Soma makala tofauti

Hijabu ya Mwanamke

Dini ya Haki

Umuhimu wa Elimu

Kutoa Zaka

Kumshabisha Allah

Matendo ya Salaa

Aina za Najasa

Hatari ya kula Riba

Kifo cha punda

Ndoa ya Waliozini

     Nguvu na Haki
 Cheo cha Mtume       
  Unyanyapa ni nini?     
    Kusemana
      Namima
 
 
 
 

 

Makala Yaliyopita

 

Alhamdulilah Rabil-Aalamin. Baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumtakia rehma Bwana Mtume S.A.W na kuwatakia Radhi Masahaba zake wote, na kila atakefuata mwendo wao mpaka siku ya malipo.

Ama Baad:

Wasomaji watukufu  wa mtandao huu wa uislam.net idara yetu inatowa shukurani za dhati na kuwapongeza, na Wallahi kazi hii haiwezi kwenda mbele ila kwa kusaidiana na kupeana mawazo ya kupeleka Daawa mbele. Na moja katika kazi hiyo ni kutuandikia makala mbali mbali ambayo huleta faida kubwa kwa wasomaji wengine, Ndugu zetu musichoke kutuandikia makala mema, huwenda kalamu yako ikaleta baraka katika maneno unayoyandika kutoka moyoni mwako kwa ajili ya kuelimisha wengine.

Kisha jambo la muhimu kuzingatia kwa wale ndugu zetu ambao huchukuwa makala katika ukumbi huu, tuna furaha sana inapochukuliwa makala na kutolewa  kopi ili na wengine wafaidike, lakini tusisahau kwamba makala hiyo haikuja hivi hivi tu, bali kwa juhudi ya mwandishi wake, kwa hivyo ni vyema unapochukuwa makala unukulu wapi umeyatowa na kuweka jina la mwandishi. au kama hakuna mwandishi basi andika tu kutoka katika uislam.net. Ili kama kuna chochote kilichokosewa wewe usichukuwe jukumu.

Mwisho: Tunatowa shukurani za dhati kwa kila ambaye anachangia katika kazi hii tukufu. Na kila mtu anachangia kuendesha mbele uislamu kwa kadiri anavyoweza. usijidharau ukaona kwamba huna la kuchangia, Laa sivyo hivyo. Kila mmoja wetu ni masuuli katika kazi hii ya kutangaza Dini. Tafadhali ukiona kosa au unataka kutoa rai au nasaha, tutafurahi sana, kwani binaadamu tuna upungufu wa maarifa na aliyekamila ni Allah Pekee.

Shukran.

 

Email: uislamu@uislamu.net

 

 

 

Copyright ©2005  Uislam.net