SAUMU YA NADHIRI

 

Suala1: Nini jawabu lenu juu ya mtu aliyetia nadhiri ya kufunga mwezi mzima, je anaweza akafungua katikati ya huo mwezi kisha aka kamilisha?
Jawabu: Ni juu yake kukamilisha mwezi mzima aliotia nadhiri kufunga isipokuwa kwa dharura anaweza kufutari (kufungua), na ikiwa hana dharura ya kufutari(kufungua) katika huo mwezi basi asifutari(asifungue).
 
Suala 2: Mtu ametia nadhiri ya kufunga mwezi mzima, lakini kwa sababu ya dharura (maradhi) hajaweza kufunga huo mwezi. Nini juu (hukumu) yake?

Jawabu: Afunge huo mwezi wakati wowote atakao pata uwezo (atakapo pona maradhi yake) hata baada ya miaka, ikiwa haja weka wakati maalumu wa kufunga huo mwezi aliotia nadhiri kufunga. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).

Na akajibu Shk Ahmed Al-Khalily jawabu jingine:

Ni juu yake asubiri mpaka apate uwezo wa kufunga huo mwezi, akiwa hajapata uwezo (hajapona maradhi yake) na akashindwa kufunga basi alishe maskini mmoja kwa kila siku aliyoshindwa kufunga.  (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).

 

Suala 3: Ametia mtu nadhiri ya kufunga miezi miwili mfululizo (Kwa pamoja), na miezi hiyo ni Rajab na Sahaabani, lakini akajua kuwa haijuzu kuunganisha kufunga Shaabani na Ramadhani. Je anaweza kuchelewesha kufunga mwezi mmoja katika miezi hiyo miwili mpaka imalizike Ramadhani?

Jawabu:Atakae tia nadhiri ya kufunga miezi miwili mfululizo(kwa pamoja), haisihi (haifai) akaitenganisha kufunga miezi hiyo miwili (yaani afunge mwezi kisha afutari ndio afunge tena mwezi wa pili). Na akiitenganisha basi ni lazima alipe (arejee) kufunga miezi hiyo miwili tena. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).

 

Suala4:Nini neno(jawabu) lenu kwa yule aliyetia nadhiri ya kufunga siku mbili juu ya kila mwezi, na kufunga siku mbili katika kila mwezi. Nini tafauti ya hizi nadhari mbili, Mfano, je inamjuzia kujumuisha funga za hizo siku kwenye mwezi mmoja tu?

Jawabu: Ama atakae tia nadhiri ya kufunga siku mbili juu ya kila mwezi, basi afunge siku mbili juu kila mwezi, na atakae tia nadhiri ya kufunga siku mbili katika kila mwezi, basi anaweza kuzijumuisha hizo siku na akazifunga kwenye mwezi mmoja, ikawa anafunga katika kila mwaka siku 24 kwa ajili anahusisha siku mbili za kila mwezi, wala haikatazwi kuzijumuisha zote pamoja. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).

 

Suala5: Aliyetia nadhiri ya kufunga siku moja maalumu (mfano: ametia nadhiri kufunga siku ya jumamosi) kisha hakuifunga, kitu gani kinamlazimikia afanye?

Jawabu: Imesemwa na Ulamaa kuwa afunge siku nyingine mahali pake(badala ya Jumamosi), wengine wakasema imepita saumu ya hiyo siku kwa kupita siku aliyotia nadhiri kufunga, kwa kutegemea kuwa amri ya kulipa jambo sio kama amri ya kutekeleza, kutokana na hivyo inambidi atubu kwa kuto tekeleza nadhiri yake na hamna jambo jingine juu yake. Lakini rai ya Ulamaa ya mwanzo ndio bora kuifuata (afunge siku nyingine mahali pake) (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).

 

Suala 6:Atakae tia nadhiri ya kufunga siku baada ya siku, kama vile mtu kusema: (Nimetia nadhiri juu ya Mwenyezi Mungu nifunge Jumamosi na Jumapili na jumatatu), kisha akafutari (akafungua) katika siku ya pili (jumapili). Nini inamlazimikia?

Jawabu: Akifungua kwa sababu ya dharura inamlazimikia ailipe hiyo siku, ama akifungua bila ya dharura inamlazimikia azifunge tena siku zote tatu kama alivyozitilia nadhiri (alivyozipanga) (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).

 

Suala 7: Je yule aliyefunga saumu ya nadhiri afungue akitaka kusafiri, kisha ailipe hiyo siku akirejea kutoka safarini?

Jawabu:Kuna khilafu katika kufunga nadhiri, je inajuzu kufutari(kufungua) nadhiri hiyo katika safari, na atakae jilazimishia kitu basi amelazimishiwa hicho kitu, Ama waliokubali afungue akiwa safarini wamesema saumu ya nadhiri si nzito (muhimu) kama saumu ya ramadhani ambayo mwenyezi mungu ameifaradhisha na Mwenyezi Mungu ametoa ruhusa mtu afungue akiwa safarini.  (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).

 

Suala 8: Nini neno (jawabu) lenu, kwa yule aliyeshindwa kufunga nadhiri kwa sababu au bila ya sababu yeyote ile? 
Jawabu:Ikiwa ni kutoweza kwa wakati maalumu (mfupi), basi asubiri mpaka apone kisha afunge. Ikiwa kutokuweza kwa kuendelea maradhi bila ya kupona basi alishe maskini mmoja kwa kila siku aliyotia nadhiri kufunga.  (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).