|
Anasema Mwenyezi Mungu aliyetukuka:
ÃÞã
ÇáÕáÇÉ áÏáæß ÇáÔãÓ Åáì ÛÓÞ Çááíá
æÞÑÂä ÇáÝÌÑ Åä ÞÑÂä ÇáÝÌÑ ßÇä ãÔåæÏ" ÇáÅÓÑÇÁ78
“Shika Sala jua linapo pinduka mpaka giza la usiku, na
Qur'ani ya al fajiri. Hakika Qur'ani ya alfajiri inashuhudiwa daima”Israa
78
Na akasema:
ÍÇÝÙæÇ Úáì
ÇáÕáæÇÊ æÇáÕáÇÉ ÇáæÓØí æÞæãæÇ ááå ÞÇäÊíä" ÇáÈÞÑÉ238
“Zilindeni Sala, na khasa Sala ya katikati, na simameni kwa
ajili ya Mwenyezi Mungu nanyi ni wenye kunyenyekea”Al-Baqara
238.
Amesema Mtume (SAW): “Funguo za pepo ni sala, na
funguo za sala ni tahara”
Na akasema pia: “Hakika malaika wanamuombea mmoja
wenu dua akiwepo juu ya msala aliosalia ikiwa hajatengua udhu.Ewe Mola
mghafirilie madhambi yake, ewe Mola mrehemu”
Yanagawanyika matendo ya sala
katika vipengele viwili navyo ni:
(A) Matendo ya Nyoyo
(Moyo).
(B) Matendo ya viungo vyote vya mwili.
(A)
Matendo ya Nyoyo (moyo) nayo ni:-
1. NIA: Na pahali pake ni moyoni, nako ni
kutia nia moyoni (Kuhakikisha kwa moyo), kuwa unatekeleza faridha ya sala ,
kwa kumtii Mwenyezi Mungu.
Amesema Mtume (SAW): “Hakika matendo ni nia, na kila
tendo ni lile ulilolitilia nia”.
2. IKHLAS (Mtakaso): Nako ni yule mwenye
kusali kufanya ikhlas (kumtakasa Mola) juu ya matendo yake yote, na maneno
yake yote anayo yanena (anayo yasema), juu ya Mwenyezi Mungu. Na sala bila
ya ikhlas inakuwa ni kumdanganya Mwenyezi Mungu.
íÞæá Çááå ÊÚÇáì: "æ ãÇ ÃãÑæÇ ÅáÇ
áíÚÈ쾂 Çááå ãÎáÕíä áå ÇáÏíä" ÇáÈíäÉ 5
“Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi
Mungu kwa kumtakasia Dini" Al-Bayyina 5.
3. UNYENYEKEVU: Ndio
roho ya sala, na sala bila ya unyenyekevu ni sala yenye udanganyifu juu ya
Mwenyezi Mungu. Unyenyekevu ndio nguzo ya sala.Amesema Mtume (SAW): “Kila
kitu kina nguzo, na nguzo ya dini ya kiislamu ni sala, na nguzo ya sala ni
unyenyekevu”. Na njia ambazo zinasaidia kuwa na unyenyekevu: Ni kutakasa
maneno, kutukuza ufalme wa Mola, na kuwa na yakini ya ukamilifu, na
kukusanya hima juu ya ibada.
(B)
Matendo ya viungo vya mwili wote:
1. KUSIMAMA: Nako ni kusimama sawasawa bila
ya kuelemea upande mmoja au kulega lega. Na yawe macho yameelekea pahali
unaposujudu au baina ya pahali unaposujudu na sehemu za miguu.
2. TAWJIYH: Sifa yake ni mwenye kusali aseme:
(SUBHAANAKA LLAHUMA, WABIHAMDIKA, TABAARAKA S’MUKA, WATAALA JADUKA, WALA
ILAHA GHAIRUKA. INNI WAJJAHTU WAJHIYA LILLADHI FATTARA SAMAAWAATI WAL ARDHA
HANIIFAN WAMAA ANAA MINA L’MUSHRIKIIN).
3. TAKBIRAT AL-IHRAAM (Takbira ya kuingia kwenye
sala): Nayo ni nguzo katika nguzo za sala. Na sala haitimii bila ya hiyo
Takbira. Sifa yake ni yule mwenye kusali kusema: (ALLAHU AKBAR).
4. ISTIADHA ( Kujikinga na Shetani) : Nako ni
kumuomba Mwenyezi Mungu akulinde na shetani, na inakuwa baada ya TAKBIRAT
AL-IHRAAM na kabla ya kuisoma Surat Al-Fatiha (Al-Hamdu) katika rakaa ya
mwanzo peke yake. Na sifa yake ni kusema (AUDHU BILLAHI MINA SHAYTANI
RRAJIYM).
5. KUSOMA SURAT AL-FATIHA : Nayo ni nguzo
katika nguzo za sala, na inamuajibikia mtu kuisoma katika rakaa zote za sala,
ikiwa anasali peke yake au anasali sala ya jamaa (maamuma). Na sala haitimii
bila ya kusoma sura hii, dalili ni hadithi ya Mtume (SAW): Hakuna sala ila
kwa kifunguzi cha kitabu (Surat Al-Fatiha).
6. KUSOMA SURA(baada ya
surat Al-Fatiha): Nayo ni Sunna, na unasoma sura katika sala ya
faridha, isipokuwa rakaa kumi na moja za sala ya faridha. Nazo ni: Rakaa nne
za sala ya faridha ya Adhuhuri. Rakaa nne za sala ya faridha ya Al-Asr.
Rakaa ya mwisho ya sala ya Maghrib. Rakaa mbili za mwisho za sala ya Ishaa
ya mwisho. Sala zote za Sunna na za Nafila unasoma sura katika rakaa zote za
sala.
7. RUKUU: Sifa yake ni mwenye kusali
kupinda(kuinamisha) mgongo wake, kwa kutamka Takbira (ALLAHU AKBAR), kuweka
mikono yake juu ya magoti yake hali ya kuwa vidole vyake vimetengana, aweke
mgongo wake sawasawa, na huku anasema (SUBHANA RABIYA L’ADHYM X 3). Idadi
ndogo ya tasbih anayoisema mwenye kusali katika rukuu ni mara tatu. Kisha
anainuka (anasimama) kutoka kwenye rukuu mpaka viungo vyote vya mwili
virejee mahali pake, huku anasema (SAMIA LLAHU LIMAN HAMIDAH) ikiwa ni Imam
au mwenye kusali peke yake. Akisha simama sawasawa anasema (RABBANAA WALAKA
L’HAMD). Na ikiwa mwenye kusali ni maamuma hasemi (SAMIA LLAHU LIMAN HAMIDAH),
bali anamfuata imamu kwa kusema (RABBANAA WALAKA L’HAMD).
8. SIJDA: Sifa yake ni kwenda mwenye kusali
kwenye sijda (kuinamisha kichwa chini mpaka kiguse ardhi) huku anasema (ALLAHU
AKBAR), wakati anatanguliza magoti yake, kisha mikono yake, kisha
anakutanisha (kuambatanisha) pamoja vidole vyake vya mikono, huku vinaelekea
Qibla. Na aweke mikono yake baina ya magoti na masikio, na ncha za vidole
ziwe katika masikio. Kisha anaweka kipaji cha uso na pua yake kwenye ardhi,
na aweke miguu yake sawa sawa mpaka tumbo za vidole vyake vya miguu viguse
ardhi, hali ya kuwa anategemea nguvu za vipaji vyake vya mikono yake kwenye
sijda yake. Na mwenye kusali anasema katika sijda yake (SUBHANA RABBIYA
L’AALA X 3). Idadi ndogo ya tasbih anayoisema mwenye kusali katika sijda ni
mara tatu.
9. KUKAA KITAKO: Nako ni mwenye kusali kukaa
kitako sawa sawa na kuunyoosha mgongo sawa sawa, huku amekalia mguu wake wa
kushoto na kunyoosha mguu wa kulia huku tumbo za vidole vyake vinagusa ardhi.
Na viganja vya mkono wa kulia vinakaa juu ya goti la kulia na viganja vya
mkono wa kushoto vinakaa juu ya goti la kushoto.
10. TASHAHHUD (TAHIYAT) YA
KWANZA: Nayo ni sunna katika sunna za sala. Sifa yake ni yule mwenye
kusali kusema: Attahiyyaatu lillahi wassalawaatu wattayyibaatu. As’salamu
alayka ayyuha nnabiyyu warahmatu llahi wabarakaatuh. As’salamu alayna wa
alaa ibadi llahi ssaalihin. Ash’hadu an’laa Ilaaha illa llah wa ash’hadu
anna Muhammadan abduhu warasuluh.
11. TASHAHHUD (TAHIYAT) YA MWISHO: Anazidisha baada
ya maneno ya Tashahud ya mwazo maneno yafuatayo: Allahuma Sali alaa Muhammad
wa alaa aali Muhammad kama sallayta alaa Ibrahim wa alaa aali Ibrahim,
wabaarik alaa Muhammad wa alaa aali Muhammad kama baarakta alaa ibrahim wa
alaa aali Ibrahim fil aalamina innaka hamiidun majiid.
Baada ya Tashahud ya mwisho na kabla ya kutoa salaam: Zimekuja riwaya za dua
juu ya Mtume Muhammad (SAW), inatakikana mwenye kusali aziombe kabla ya
kutoa salaamu (kumaliza sala). Nazo ni: Allahuma inni audhubika min adhaabi
l-qabri, wa audhubika min adhabi jahannam wa audhubika min fitnati l’masihi
ddajjal, wa audhubika min fitnat l’mahya wal mamaat, wa audhubika mina
l’ma’atham wal’maghram. Allahuma innii dhalamtu nafsii dhulman kathiyra,
walaa yaghfiru dhunuuba illaa anta, faghfir liy maghfiratan min indik.
warhamnii innaka anta l’ghafuru rrahiym. Allahuma ighfir lii maa qadamtu
wama akkhartu wa maa asrartu wa maa aalantu wa maa asraftu wa maa anta
aalamu bihi minni anta l’muqadimu wa anta l’muakhir, la ilaaha illaa ant.
Allahuma innii as’aluka l’jannata wa audhubika mina nnaar.
TASLIIM (KUTOA SALAAM):
baada ya kumaliza hizi dua, anatoa salaam mwenye kusali akisema (ASSALAMU
ALAYKUM) huku anaelekeza uso wake upande wa kulia, kisha anasema (WARAHMATU
LLAHI) huku anaelekeza uso wake upande wa kushoto. Pia kuna kauli kuwa kutoa
salamu mbili inafaa. Anasema mwenye kusali akitoa salamu: (Assalamu Alaykum
Wa Rahmatullah), huku anaelekeza uso wake upande wa kulia. kisha anasema (Assalamu
Alaykum Wa Rahmatullah), huku anaelekeza uso wake upande wa kushoto.
Dua (adhkaar) zilizothibiti kusomwa (kuombwa) baada
ya kutoa salaam: Inatakikana mwenye kusali baada ya kutoa salaam (akimaliza
kusali) aelekee kwa Mwenyezi Mungu kwa kuomba dua.
Zifuatazo ni baadhi ya dua zilizothibiti juu ya
jambo hili:
● Kusoma AYATU L’KURSI.
● kusoma SURATI L-FALAQ na SURATI NAAS.
● Subhaana llah (mara 33), Al-hamdulillah (mara 33),
AllahuAkbar (mara33 au mara34). Unasema baada ya kukamilisha. La Ilaaha illa
llahu wahdahu laa shariyka lah, lahu l’mulku wa lahu l’hamdu wa huwa alaa
kuli shay’in qadiyr (mara 100).
● Astaghfiru llahu l’adhiym wa atuubu ilayhi (mara
3).
● Allahuma anta ssalaam wa minka ssalaam tabarakta
yadha l’jalaal wal’ikram.
● La Ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariyka lah,
lahu l’mulku wa lahu l’hamdu wa huwa alaa kulli shay’in qadiyr. Allahuma la
maani’a
lima aatayta wala
mu’uttiy limaa mana’ata, wala raadda limaa qadhayta walaa yamnau dha l’jiddi
minka l’jadd.
● Allahuma ghfir lii maa qadamtu wamaa akhartu wamaa
asrartu wamaa aalantu wamaa asraftu wamaa anta aalamu bihi minni, anta
l’muqadimu wa anta l’muakhiru laa Ilaaha illaa anta.
● La Ilaaha illa llahu wahdahu laa shariyka lah,
lahu l’mulku wa lahu l’hamdu wa huwa alaa kuli shay’in qadiyr. Walaa hawla
walaa quwata illaa billaah, wala na’abudu illaa iyyah, lahu niimatu walahu
l’fadhlu walahu thanau l’husna la ilaha illa huw, mukhlisiyna lahu ddiin
walaw kariha l’kaafiruun.
● Allahuma ainniy alaa dhikrika wa shukrika wa husni
ibaadatik (mara 3).
● Rabii qinnii adhaabak yawma tab’ath ibaadik.
● Allahuma innii audhubika mina l’jubni wa audhubika
min ardhali l’umr wa audhubika min fitnati dduniya, wa audhubika min adhaabu
l’qabr.
● Allahuma ajirni mina nnaar (mara 7 baada ya Al-Fajr
na Al-Maghrib)
● Allahuma inni as’aluka I’lman naafia, wa amalan
mutaqabala warizqan tayyiba (mara 3 baada ya Al-Fajr)
Imefasiriwa na: Ahmed bin Saif Al-Harthy.
|