MAFANIKIO NA MAHITAJIO

 

Unguja na Pemba zimefunguliwa madarasa za kiarabu na dini. Kiasi ya madrasa 95, na zaidi ya walimu 100 wote wanataka kulipwa. Kila mwalimu analipwa kiasi ya dola 30 kwa mwezi hivyo msaada wenu tunauhitaji asikose mmoja wenu kumdhamini mwalimu mmoja.

Ujenzi wa Maahad ya Istiqaama ushafika nusu mpaka hivi sasa, bado nusu ya pili na kumaliza kwake ni kheri yetu sote, kwa hivyo unaombwa utowe mchango wako kadiri ya uwezo wako ili ikamilike na wewe upate kuandikiwa sadaka jaria.

Maahad ya Istiqaama iliofunguliwa Unguja Iko Tunguu inaendelea kuchukuwa wanafunzi kutoka kila Mkowa wa Tanzania na pia nchi jirani . Pesa zinazohitajika kila mwezi zinakaribia dola elfu kumi na nne ( $14000/-) .

Katika hiyo Maahad imefunguliwa skuli ya kisasa ambayo wanafunzi watasoma masomo yote ya kiserekali na pia mafunzo ya kiarabu na dini kwa jumla. Tumeanza kuchukuwa wanafunzi kutoka chumba cha kwanza na itakua imefunguliwa kwa ajili ya wanafunzi wa kiislamu kutoka Tanzania na nchi karibu. Mwanafunzi anatakiwa kulipa fees ambayo hatakuwa kubwa.

Fees kwa kila mwanafunzi ni $35/-kwa kila mwezi

Ukitaka kutuma mchango wako wa kumsponsa mwanafunzi au kuchangia katika ujenzi tumia  Banki ya OIB Al-Istqaama Al-khairiya A/C 12-057808-03 Madinat Al-Nahdha Branch.

Pia mwelekeo wa sasa ni kufunguwa shule kama hii kila Mtaawi ya Istiqaam kama:

Pemba: Karibu tutaanza katika ujenzi wa shule na ukitaka kuchangia katika ujenzi, tumia  Banki ya OIB Al-Istqaama Al-khairiya A/C          12-057808-02 Madinat Al-Nahdha Branch. Pesa zitatumika katika ujenzi, mishahara ya walimu wa madaris za Qur'n na ujenzi wa shule na mengineo.

 

Uganda Bugiri: Karibu tutaanza katika kuanza ujenzi wa secondary  na ukitaka kuchangia katika ujenzi, tumia  Banki ya OIB Al-Istqaama Al-khairiya A/C 12-057808-01 Madinat Al-Nahdha Branch.

Pia katika akaunti hii tunapokea mchango wenu kwa ajili ya mishahara ya walimu, kusponsa mwanafunzi, uchimbaji wa visima huko Uganda na mengineo.

 

Ujenzi wa skuli ya secondari Mpanda Mkowa wa Rukwa pia ushafika mbali wanaomba msaada wetu kifedha na pia anaetaka kuuzuru mradi huu halmashauri ya Istiqaama ilioko huko iko tayari kumpokea yeye na rai zake.

 

Ujenzi wa primary school ya Chumbageni Tanga karibu itaanza lakini pesa za ujenzi bado hazijakamilika, tinaomba msaada wenu.

Ukitaka kutuma mchango wako tumia  akaunti ya Al-Istiqama Al-Khaiyriya Alukhwer branch A/c 08-440661-01

Maendeleo ya madaris na misikiti katika mikoa ya Bukoba na Tabora zinaendelea vizuri sana na imebidi kufungua hesabu za benki kwa ajili ya tawi hizo mbili nazo ni:

Mkua wa Tabora:

Akaunti yake ya benki ni: Al-Istiqama Al-Khaiyriya Alukhweir branch A/c   08-440661-02

 

Mkoa wa Kagera:

Akaunti yake ya benki ni: Al-Istiqama Al-Khaiyriya Alukhweir branch A/c 08-440661-03

 

Pia Jumuiya hii ishaanza kupeleka wataalamu katika baadhi ya Matawi ya jumuiya ili kufanya study ya kujenga primary schools kwa ajili ya maendeleo ya watoto wetu kielimu na kupata akhlaki za kiislamu.

Maendeleo ya madrasa za dini na kiarabu Mikoani Bara zinaendelea vizuri mchango wenu unangojwa ili yapatikane mafanikio mazuri.

 2.Jumuiya ya waarabu wa KI OMANI Burundi na matawi yake: ROMONGE KITEGA,KIRUNDO,NGOZI NA RUYIGI. Jumuiya hii inadhamiria kujenga primary na secondari school na sisi tunatakiwa sote tushirikiane nao kifedha. Wanachama wa Jumuiya hiyo wamejitahidi kujenga maduka ni mradi wa kuingiza pesa za kuendeshea kazi za msikiti wao, na pia wemejenga maktaba kubwa na vitabu pamoja na mahitajio mengine vimepelekwa na Jumuiya.

Ujenzi wa maktaba katika Tawi la Gitega imesimama kutokana  na upungufu wa pesa, kwa hivyo tunaombwa sote tushirikiane nao.

3.Jumuiya ya waarabu wa KIOMANI RWANDA na matawi yake: BUTARE, RWAMAGANA na KIGALI . Ndugu zetu hawa wanania ya kujenga misikiti mitatu mmoja Kigali, mmoja Butari na mwengine Ruwamagana Pamoja na madarasa ya kusomesha Dini na Lugha wanaomba msaada wenu.

 

 4. Jumuiya ya Istiqaama Ghana na matawi yake Acra, Wenchi, Kumasi, Wa, Bandankwanta, Budu, Subinsu, Sinyani, Kintanbu zinaendelea kuimarisha kazi za Istiqaama na Jumiya imeweza kuwasaidia katika ujenzi wa misikiti miwili na madarasa ya dini na lugha ya kiarabu na skuli ya primary na secondary na Maktaba na kufundisha ushoni kwa wanawake, pia imewezekana kuwanunulia Ardhi ya ziraa ili waweze kuiamirisha kwa ajili ya chakula ya wananchi masikini.

5. Jumuiya ya Istiqaama Mali na matawi yake Wanahitaji misikiti miwili kila msikiti utagharimu $35000/- pia shule itagharimu $40000/-

Angalia: -

Hii juhudi tunayochukuwa kwa upande wa pili ni kupigana na Mayahudi na Manasara, ambao wanaingia kwa juhudi kubwa katika jamii ya Kiislamu . Mfano wahayo ni kuanzisha skuli za malezi (nursery) ambao wanawafundisha watoto wa kiislamu kuwa yesu ni bora kuliko Nabii Muhammad na mengineo ya upotefu.

Pili wananunuwa ardhi za Waislamu kwa bei kubwa na kujenga makanisa.

Tatu wanatoa misaada kwa masikini kama kuwalea wazee na kujenga spitali kwa malipo madogo sana.

Nne wanatoa vipindi vya mafunzo ya dini yao katika radio na TV.

Ili Waislamu waweze kujilinda na dhamiri zao hizi ni jukumu letu kuwaokoa ndugu zetu huko kwa hali na mali , na kujiokoa nafsi zetu siku ya hesabu.

 

Copyright ©2004  Uislam.net