|
KUKOGA JANABA NA HUKUMU ZAKE |
|
Suala: Ikiwa Mume ameingiliana na Mkewe na hajatoka manii. Je inawajibikia wakoge janaba? |
|
Jawabu: Vikikutana viumbile viwili (utupu wa mume na mke) inawajibika kukoga janaba ikiwa mume ametokwa na manii au hajatokwa. Hivi ndivyo ilivyothibiti katika hadithi isemayo: (Maji yanatokana na maji) ni mansukh (imefutwa na hadithi nyingine) kwa kuwafikiana wanavyuoni wote.(Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).
|
|
Suala: Mimi ni kijana nina umri wa miaka 19, imefika wakati wangu wa kuowa, na nilipo muuliza rafiki yangu aliyekwisha kuowa kuhusu kujitoharisha baada ya kuingiliana na mke akanijibu jawabu lisilo kuwa wazi. Naomba unipe faida kuhusu kujitoharisha baada ya kuingiliana na mke? |
|
Jawabu: Kujitoharisha baada ya kuingiliana na mke ni vile vile kama kukoga janaba inayowajibika baada kutokwa na manii. Na kukoga janaba hiyo inatakikana ufanye kama ifuatavyo: kwanza unajisafisha baada ya kukojowa kisha unatawadha udhu wa sala au inatosheleza kusukutuwa mdomo na kusafisha pua tu (kutia maji puani). Baada ya hapo unakosha kichwa chako kisha unajimwagia maji mwili mzima na ufikishe maji kwa kutumia mikono yako mpaka yafike sehemu zilizojificha mwilini mwako kama vile kitovu, baina ya utupu na mapaja, na makwapani. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).
|
|
Suala: Je inajuzu kusema "Bismilah" na kutamka nia wakati unakoga janaba? Na je inajuzu mtu akoge huku yuko utupu kama alivyozaliwa katika sehemu iliyositirika (chooni) ikiwa kukoga huko ni wajibu au ni sunna? |
|
Jawabu: Haina haja kutamka "Bismilah" ikiwa unakoka janaba, na nia ya moyoni inajuzu (inatosha), Na haikatazwi kukoga utupu sehemu iliyositirika (chooni).(Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).
|
|
Suala: Jee inajuzu kusalia kwa udhu iloyotiwa wa kukogea janaba, hata baada ya kupita muda? |
|
Jawabu: Ndio sala inajuzu kwa udhu huo ikiwa udhu huo haujaharibika (haujatenguka) (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).
|
|
Suala: Ikiwa mtu mwenye janaba ametayamum kwa ajili ya kusali. Je inajuzia kusoma Qur'aan au kugusa msahafu (Kitabu cha Qur'aan)? |
|
Jawabu: Wamekhitalifiana wanavyuoni kwenye tayamum, je inatumika kwa kuondosha hadath (uchafu) au inatumika kukubalisha kusali tu. Na kauli bora ni ya pili, lakini la msingi kwake atiye nia ya kukubalisha sala, kusoma Qur'aan na kugusa msahafu.(Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).
|
|
Suala: Nini hukumu ya maji yanayotoka kwenye utupu wa mwanamke kwa matamanio? |
|
Jawabu: Ikiwa ni manii inamuajibikia kukoga janaba, na ikiwa kinyume na hivyo basi ni juu yake atawadhe baada ya kujisafisha na maji. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).
|
|
Suala: Je inamjuzia mwanamke atie maji vidole vyake kisha avitie ndani ya nywele zake wakati anakoga janaba bila ya kurowesha kichwa chake na maji? |
|
Jawabu: Hana budi kuchukuwa kiwango cha maji katika mikono yake ili aroweshe misuko ya nywele zake kwa hayo maji kama ilivyokuja katika sunna.(Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).
|
|
Suala: Je inakubalika (inajuzu) kujimwagia maji tu mwili mzima bila ya kujisugua kwa kutumia mikono wakati unakosha janaba? |
|
Jawabu: Wanavyuoni wamekhitalifiana kuhusu jambo hilo, lenye nguvu ni kujuzika (kukubalika) kufanya hivyo ikiwa maji yataingia sehemu zilizojificha mwilini mwake (kitovu,baina ya utupu na mapaja,makwapa)(Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).
|
|
Suala: Mwanamume ana janaba alipotaka kukoga akakuta maji ni baridi sana akasahau kuyapasha moto, lakini akajisafisha pahala penye najasa kisha akakoga kutokea kwenye kitovu mpaka magotini. Baada ya hapo akatayamam na akasali kwa kutayamam kwake. Nini inamlazimikia mtu huyu? |
|
Jawabu: Akiwa anaokopa kudhurika akikoga kwa kutumia maji hayo baridi, basi haikatazwi kutayamam isipokuwa akiwa anaweza kukogea maji hayo baridi itakuwa haifai kutayamam.(Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).
|
|
Suala: Nini jawabu lenu kwa mtu aliyewacha kukoga janaba kwa sababu ya baridi ya maji, akasali bila ya kukoga janaba. Nini inamlazimikia? |
|
Jawabu: Sala haijuzu bila ya kukoga janaba, ikiwa itashindikana kukoga kwa ajili maji ni baridi inawajibika kuyapasha moto maji hayo ikiwezekana. Ikishindikana kuyapasha moto pamoja na kutoweza kuyatumia maji hayo baridi. Inawajibika kuelekea katika kutayamam. Na atakae Sali bila ya kukoga janaba wala kutayamam basi sala yake imebatilika. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).
|
|
Suala: Nini jawabu lenu atakae chukuwa dalili ya maneno ya Mtume (SAW):"Hedhi yako haimo mikononi mwako" kwa kuwa mwili wa mwanamke mwenye hedhi na mtu mwenye janaba ni tahir,akawa anasali bila ya kukoga janaba mpaka ikambainikia hukumu ya jambo hili. Nini inamlazimikia juu ya sala zake na saumu zake zilizopita? |
|
Jawabu: Ni juu yake azilipe sala na saumu alizofunga katika hali ya kuwa na janaba kwa kusharitishwa kuondosha (kukoga) hadath kubwa (janaba au hedhi au nifas) ndio sala na saumu ikubalike. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).
|
|
Suala: Nini jawabu lenu juu ya mwanamke aliyeona (aliyeota) usingizini akayaona (anayoyaota) mwanamume usingizini, kisha hajakoga janaba kwa ajili ya ujahili wake juu ya jambo hilo ikampitia siku nzima bila ya kukoga mpaka hukumu ya jambo hili likambainikia. Nini juu yake afanye? |
|
Jawabu: Ni juu yake alipe sala zote alizo Sali hali ya kuwa na janaba. Akiwa hatajuwa idadi za sala hizo,basi azilipe sala zote toka alipo olewa mpaka situ aliyo anza kukoga janaba(Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).
|
|
Suala: Mwanamke ametawadha udhu wa sala na akasali, kisha baada ya sala akaona katika nguo yake maji meupe (manii). Je ni lazima arejee kutawadha na asali tena, au nini afanye? |
|
Jawabu: Ikiwa hategemei kuwa manii yamemtoka baada ya sala hiyo, basi ni juu yake atawadhe na asali tena.(Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).
|
|
Suala: Atakae wacha kusukutuwa mdomo na kukosha pua wakati anakoga janaba kwa ajili ya ujahili juu ya jambo hilo, nini hukumu ya sala zake alizo sali katika hali hii? |
|
Jawabu: Ikiwa anatawadha akitaka kusali na anasukutuwa mdomo na anakosha pua basi, anasamehewa yaliyopita na achukuwe hadhari siku za mbele.(Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu). |