|
Kuhiji kuna namna tatu, nazo:
1-
Tamat-tuu: Nayo ni
kuhirimia umra peke yake katika miezi ya hija, akimaliza atatokana na ihramu
ya ibada hiyo, kisha atahirimia hija siku ya Tarwiya (8 Dhul-hija) au
kabla yake. Tamat-tuu ndio namna bora ya kuhiji, na inashurutiziwa
iwe umra na hija katika mwaka mmoja na safari moja na asirejee nchini kwake
au mfano wake kwa umbali baina ya ibada mbili hizo.
Mfanya-tamat-tuu humwajibikia
kichinjo cha Tamat-tuu.
2-
Qiraanu: Nayo ni
kuhirimia hija pamoja na umra katika miezi ya hija kisha kubaki na ihramu
mpaka atakapotokana na ihramu ya ibada mbili hizo kwa pamoja siku ya
kuchinja (10 Dhul-hija).
Mfanya-Qiraanu huwajibika pia kuchinja. Yeye
inamtosheleza Tawafu moja na Sai moja kwa hija na umra yake, kutokana na
kauli yake - rehema za Allah na amani zimshukie:
“Mwenye kuhirimia hija pamoja na umra itamtosha
Tawafu moja na Sai moja kwa zote mbili mpaka ajihalalishe nazo pamoja.”
Ameipokea Tirmidhi na Ibnu Maajah. Na kuna kauli kuwa
lazima kuwe na Tawafu mbili na Sai mbili.
Lakini huyu aingiapo Maka atatufu Tawafu ya
Quduum (kufika Maka), na anaweza kufanya Sai kabisa akitaka, halafu
atakaporejea siku ya kufanya Tawafu ya Ifadha akatoshelezeka kwa Tawafu tu;
kwasababu ameshafanya Sai hapo kabla kwa uoni wa baadhi ya wanazuoni. Na
kuna kauli aakhirishe Sai apate kuifanya pamoja na Tawafu ya Ifadha.
3-
Ifraadu: Nayo ni
kuhirimia hija peke yake na kubaki na ihramu yake mpaka atakapolirushia
vijiwe Jamratul-Aqaba siku ya kuchinja (10 Dhul-hija).
?
Mfanya-Ifraadu
haimlazimu umra anapofanya hija pekee. Akitaka kufanya umra ni baada ya siku
za Tashriiq (ambazo ni 11 – 13 Dhul-hija).
?
Inajuzu kuhirimia hija
pekee hata kwa ambaye hakufanya umra hapo kabla.
Mfanya-Ifraadu inamjuzia kutufu Tawafu ya Quduum
bila kufanya Sai
|