القرآن والسنّة في ذاكرة الأمّة

QUR-ANI NA SUNNA KATIKA FIKRA ZA UMMA

Baada ya kumshukuru Allah kama anavyostahiki kushukuriwa sala na salamu zimfikie Nabii Muhammad s.a.w. pamoja na sahaba zake na kila anayefuata njia yake .

Umma wa Kiislamu :

Anasema Allah Mtukufu katika kitabu chake kitukufu, akielezea sifa za utume na kazi zake, :

هو الّذي بعث في الأميّين رسولا منهم يتلوا عليهم آياته ويزكّيهم ويعلّمهم الكتاب والحكمة وإن كانوا من قبل لفي ضلال مبين .  الجمعة : 2

Yeye ndiye aliyeleta mtume katika watu wasiojua kusoma, anayetokana na wao, awasomee aya zake na kuwatakasa na kuwafunza kitabu na hikma, na kabla ya haya walikuwa katika upotofu uliodhahiri.

Kwa hivyo kuletwa kwa manabii na mitume Alayhimu Salaam, ilikuwa kwa ajili ya kutiliamkazo yale yaliyotambuliwa na akili, au kuwekawazi yale yasiyoeleweka, na vilievile kuja kwao kupitia njia ya ujumbe wao ni kuitika wito wa maumbile ya mwanadamu na haja zake, na kukihifadhi cheo chake na mali yake na nafsi yake, lakini juu ya hayo yote ujumbe wa mbinguni ulipata upinzani mkali kutoka kwa kaumu yake na vita vikali kutoka kwa wakanushaji, anasema Allah Mtukufu

يا حسرة على العباد ما يأتيهم من رسول إلاّ كانوا به يستهزئون . / يس : 30

Inafaa kusikitikiwa hawa waja , hakuwajia mtume yeyote ila walikuwa wanamfanyia mzaha .

Lakini wakati huohuo ulikubaliwa na wenye akili timamu na wenye maumbile yaliyosalimika , anasema Allah Mtukufu :

وما أرسلنا من رسول إلاّ ليطاع بإذن الله . / النساء 64

Na hatukumleta mtume yeyote ila atiiwe kwa amri ya Allah .

 Na siri ya kuwepo tofauti baina ya makundi mawili ni kwamba watu wana malengo tofauti, wamo wanaoamrishwa na matamanio yao, na wengine wanaoshindwa na nafsi zao, na wengine waliopofolewa na chuki zao, na kuna wengine waliotakaswa na akili zao na kuokolewa na busara zao, na ujumbe wa Nabii Muhammad s.a.w. hautafautiani na ujumbe wa mitume waliotangulia, hakuwahi kuitika vizuri amri ya mola wake isemayo :

وأنذر عشيرتك الأقربين . / الشعراء : 214

Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe .

 Mara akasimama miongoni mwa wenye chuki akasema :

تبّا لك أ لهذا جمعتنا .

maangamio juu yako kwa jambo hili ndio umetuitia.

 Kwa hivyo mwenye kuzingatia katika historia ya daawa ya kiislamu, atakuta kuwa kuipiga vita batil, katika zama zote ni kushindana baina ya elimu na ujuzi, na upotofu na uongofu, na baina ya uovu na wema, na mara zote hatima ya vita hivi haki huwa ni mshindi na batil huporomoka, kwa sababu hoja za batil hazina nguvu mbele ya haki, anasema Allah Mtukufu :

بل نقذف بالحقّ على الباطل فيدمغه فإذا هو زاهق ولكم الويل ممّا تصفون . / الأنبياء : 18

Bali tunaitupa haki juu ya batil ikalivunja bufuru la kichwa chake, na mara batil ikatoweka, na adhabu inakungojeeni kwa ajili ya haya mnayonena (kumsingizia Allah).

 Umma wa Kiislamu :

Ilivyokuwa mpo katika kumbukumbu ya historia ya mtume s.a.w. huwa hapanabudi kuzingatia misukosuko iliyoikumba qur-ani pamoja na sunna ya Mtume s.a.w. ikiwemo misukosuko ya kivitendo au kimatamshi au vinginevyo, lakini yote iligonga mwamba na kugongana wenyewe kwa wenyewe, kwa mfano mara walikuwa wakiisifu qur-ani kuwa ni mashairi na mtume ndio mtunzi wake, na sababu ya kusema hivyo ni kuwepo upangilizi mzuri wa aya zake, lakini ilikuwa inatafautiana sana na mfumo wa mashairi yao, anasema Allah :

وما علّمناه الشّعر وما ينبغي له إن هو إلاّ ذكر وقرآن مبين . / يس : 69

Na wala hatukumfundisha mashairi, wala haiwi kwake (kuwa mtunga mashairi) haikuwa qur-ani ila ni ukumbusho na kitabu kibainishacho .

Na mara nyengine wanaisifu qur-ani kuwa ni uchawi, kwa sababu huwatoa watumwa katika taa ya mabwana zao na kuwafanya watukufu wao kuvutika na kuikubali dini hii, na mara humsifu Mtume kuwa ni mwendawazimu kwa sababu :

أجعل الآلهة إلها واحدا إنّ هذا لشيء عجاب . / ص : 5

Oh! Amewafanya miungu wote kuwa mungu mmoja tu! Bila shaka hili ni jambo la ajabu.

 Umma wa Kiislamu :

Hakika qur-ani tukufu na sunna iliyokirimiwa zilikuwa na zitaendelea kuwa misingi ya uongofu,

إنّ هذا القرآن يهدي للّتي هي أقوم ويبشّر المؤمنين الّذين يعملون الصّالحات أنّ لهم أجرا كبيرا ./ الإسراء : 9

Hakika hii qur-ani inaongoza katika njia iliyonyooka kabisa, na inawapa habari njema waislamu wafanyao vitendo vizuri, ya kwamba watapata malipo makubwa.

 Lakini juu ya hayo, ujinga unaweza kumpofoa mwenye kuona na kuiondosha akili pahala pake na kumfanya mwanadamu atumbukie shimoni hali ya kuwa anamacho, na haya yanatokana na ushabiki wa kijinga, ambao hupelekea mtu kukataa jambo ambalo anauona ukweli wake, kama walivyofanya baadhi ya watu, katika kuipiga vita sunna ya Mtume Muhammad s.a.w. Kwa hivyo kila anayetafuta ukweli ili aweze kupambanua baina ya haki na batil na baina ya ujuzi na ujinga, basi huyo ndiye aliyefanikiwa katika njia yake, anasema Allah :

قل هل يستوي الّذين يعلمون والّذين لا يعلمون إنّما يتذكّر أولوا الألباب . / الزمر : 9

Sema: Je! Wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua? Wanaotanabahi ni wale wenye akili tu.

 Lakini ikiwa mtu anatafuta ukweli kwa lengo la kuupoteza na kuuficha, basi huwa sawa na nyumba ya buibui,

وإنّ أوهن البيوت لبيت العنكبوت لو كانوا يعلمون . / العنكبوت : 41

Na bila shaka nyumba iliyodhaifu kuliko zote ni nyumba ya buibui, laiti wangalijua.

 Na inatupasa tutambue kuwa qur-ani tukufu pamoja na sunna ya Mtume s.a.w. zimehifadhiwa na zitabaki hadi kiama, anasema Allah Mtukufu :

إنّا نحن نزّلنا الذّكر وإنّا له لحافظون . / الحجر : 9

Hakika sisi ndio tulioteremsha mauidha haya (hii qur-ani) na hakika sisi ndio tutakaoilinda.

 Na kuhifadhika kwake na kubakia kwake, ni pale waislamu watakapoisoma na kuifanyia kazi, kwani Mtume s.a.w. hakuweza kushinda isipokuwa pale alipoifanya qur-ani kuwa mwenendo wa sahaba zake na inatembea katika maisha ya watu, na wakawa wanafuata mwenendo wa mtume wao,

لقد كان لكم في رسول الله أسوة حسنة لمن كان يرجو الله واليوم الآخر وذكر الله كثيرا . / الأحزاب : 21

Bila shaka mnao mfano mwema kwa mtume wa Allah, kwa mwenye kumuogopa Allah na siku ya mwisho, na kumtaja Allah sana.

Na sisi hii leo ikohaja kubwa ya  kushikamana na sunna ya mtume wetu, na kupandikiza katika nyoyo za watoto wetu mapenzi ya mtume wetu, na kuwahimiza kuihifadhi, anasema Allah :

قل إن كنتم تحبّون الله فاتّبعوني يحببكم الله ويغفر لكم ذنوبكم والله غفور رحيم . / آل عمران : 31

Sema : ikiwa nyinyi mnampenda Allah, basi nifuateni, hapo allah atakupendeni na atakughufirieni madhambi yenu. Na Allah ni mwenye maghufira na mwenye rehma.

 Basi mcheni Allah ndugu waislamu na fuateni mwenendo wa mtume wenu mtafaulu hapa duniani na mtafuzu kesho akhera.

والسلام عليكم ورحمة الله وبركاته .