SAUMU YA SIKU SITA SHAWALL

Ndugu zangu waislamu:
Asalamu Aleikum Warahmatu llahi Wabarakaatu:


Anasema Mtume (SAW): Mngelikuwa mnajuwa yaliyokuwemo katika mwezi wa ramadhani basi mngelitamani ramadhani iwe mwaka mzima).
Haya ni maneno ya Mtume (SAW), je si kweli kuwa ramadhani imekwisha na sisi tuko katika kusheherekea EID na huku tunatamani kuwa laiti ramadhani ingalikuwa haikumalizaka. Haya majonzi (huzuni) ya kuondokewa na ramadhani anayajuwa yule anayejuwa nini hasa saumu si kila mtu anaweza kuwa na fikira hiyo ya kuwa na huzuni ya kuondokewa na mwezi wa REHMA-MAGHFIRA-ITQU MINA NAAR(Kuepushwa na jahanam). Ni kama vile mpenzi ikiwa kweli anajuwa nini maana na faida ya mapenzi, basi anahuzunika akiondokewa na mpenzi wake. Hivi ndivyo inavyotakikana tuwe leo baada ya kuondokewa na mwenzi mtukufu ambao uongozi wa maisha yetu umeshushwa katika mwezi huu.
Lakini Mtume alijuwa kuwa kutakuwepo na watu ambao watakuwa na majonzi (huzuni) kupita kiasi kwa kuondokewa na mwezi wa ramadhani, ndio maana Mtume (SAW) akasema:

(ãä ÕÇã ÑãÖÇä Ëã ÃÊÈÚå ÓÊÇð ãä ÔæÇá ßÇä ßÕíÇã ÇáÏåÑ)

(Atakae funga ramadhani kisha akafuatilia kufunga siku sita za SHAWAAL anakuwa ni kama amefunga mwaka mzima).

Ama kweli Mtume anahikma ambayo haina kifani vipi alijuwa kuwa katika mwaka kuna siku 365, na mwezi una siku 30. Na kila jema unalofanya katika siku ALLAH anakulipa mara 10. Sasa fanya hesabu ifuatayo:-
1) Mwezi wa Ramadhani unasiku 30.
2) funga ya SHAWAAL ni siku 6.
3) Kila jambo jema ukifanya linakuwa thawabu zake mara 10.
Kwa hiyo (30+6)X10= 360 days.
Hapa ndio nyoyo za Waumini zikapowa kidogo baada ya kujuwa kuwa ukifunga mwezi wa ramadhani kisha ukafunga siku sita za SHAWAAL ni kuwa ni kama umefunga siku 365 (mwaka mzima). Lakini mbona katika hesabu ya juu zimepunga siku tano? i.e 365 days-360 days= 5 days.
Hizi siku tano ni nyongeza yako ili upate kuwa katika ibada ya saumu mpaka kufa kwako, na hizi siku ni funga ya Jumatatu na Al-Khamis(2days) katika kila wiki pamoja na funga ya siku tatu katika kila mwezi (funga ya siku za ayaam al-biidh, tarehe 13,14 na 15).
FUNGA YA MAWAKA= (30days+6days)X10+5days = (360days+5days)=365days.
Sasa JAZA mwenyewe?
Shukraan,
 

æÇáÜÜÓÜÜáÇã ÚÜáÜíÜßÜã æÑÍÜãÜÉ Çááøå æÈÜÑßÜÜÇÊÜÜå