|

NASAHA ZA RAMADHAN
1-
Jitahidi kuufanya mwezi huu mtukufu uwe mwezi wa
kuihisabu amali zako na kutubia na kutengeneza makosa yako.
2-
Jitahidi kusali sala ya jamaa na tarawehe; kwani
Mtume (SAW) kasema: “ Atakae Sali na Imam mpaka akamaliza, basi ataandikwa
kuwa miongoni mwa wale waliosali usiku”
3-
Jikinge na israfu ya mali na nyegineo; kwani
israfu imeharamishwa na inakupunguzia nafasi ya kutoa sadaka na thawabu
zake.
4-
Weka juhudi kuendelea na mambo mema ambayo
umejizowesha kuyafanya katika mwezi huu mtukufu.
5-
Hakika mwezi huu ni mwezi wa ibada, sio mwezi wa
uvivu na kulala.
6-
Uzoweshe ulimi wako kwa kuudumisha na kumdhukuru
Allah, na wala usiwe miongoni mwa wale walio kuwa hawamdhukuru Allah
isipokuwa kidogo.
7-
Unapohisia njaa kumbuka kuwa wewe ni dhaifu na wala
huwezi kuvumilia kukosa neema za Allah (chakula, maji…..nk).
8-
Usiwache nafasi ya mwezi huu mtukufu kwa kujizuwia
kwa mabaya ambayo hayakupi manufaa yoyote bali yanakuletea madhara.
9-
Juwa kuwa kazi ni amana, basi jihisabu nafsi yako
kwa kujiuliza : Je nimeifanya kama inavyotakikana.
10-
Kimbilia kuomaba msamaha kwa yule uliyomdhulumu
kabla ya kukuchukulia thawabu zako (kesho Akhera).
11-
Jitahidi kulisha aliefunga ili upate ujira (malipo)
kama yake.
12-
Jua kuwa Allah ni mwingi wa kukirimu na mwingi wa
kurehemu na anakubali toba ya wenye kutubia na kuwa Allah ndiye mwenye
kuadhibu adhabu kali, anatoa nafasi ya kutubia na wala hapuuzi waja wake.
13-
Kama ulifanya ovu na Allah (SWT) akakusitiri, basi jua kuwa hilo ni
onyo kwako wewe ili utubie, basi kimbilia kuomba msamaha na azimia
kutorudia kutenda ovu hilo.
14-
Juwa kuwa Allah ametuhalalishia kuzifurahisha nyoyo
zetu mbali na haramu, lakini usijiendekeze kwa kuutumia wakati wote kwa
kujifurahisha nafsi yako na ukapitisha nafasi ya kufanya mambo ya kheri.
15-
Juwa kuwa kutafuta ilimu ni ibada, basi jitahidi na
kusoma tafsiri za Qur’an, hadithi za Mtume (SAW) na mwendo wake pamoja na
elimu ya dini.
16-
Jitenge na marafiki wabaya na jitahidi kukaa na
marafiki wazuri (wema).
17-
Kwa hakika kujizowesha kwenda msikitini mapema ni
dalili ya imani na kuwa na hamu ya kufanya ibada.
18-
Jitahidi kuwaongoza waliokuwa chini ya uwongozo
wako kwa mambo yanayowafaa na dini yao, kwani wao wanakusikiliza
zaidi kuliko wengineo.
19-
Usifanye/usipike namna nyingi za vyakula kwani
itakushughulisha kutopata nafasi ya kusoma Qur’an na kufanya ibada.
20-
Punguza kwenda sokoni au madukani katika siku za
Ramadhani na hasa siku za mwisho wa Ramadhani ili usije ukapitwa na hizo
siku thamini.
21-
Kumbuka kuwa mwezi huu mtukufu ni mgeni wa kupita
njia basi jitahidi na kuupokea (kumkirimu mgeni huyo) kwa vizuri. Kwani
ni haraka kumkumbuka akiondoka.
22-
Jitahidi na kuamka usiku kusali katika kumi la
mwisho la Ramadhani kwani hizo siku zinafadhila kubwa sana, na
ndani yake kuna usiku mmoja ambao bora kuliko miezi elfu moja.
23-
Kaa ukijua kuwa siku ya Idi ni siku ya kumshukuru
Mola basi usiifanye kuwa siku ya kuanza kuyarudia yale maovu ambayo
ulikuwa umejizuia katika mwezi wa Ramadhani.
24-
Tahadhari na kula mchana wa ramadhani bila ya
dharura ya kukubalika, kwani atakae fanya hivyo hatoweza kuikidhi siku
hiyo hata akifunga milele.
25-
Jitahidi kufanya itikafu japo kidogo (hasa katika
kumi la mwisho).
26-
Inapendeza kupiga Takbir kwa sauti kuanzia usiku wa
Idi na asubuhi yake mpaka ifike wakati wa sala ya Idi.
27-
Jihisabu/jipime nafsi yako katika mambo yako yote
kama:
Kuhifadhi sala ya jamaa-zakaa-kutembelea jamaa
zako-kuwafanyia wema wazi wako (mama na baba)-kutembelea jirani-kutofanya
israfu-kuwapa malezi mazuri waliokuwa chini ya uongozi
wako-kujishughulishe na mambo yanayowahusu ndugu zako wa kiislamu-
kutahadhari na kujionesha-kumpendea ndugu yako muisilamu jambo
unalolipendea nafsi yako-kutowasema (nyuma yao) ndugu zako wa
kiisilamu-kuisoma qur’ani na kuzingatia maana yake-kuwa na utulivu
unapoisikia.
æÇáÜÜÓÜÜáÇã ÚÜáÜíÜßÜã æÑÍÜãÜÉ Çááøå æÈÜÑßÜÜÇÊÜÜå
|