Madhambi ya ulimi

NAMIMA

Namima maana yake ni kuchukua maneno ya huyu na kuyapeleka kwa yule kwa kusudi ya kuwagombanisha. Na hii ni katika sifa mbaya ambayo imepingwa na Uislamu. Na mwenye kuwa na sifa kama hii ni mtu anayechukiza sana mbele ya Allah, ndio akabashiriwa moto na akaharamishiwa na Pepo hapa hapa Duniani kama hakutubia na akawacha sifa kama hiyo. Katika Hadithi iliyotolewa na Imam Al Bukhari na Muslim kwa njia ya Abu Hurairah. Kasema Mtume (S.A.W):

( Åöäøó ÔóÑøó ÇáäøóÇÓö Ðõæ ÇáúæóÌúåóíúäö ÇáøóÐöí íóÃúÊöí åóÄõáóÇÁö ÈöæóÌúåò æóåóÄõáóÇÁö ÈöæóÌúåò )

“Kwa hakika watu wabaya kabisa ni wale wenye nyuso mbili. Anawajia watu hawa kwa uso huu. Na Huwendea wengine kwa uso mwengine”.

Na kawaidi ya Mtu mwenye sifa kama  hii ni yule munafiki. Ndio hata Mwenyezi Mungu akatutahadharisha nao watu kama hawa tusikae nao wala tusiwatii. Kasema Mwenyezi Mungu katika Surat Nuun Aya ya (8-11):

( ÝóáóÇ ÊõØöÚú ÇáúãõßóÐøöÈöíäó*æóÏøõæÇ áóæú ÊõÏúåöäõ ÝóíõÏúåöäõæäó*æóáóÇ ÊõØöÚú ßõáøó ÍóáøóÇÝò ãóåöíäò*åóãøóÇÒò ãóÔøóÇÁò Èöäóãöíãò)

“Basi usiwatii wanaokadhibisha* Wanapenda ungalikuwa laini kwao* Wala usimtii kila muapaji sana, aliye dhalili* Msengenyaji (msemaji watu) aendae akitia fitina”.

Mara moja Mtume (S.A.W) alipokuwa yumo safarini alipita katika makaburi ya watu wawili bado ni mepya. Akasimama akasema: Hakika ya maiti hawa wanateswa. Na sababu ya mateso yao si kubwa. Ama mmoja kati yao alikuwa hajilindi na mkojo.  Na wa pili  alikuwa anatembeza namima.

Kwa hivyo mtu kama huyo huanza kuadhibiwa tokea kaburia kwa sababu ya dhambi kama hiyo iliyochumwa na ulimi wake mwenyewe. Na katika Hadithi iliyotolewa na Imam Ahmad kwa njiya ya Asmaa bint Yazeed (Radhi za Allah ziwe juu yake). Kasema Mtume (S.A.W):

( ÃóáóÇ ÃõÎúÈöÑõßõãú ÈöÎöíóÇÑößõãú ÞóÇáõæÇ Èóáóì ÞóÇáó ÝóÎöíóÇÑõßõãö ÇáøóÐöíäó ÅöÐóÇ ÑõÁõæÇ ÐõßöÑó Çááøóåõ ÊóÚóÇáóì ÃóáóÇ ÃõÎúÈöÑõßõãú ÈöÔöÑóÇÑößõãú ÞóÇáõæÇ Èóáóì ÞóÇáó ÝóÔöÑóÇÑõßõãõ ÇáúãõÝúÓöÏõæäó Èóíúäó ÇáúÃóÍöÈøóÉö ÇáúãóÔøóÇÁõæäó ÈöÇáäøóãöíãóÉö ÇáúÈóÇÛõæäó ÇáúÈõÑóÂÁó ÇáúÚóäóÊó).

“Je! Nikwambieni wale waliobora miongoni mwenu. Wakasema: Ndio. Akasema  Mtume (S.A.W): Waliobora miongoni mwenu ni wale wanapopata matatizo humkumbuka Mwenyezi Mungu.** Kisha Mtume (S.A.W) akauliza tena. Je! Nikwambieni wale walioshari baina yenu. Wakasema: Ndio. Akasema (S.A.W) Walioshari baina yenu ni wale wanaofisidisha baina ya wapenzi na kwenda na namima”

Na Mtume (S.A.W) katika Hadithi nyingi alikuwa akiwatahadharisha Masahaba zake na sifa hii mbaya ya namima. Mpaka ilifika hadi ya kusema: “Hatoingia Peponi mtu mwenye sifa ya namima.”

Ewe mwenye kuwa na sifa kama hii. Umepata lipi kubwa pale ulipowagombanisha watu. Huogopi adhabu kali Kesho Akhera. Una nguvu gani za kuweza kusubiri Moto wa Jahannam. Wallahi nyumba nyingi zimebomolewa kwa sababu ya maneno ya uwongo na fitina. Wangapi wameachana baada ya kuishi uzuri. Wangapi waliokuwa wakipendana kama ndugu na kusaidiana. Akaja mleta namima akayavunja mapenzi yao wakawa kila mmoja anamkimbia mwenzake.

Ndugu yangu Muislamu chuki ni katika maradhi makubwa ambayo watu wanaumwa nayo. Mara nyengine huchukiwa mtu bila ya sababu, au huwenda ikawa katika sababu za kijinga. Waislamu haifai kuwa na chuki baina yao. Lazima wawe wanapendana lao liwe moja. Sio kila mmoja anamuona mwenzake kama nyoka. Imefika hadi Waislamu wawili wanakutana pahala basi hata salamu hawatoleani. Kila mmoja anajiona kuwa yeye ni bora zaidi. Eti tunatafuta sababu ya kutokukubaliwa dua zetu, na kumbe tunayoyafanya ni makwubwa kwa Mola wetu. Mfano mzuri  wa kuufata ni Masahaba. Hebu tuwatazame vipi yalikuwa maisha yao. Walikuwa kama hawakumuona mwenzao katika Sala moja ya Jamaa hakuja, basi upesi hukimbilia kwake kumtazama labda anaumwa. Lakini leo anakufa jirani yako habari huna. Unashtukia janaza tu linatolewa ndani ya nyumba. Waislamu amkeni na ghafla kama hii. Kuna kisa kizuri kilitokezea zama za Bwana Mtume

(S.A.W) kinachomaanisha kwamba Muislamu anatakiwa asiwe na bughdha wala chuki wala hasadi juu ya Muislamu mwenziwe.

Mara moja Mtume (S.A.W) alikuwa kakaa na Masahaba zake Msikitini akawaambia: Ataingia Mtu hivi sasa katika watu wa Peponi. Baada ya muda kidigo akaingia bwana mmoja kishatoka kutia udhu na kungojea Sala. Siku ya pili Mtume alipokuwa kakaa tena na Masahaba zake, akawaambia tena maneno yale yale ya kuwa ataingia mtu hivi sasa katika watu wa Peponi. Baada ya muda kidogo akaingia bwana yule yule wa jana. Siku ya tatu Mtume (S.A.W) akasema yale yale yaliopita na akatokezea tena bwana yule yule. Sahaba mmoja  anaeitwa Abdillahi bni Omar (mtoto wa Sayyidna Omar bni Lkahataab) akataka kujua kitu gani kikubwa huyu anachokifanya mpaka Mtume (S.A.W) akambashiria Pepo mara tatu. Akasema Inshaala nitakifatilia nami nikijuwe ili nami nifanye. (Hapo bila ya kuwa na hasadi wala choyo, isipokuwa ni kutaka kushindana katika mambo ya kheri). Huyu Bwana Abdillahi bni Omar akatoka mpaka katika nyumba ya yule sahaba aliyebashiriwa Pepo mara tatu, na inasemekana ya kwamba jina lake alikuwa anaitwa (Hurquus bin Zayd Al Saadi).

Bwana Ibn Omar akafunguliwa mlango na kuingia. Kisha akaomba ombi la kutaka awe mgeni muda wa siku tatu katika nyumba ya (Hurquus) kwa sababu ya maatizo nyumbani kwao baina ya yeye na baba yake. (Hila hii aliitumia sahaba huyu ili apate kukaa mle ndani ya nyumba ili aone amali gani nzuri mtu hufanya mpaka akabashiriwa Pepo mara tau. Bwana Abdillahi akakaa humo siku ya kwanza huku akichunguza. Muda wa siku tatu hakuona kubwa linalotendeka ili ifike daraja ya kubashiriwa Pepo. Hapo tena ilimbidi amuulize mwenyewe kwa kumwambia (Ewe Hurquus ndugu yangu) mimi nilikuwa sina shida ya kukaa kwako ila kwa jambo moja tu, ni kutaka kujua amali gani nzuri unayoifanya mpaka Mtume (S.A.W) akakubashiria Pepo mara tatu. Hebu niambie nami nipate kunufaika. Bwana Hurquus akajibu (Wallahi hakuna jengine ila hayo uliyoyaona. Lakini mimi kawaida yangu ninapoingia kulala huwa moyo wangu kama karatasi nyeupe, sina chuki wala bughdha na Muislamu yoyote katika ulimwengu huu.

Subhana Llaah! Leo hii ukitaka kuwahisabu unaowaonea chuki ni wengi sana. Mtu anaingia kulala na moyo wake umejaa hasadi na chuki. Hili ni somo watu lazime wachukuwe riwaza katika maisha yao. Waliogombana warudi na wapatane. Walioachana warudiane. Kwani hakuna bainaadamu aliyekamilika katika Ulimwengu huu. Kila mmoja wetu ana ila yake lakini wajibu wetu ni kustahamilina na kusameheana.

Tukibakia bado katika mlango wa namia nadhani msomaji atakuwa pamoja nami ya kuwa kila mwenye sifa ya namima huwa na chuki katika moyo wake. Ndio akataka kuuburudisha moyo wake kwa kuwafitinisha watu. Na mwenye sifa ya namima huwenda ukaka naye lakini humjuwi. Mbele yako hukupa maneno matamu lakini ukiondoka tu, huyabadilisha yakawa mengine mabaya ya kufedhehesha. Kuna kisa kilitokezea hapo zamani. Kinachobainisha ya kuwa mwenye sifa kama hii ya namima lazime tuepukane naye. Tena tumuogope wala  tusimtolee siri  zetu.

Hapo zamani palikuwa kuna bwana mmoja akiishi na mkewe. Lakini Mwenyezi Mungu hakuwapa neema ya watoto. Akaamua ende akatafute mtumishi kijana mdogo ili aishi naye humu nyumbani yeye na mkewe. (Kama mnavyojuwa zamani watoto walikuwa wakiuzwa kama watumwa). Bwana akenda sokoni akatafuta kijana mpaka akampata. Kabla ya kumnunua akamuuliza muuzaji. Vipi sifa za kijana huyu? Muuzaji akajibu. Hodari lakini ana sifa moja tu! Ya namima. Bwana mnunuwaji akaiona hiyo ni sifa ndogo tu haina madhara kwake, basi akamnunuwa. Kijana huyo akaishi muda katika nyumba ile. Ilipofika taimu ya kuanza na tabia yake mbaya ya kupeleka namima, akamuanzia bibie kwa kumwambia: Huyu mumeo ana mwanamke mwengine nje na karibu hivi atakuwa hakujali tena. Bibie baada ya kuyasikia maneno hayo roho ilimruka (kama ilivyo tabia ya wanawake wa siku hizi wanaposikia waume zao wanataka kuengeza mke). Bibie akawa tayari afanye kitu chochote kile ili bwana ampende yeye tu, akamuuliza yule kijana. Sasa jee kuna dawa yoyote ya kuifanya. Kijana akajibu akasema: Ndio, dawa ipo. Wewe nipatie ndevu za mumeo za nchani leo anapoingia kulala nenda na kiwembe umkate kisha uniletee. Nitakufanyia dawa. Baada ya muda mdogo tu akatoka kwenda kwa bwana wake ili amueleze yaliyo shari kuliko yaliyopita. Akasema kumwambia bwana wake: Una habari ya kuwa huyu mkeo ana mwanamme mwengine na wameshaamua wakuuwe ili waishi kwa raha yao. Na usiku wa leo kuwa na hadhari kubwa huwenda ukauliwa. Bwana akawa hana raha. Ulipofika usiku kila mmoja ana khofu ya ajabu. Bwana anaogopa kuuliwa na mke anataka ndevu. Bwana akaingia chumbani kulala. Lakini hakulala kajitia tu kulala anamngojea huyo atakaekuja ili apambane naye. Huku bibie kaona hivi sasa bwana tayari kishalala niende nikazikate zile ndevu. Akachukuwa kiwembe chake alipokurubia tu, bwana akaamka akamuona mkewe ana kiwembe kikali mkononi akajuwa kwamba haya ni mauti na maneno aliyoambiwa ni ya kweli. Papo hapo akamnyan’ganya mkewe kiwembe akakichukuwa kisha na kumchinja mkewe shingoni. Watu wa mwanamke waliposikia mtoto wao kauliwa hawakukubali wakataka kuchukuwa kisasi wakenda kumuuwa yule mume. Vile vile watu wa Mume nao hawakukubali wakataka kuchukuwa kisasi.  Ikabidi makabila mawili yapigane siku nyingi kwa sababu ya kijana mwenye sifa ya namima.

Subhana Llaah! Nadhani ndugu msomaji baada ya kisa hiki sina haja ya kurefusha sana katika mada hii. Hayo ndio madhara ya namima. Kheri yote huondoka katika nyumba yenye mtu kama huyo. Waislamu tahadharini na watu kama hawa. Ewe Mwenyezi Mungu tuepushe nao na utulinde kwa nguvu zako (Amin).

Copyright ©2005  Uislam.net