|
Watu wengi wanajua makatazo ya sigara na
wazipuuza dalili (zinazothibitisha madhara na hatari yake), tunaomba
utubainishie katika Qurani na Sunna na nini hukumu ya anayesali nyuma ya (imamu)
anayevuta sigara baada ya udhu…?
Sigara ni
sumu ambayo inayoathiri kidogo kidogo na kusababisha mauti ya kufa mamilioni
ya watu kila mwaka kwa ajili ya sigara, na kabla ya miaka miwili imekadiriwa
kufikia kiasi ya watu milioni tatu (wanaokufa) kila mwaka, na inaendelea
kuzidi kwa haraka kuongezeka idadi yake, mpaka wamekadiria kwamba baada ya
myaka michache itafikia mpaka idadi ya watu watakaokufa (kwa ajili ya sigara)
milioni kumi kila mwaka. Na madhara yake (sigara) hapana khitilafu yoyote
baina ya madaktari (wote wameafikiana (kwamba madhara yake ni makubwa sana)
kwahiyo madaktari wameafikiana kuipiga vita sigara na imewabainikia kwamba
inasababisha tafauti ya maradhi ya kensa inayoua, na kadhalika inasababisha
maradhi ya moyo na mishipa ( ya mwilini aina nyingi) na kukwaruzika ngozi,
na kukwaruzika mishipa kwa ndani ni kuziba njia za damu ndani ya mwili, na
anayetumia sigara basi aelewe kuwa antaumia sumi inayompeleka katika mauti
na anaiua nafsi yake mwenyewe.
Amesema
Allah (katika Qurani Surat Annisaa aya na. 29/30): “wala msiziue nafsi zenu,
hakika mwenyezi Mungu ni mwenye kukuhurumieni – na atakayefanya hivyo kwa
uadui na dhulma, basi huyo tutamwingiza motoni, na hayo ni mepesi kwa
Mwenyezi Mungu:… Na bila shaka hiyo sigara ni kitu kibaya kabisa na athari
yake mbaya kabisa kwa mwenye kuitumia na wengineo pia (inawadhuru ukiwapata
moshi wake), na kila kibaya basi ni haramu kama alivyosema Allah. Na Mtume
(S.A.W) ameamrisha awakataze (hata hao) watu wa kitabu mayahudi na manasara
mabaya yaliyotajwa katika vitabu vyao Taurat na Injili… Kasema Allah (katika
Qurani Suratul-Aaraaf aya na 157: “…Anahalalishia vilivyo vizuri na
anawaharamishia vilivyo vibaya..” Na hakuna kitu kibaya kama sumu hii (ya
sigara) inayoangamiza, anaye nusa harufu ya moshi wake tu ataumwa kichwa,
vipi tena anayeitumia? … anapata madhara katika koo, na kikoromeo cha sauti,
na katika kaakaa la kinywa ndani ya ulimi, na katika mrija (unyasi), na
katika ini, na mapafu, na katika mwili wote unaathirika, na… na…
Na kama
inavyojulikana kwamba afya na mali ni neema mbili katika neema za Allah (alizowaneemesha
waja wake) amesema Allah (katika Qurani Suratul-Baqarah aya na. 211: “…Na
mwenye kubadili neema za Mwenyezi Mungu baada ya kufikia basi hakika
Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu.” Jee! Mwenye akili atatia shaka kwamba
anayetumia sigara ni miongoni mwa wenye kubadili neema ya Mwenyezi Mungu?
Basi yeye (mvuta sigara) anaiharifu afya yake na anaungamiza mwili wake na
akili yake, na anaangamiza mali yake katika kuvuta kwake sigara, utaona mtu
anachukua sehemu maalumu katika mali yake anaitupa katika moto kwa ajili ya
sigara, Jee! Haingii huyu mtu katika hukumu ya wapumbavu na mwovu kwa
kuitumia mali yake katika jambo la kipumbavu la madhara?…. na hali Mwenyezi
Mungu amekataza kuipoteza mali (katika mambo ya kuiumbavu na yenye madhara)
na wala asiyapeleke maisha yake katika hatari?… basi vipi watu wanatumia
mali kwa kuzipoteza ovyo na kuharibu afya yao na maisha yao kuwa katika
hatari, Jee! Hii si kubadili kukubwa kwa neema za Mwenyezi Mungu?
Na kama
tulivyosema kwamba sigara ni sumu inayoua mtu, na anayevuta sigara anajuiua
nafsi yake, katika hadithi iliyopokewa na Ibn Murdawih kwa njia ya Abu
Hurairah ®, kasema Mtume (S.A.W.): “Atakayejiua nafsi yake kwa (silaha ya)
chuma, basi ataletwa na chuma chake kakishika mkononi mwake anajichoma nacho
tumboni mwake siku ya kiyama na kutupwa katika moto wa Jahannam akae humo
milele, na anayejiua nafsi yake kwa sumu, basi atakuja na sumu yake mkononi
mwake anakwenda nayo kuila humo katika moto wa Jahannam milele”
Ama kuhusu
Imamu anayevuta sigara baada ya kutia udhu, haijuzu kusali nyuma yake, na
yoyote anayefanya hivyo basi sala yake batili.
|