه بينهم إلاَّ نزلت عليهم السَّكينة، وغشيتهم الرحمة، وحفتهم
الملائكة،
وذكرهم الله فيمن عنده
(رواه
مسلم
(Na
hawatakusanyika watu katika nyumba ya Mwenyezi Mungu, wanakisoma kitabu cha
Mwenyezi Mungu, na wanasomeshana baina yao, ila Allah huwateremshia utulivu,
na rehma huwafunika na Malaika huwazunguka kwa kuwaombea maghufira, na Allah
huwataja waja hawa kwa wema katika Mamlaka yake).
Imetolewa na Imam Muslim.
Ndugu zangu
Waislamu, Fadhila kama hizi hazipatikani isipokuwa katika vikao
kama
hivi vya kuelimishana. Na Muislamu anatakiwa achukue juhudi kubwa katika
kujielimisha mambo ya Dini yake.
Orodha ya mambo mema anayotakiwa Muislamu
ajilazimu nayo kila siku katika maisha yake:
1-
Jitahidi sana kupata Sala zote katika Jamaa, na usikose Takbiratul
Ihraraam pamoja na Imam, kwani jambo la kwanza atakaloulizwa mja siku ya
Kiama ni Salaa. Na wanawake wasali kila Salaa kwa wakati wake.
2- Jitahidi uzihifadhi sunna za kabliya na
baadiya katika kila Salaa.
3- Jitahidi kusoma URADI baada ya kila Salaa
na madua ya asubuhi na jioni, kwani kuna fadhila kubwa katika jambo hilo.
4- Kudumisha ibada ni jambo muhimu, pamoja na
kuleta istighfaar na tasbihat za kila aina na kumsalia sana Bwana Mtume
S.A.W. kwani kasema:
(من
لزم الاستغفار جعل الله له من كل ضيق مخرجا ومن كل هم فرجا ورزقه من حيث لا
يحتسب)
(Atakaedumisha
Istighfaar basi Allah atamuondolea kila dhiki, na kila tatizo atalitatua
kisha humruzuku kwa njia asiyoitaraji).
5- Jitahidi sana kusoma Qur`aan kila siku
hata kidogo kadiri ya karatasi moja.
6- Jitahidi usali Sala za usiku japo rakaa
mbili kabla ya Alfajiri, kwani Sala hii ni nuur katika moyo wako.
7- Kujikurubisha sana kwa Allah, khasa pale
unaposimama kufanya ibada, ujidhalilishe kwake na kutaka rehma yake na
kumuomba Yeye Pekee.
8- Jitahidi sana kutoa Sadaka na misaada kama
una uwezo, kwani Sadaka huondoa balaa. Kama huna cha kutoa basi jikurubishe
kwa Allah na vitendo vyengine ili upate ujira sawa na mtoaji sadaka. Mtume
kasema: Kutabasamu mbele ya Muislamu mwenzako ni sadaka.
8- Kuwatii wazazi wawili na kuwatembelea
jamaa na majirani.
9-Jitahidi uhudhurie darsa na mihadhara,
kwani huko ndiko kuuhuisha moyo na kunawiri akili.
10- Jitahidi uwatumikie Waislamu wenzako kwa
kuwasaidia kwa kila unaloliweza bila kujikalifisha.
|