Mayatima
فأما اليتيم فلا تقهر * وأما السائل فلا تنهر * وأما بنعمة ربك فحدث*
Basi yatima usimwonee! Na anaye omba au
kuuliza usimkaripie! Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie.
Ndugu zangu Waislam.
Katika hekima kubwa za Mola wetu Mtukufu ulimwenguni ni kuwafadhilisha baadhi ya viumbe katika maisha yao wakawa bora kuliko wengine kimaisha. Lakini baada ya mafadhilisho hayo haimaanishi kwamba kila mmoja baina yetu ayatazame yake bila ya kushughulika na wenzake. Ndio Sheria tukufu ya Mwenyezi Mungu ya Kiislam ikaamrisha Wafuasi kushikamana na kuzibiana mapengo ili kusipatikane uwazi katika maisha ya waislamu. Wote wawe kitu kimoja wasaidiane na kupendane.
Na katika jambo moja kubwa ni huku kuwasaidia Mayatima na kuwashughulikia..
Nani Yatima?
Yatima ni mtoto ambaye kafiliwa na baba yake angali bado yeye ni mdogo, mzazi huyo akiwa baba . Ndio mtoto kama huyu katika Uislamu anatakiwa aridhishwe na atendewe yale ambayo huwenda atayakosa kutoka kwa wazazi wake waliomzaa. Aonewe huruma apendwe. Na wamefuzu wale ambao watachukuwa jukumu na kuwalisha na kuwavisha.. Jee Ndugu yangu Muislamu ikiwa leo wewe
utaondoka katika Ulimwengu huu.. Na kama una watoto wachanga nani unadhani atawahudumikia isipokuwa waislamu wenzio. Basi jitahidi haraka uwe na budii katika kulifanya jambo hili la kuwanusuri mayatima.
Bwana Mtume (S.A.W) Kausia sana mayatima mpaka alifika kusema: (Mimi na mwenye kumkafili yatima basi tuko majirani peponi). Ndugu yangu thawabu kubwa kuzipata mja pale anapotowa au anasamehe kwa alichonacho ili kwa kuwakumbuka Wasilamu wenzake wanyonge wasiokuwa na kitu. Basi na tufanye bidii na kushirikiane katika kuimarisha ibadi hii.
Maelezo zaidi wasiliana na www.uislamu.net
email: uislamu@hotmail.com
AL – ISTIQAAMA AL – KHAIRIYA
A/C.NO: 03 – 513397 – 03
Oman International Bank (SAOG)
Mina Al- Fahal (MNF)
SULTANATE OF OMAN



