|
|
UNYANYAPAA NA UBAGUZI
(Stigma & Discrimination) |
IMETAYARISHWA NA:
SHEIKH ZAHOR SALEH OMAR
UNYANYAPAA NI NINI?
Unyanyapaa au fedheha (stigma) ni hali
inayomfanya mtu ajihisi ana kasoro au aibu. Hali hii ina athari zake kwa
wahusika watakavyojihisi au kubugudhiwa na wengine.
UBAGUZI: Ni athari
mbaya zitokanazo na unyanyapaa na kupelekea mtu kudhulumiwa, kujihisi
mpungufu, mhalifu na aliyetengwa na jamii.
Kuwepo kwa unyanyapaa na ubaguzi kunaharibu
au kudhoofisha juhudi zinazofanywa katika hatua nyengine pia za kupingana na
UKIMWI, kama vile taaluma na njia za kujikinga, kutoa huduma kwa waathirika,
matibabu au hatua za kupunguza athari za mripuko wa maradhi. Matokeo yake
ni kuongezeka kwa balaa litakalowaelemea watu fulani peke yao tu iwe ni
familia au kundi.
Kwa vile hali hii ya unyanyapaa na ubaguzi
inaonekana kukita kwa kiwango kikubwa katika jamii zetu, basi hatuna budi
sote kwa pamoja kuungana kuitokomeza tabia hii.
Ili kupata angalau hisia za muathirika wa
unyanyapaa na ubaguzi, hebu na tuangalie mifano hii ifuatayo:
MAHALA PA KAZI:
Mfanyakazi
aliyeambukizwa na UKIMWI anaweza kukoseshwa haki zake kwa kusimamishwa kazi,
kutopandishwa cheo, au kuzuiliwa nafasi za mafunzo, pamoja na kutengwa na
wafanyakazi wenzake.
HUDUMA ZA AFYA:
Aliyeathirika na
UKIMWI inawezekana akatengwa au kubugudhiwa kwa matusi na watoa huduma za
matibabu, pia huweza kudharauliwa wakati ambapo msaada wa huduma hiyo muhimu
unahitajika zaidi kwa hali yake.
DURU ZA KIDINI:
Mgonjwa mwenye UKIMWI anatazamwa na wengi kwa mtazamo wao wa kidini kama
mhalifu, kwa hivyo anakosa kushirikishwa katika shughuli za kijamii kadri
anavyostahiki.
KATIKA MASHULE:
Watoto
walioathirika kwa UKIMWI, nao hali ya kuwa si wenye hatia kwa namna yoyote
ile, hawatasilimika na kushambuliwa kwa matusi, kero na kudharauliwa.
KATIKA FAMILIA:
Suala hili likiendelea kuwepo katika familia basi athari zake huwa ni mbaya
zaidi hususan kuhusiana na kinga na kutoa huduma.
Pasipochukuliwa hadhari ndani ya familia
ndipo sawa ya gonjwa hili na mafuta yanapomwagiwa mafuta na mripuko wake
kuongezeka.
JINSIA:
Matatizo ya wanawake mara nyingine hutofautiana na yale ya wanaume. Wanawake
mfano wa vizuka wanakuwa ni wahanga wa unyanyapaa na ubaguzi.
Hii ni hali ya kuwanyanyasa kijinsia pasina
kuwepo sababu. Unyanyapaa unaweza kusababisha pia wanawake wasichukue hatua
za kujikinga na maambukizi kutoka kwa waume wao.
SABABU
ZA KUWEPO KWA UNYANYAPAA NA UBAGUZI
Ziko sababu kadhaa zinazofanya hali hii
iwepo na iendelee kuwepo. Baadhi yake na siyo zote ni hizi zifuatazo:
1.
Kutofahamu kabisa au
kikamilifu kuhusiana na UKIMWI na athari zake.
2.
Kuwepo aina fulani
ya hofu au wasiwasi juu ya kujitambulisha au kuwatambulisha walioambukizwa
na UKIMWI.
3.
Matamshi
yanayowakabili waathirika ya kuwalaani na kuwasimanga badala ya kuwaliwaza
na kuwasaidia.
4.
Kuhusishwa kiholela
baina ya UKIMWI na masuala ya ngono.
5.
Itikadi za kidini
ambazo zimekosa upeo sahihi wa kufahamu juu ya suala la UKIMWI.
MTAZAMO WA KIISLAMU JUU YA UNYANYAPAA
Japokuwa inakubalika Kiislamu kusema kuwa
UKIMWI ni adhabu itokanayo na kuenea kwa uasharati kama ilivyo sababu
mojawapo kuu ya kuenea kwa maradhi haya, lakini kuna wajibu wa kuchukua
hatua za makusudi za kupunguza athari zake kwa vile waathirika ni jamii yote
kwa ujumla - aliyemo na asiyekuwemo.
Waumini wa dini ya Kiislamu wamelazimika
kushiriki kampeni dhidi ya UKIMWI katika nyanya zake tofauti, zikiwemo
taaluma za kujikinga, kutoa huduma, kufanya mbiu shawishi (advocacy),
kupunguza arthari, n.k.
Kufanya kampeni dhidi ya unyanyapapaa ni
mojawapo ya mbinu za mpango huo wa kuzuwia maambukizi ya UKIMWI na kupunguza
athari zake.
Shughuli hii kama ni wajibu wa kila Muislamu
kwa kiwango cha nafasi au wadhifa wake aliyonao, umetokana na misingi ya
Kiislamu ifuatayo:
I.
Kauli ya Allah (S.W.) katika Qur’an, anasema:
|
Na uogopeni (jikingeni
na) mtihani au balaa ambalo halitowapata kwa maangamizo wale tu
waliodhulumu (kwa kulisababisha) peke yao. |
|
Tujue kuwa wale waumini wema haitoshi kuwa
wao wamejizuwia nafsi zao na matendo ya kuambukiza magonjwa. Matokeo ya
kunyamazia na kubakia wachamungu ndani ya nafasi zetu tu ni kuangamia sote
kwa pamoja wakiwemo watoto wadogo na wengine wasio na makosa.
II.
Mwenendo
wa Mitume (A.S.):
Mitume wote, na ndio ambao tumeagizwa
kufuata mifumo ya maisha yao,walikuja kulingania mataifa yao katika maisha
ya ndoa za halali na uaminifu kama ni sehemu ya ibada na njia muwafaka ya
kujitosheleza haja za kijinsia baina ya mwanamke na mwanamme. Njia nyengine
zote ni kinyume na maumbile na huwa ni uadui wa kuvamia nje ya mipaka
iliyoruhusiwa:
|
Basi atakayetaka kupita kinyume na hilo (ndoa) hao ndio
wanaofanya uadui.
23:7
|
{Ýóãóäö
ÇÈúÊóÛóì æóÑóÇÁó Ðóáößó ÝóÃõæúáóÆößó åõãõ ÇáúÚóÇÏõæäó
} ÇáãÄãäæä7 |
Kondomu
sio ufumbuzi wala ukewenza siyo tatizo kwenye UKIMWI.
|
Haitobeba nafsi mzigo (wa hatia)
ya mwengine.
35:18 |
{æóáÇ
ÊóÒöÑõ æóÇÒöÑóÉñ æöÒúÑó ÃõÎúÑóì } ÝÇØÑ18 |
Si halali wala ubinaadamu kwa waathirika wa
UKIMWI kubaguliwa kijamii au katika kupatiwa huduma.
Watoto yatima waliofiliwa na wazazi wao kwa
UKIMWI, au huyo aliyepatwa na maradhi akiwa muasharati, hao ni mfano wa
wenye haki kamili ya kusaidiwa sawa na misiba mingine inayowafika hata
wachamungu.
IV.
Hadithi
na Kanuni ya Kifiqhi:
Haifai
kujidhuru wala kumdhuru mwengine
|
áÇ ó ÖÜÜóÑóÑó æ óáÇ óÖÜÜÜöÑóÇÑó
|
Ni kosa kwa mtu yeyote aliyewajibika
kuifuata sheria iwapo atafanya tendo la kumletea madhara yeye binafsi au
kumdhuru mwengine.
Kwa msingi huu, inatosha kufahamu kuwa
miongoni mwa njia kuu za kuambukiza UKIMWI kama uasharati, ulevi, na kutumia
madawa ya kulevya, yote yameharamishwa na sheria ya Kiislamu na zaidi ya
hukmu hiyo yakawa ni njia ya kuleta madhara ya maradhi.
Kwa hivyo basi hata kama jambo hukmu yake
kiasli ni halali hubadilika kuwa haramu kama linamletea mtu madhara.
Na mwenye maradhi pia amelazimika kujizuwia,
au azuwiliwe kwa njia zote za hikma, asimwambukize mwengine kwa makusudi.
Kwa mfano wa hadhari za kuchukuwa kwa
mmojawapo wa watu wa karibu aliyepata maradhi ni kama mume na mke, mama
anayenyonyesha, wawili wanaotarajia kufunga ndoa, anayetoa damu kumchangia
mgonjwa, n.k. yeyote kati hayo mmojawapo akipata maradhi ajizuwie au
azuwiliwe asimmwambukize mwengine.
V.
MSINGI
WA SHERIA:
Mtuhumiwa hatiwi hatiani mpaka lithibiti kosa lake
|
ÇáúãõÊøóåóãõ ÈóÑöíÁñ ÍóÊøóì ÊóËúÈõÊó ÅöÏóÇäóÜÜÜÊõåõ
|
Mgonjwa asibaguliwe kwa Unyanyapapaa wa
UKIMWI eti kwa dhana tu ya kuwa ameupata kwa uhasharati. Kutamka kauli hiyo
ni kosa linalompasa msemaji achapwe bakora thamanini ikiwa atashindwa kuleta
mashahidi wanne wenye akili timamu na waadilifu kuwa wameshuhudia waziwazi
kitendo cha mtuhumiwa kufanya zinaa bila ya kuwepo shubha. Au kwa njia
nyengine akiri mwenyewe mtuhumiwa ili kuthibitisha tuhma hiyo.
Hata baada ya kuthibiti maasi hayo, muhusika
atastahiki adhabu muwafaka kama ilivyotajwa katika sheria lakini hatonyimwa
haki zake nyengine za kutobaguliwa na kuhudumiwa ipasavyo.
VI.
MSINGI WA SHERIA:
Dharura huzingatiwa kwa mujibu wa uzito wake.
|
ÇáÖóÑõæúÑóÇÊõ ÊÜõÜÜÜÞóÏøóÑõ ÈÜÜÜöÞóÏóÑöåÜÜóÇ
|
Haina maana ya kuondoa unyanyapapaa ni
kupita akitangaziwa kila mwenye UKIMWI mabarazani na kwenye vyombo vya
habari, bali huko ndiko kumnyanyapaa kwenyewe.
Cha msingi ni kumdhibiti baada ya
kuthibitika kikweli kusibiwa kwake na ugonjwa asiweze kuwaambukiza wengine,
badala ya kunyamaziwa kimya mgonjwa akaingiliana na wengine kwa njia
zinazojulikana za kuambukiza bila ya yeye mgonjwa kubaguliwa au kubugudhiwa.
Kinachotakiwa ni njia za busara, upole na
utaratibu za kuzinusuru pande zote mbili - mgonjwa asiache asinyanyaswe na
mzima asiambukizwe.
|