|

MAANA YA
SAUMU
Saumu imehusiwa
jambo muhimu ambalo halipo katika ibada
nyinginezo kuwa ukweli wa hiyo Saumu kwa mwenye
kufunga hakuna anaoujua isipokuwa Mwenyezi Mungu
(Subhanahu Wa Taalah) kwa hivyo Amesema
Subhanahu Wa Taalah:
( الصوم لي وأنا أجازي به الجنة )
“Saumu ni yangu
mimi na mimi namlipa (huyo anaefunga) kwa hiyo (Saumu)
Pepo”.
Na juu ya kuwa
Ibada zote ni zake yeye tu Mwenyezi Mungu (Subhanahu
Wa Taalah) (lakini imestitiziwa kwa daraja kubwa
iliyopewa kwani mtu aweza kudai amefunga lakini
akiwa peke yake huenda akala au akanywa kwa
hivyo ukweli wake anaujua Subhanahu Wa Taalah
pekee). Na katika hekima zake kuwa inaondoa
maradhi na inasafisha akili na hutia nuru katika
undani wa mwili (yaani moyo ukipata nuru
anaepukana mtu ni riyaa, hasadi, chuki, kibri
etc) na humpa mtu nguvu ya kufanya ibada na
huizowesha nafsi kuhimili njaa ili iweze
kusubiria mashaka ya maisha, na kadhalika Saumu
humfanya mtu aweze kupigana vita na magonjwa ya
nafsi na kumtakasa nayo na kumfanya awe na
huruma juu ya mafakiri na wenye shida.
Kuhusishwa Saumu na Mwezi wa Ramadhani ni kwa
ajili ya kuhuyisha kumbu kumbu ya kuteremka kwa
Qur'an ili iwe uongozi kwa watu, na hoja zilizo
wazi za uongozi na upambanuzi (wa baina ya haki
na batili) na ni kitu cha tabia kwa watu wa
Qur'an kuisherehekea kumbu kumbu hii na
kujikaribisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kuishukuru
neema hii yenye kulinda mabaya.
Saumu maana yake
katika lugha ni kukamata (kuzuia) na maana yake
katika Sheria ni kuzuiya yafikayo ndani ya mwili
kutoka nje yake na jimaa na madhambi makubwa kwa
kutiya niya kutoka Al-Fajiri mpaka kuzama jua (Magharibi)
kwa kauli ya Mwenyezi Mungu (Subhanahu Wa Taalah)
:-
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ
كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى
الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ
(183) أَيَّامًا مَّعْدُودَاتٍ فَمَن كَانَ مِنكُم
مَّرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ
أَيَّامٍ أُخَرَ وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ
فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ فَمَن تَطَوَّعَ
خَيْرًا فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ وَأَن تَصُومُواْ
خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ
(184)
شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِيَ
أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ
وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ فَمَن
شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن
كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ
أَيَّامٍ أُخَرَ يُرِيدُ اللّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ
وَلاَ يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُواْ
الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُواْ اللّهَ عَلَى مَا
هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ (185)
وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي
فَإِنِّي قَرِيبٌ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا
دَعَانِ فَلْيَسْتَجِيبُواْ لِي وَلْيُؤْمِنُواْ
بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ (186)
أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ
الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَى نِسَآئِكُمْ هُنَّ
لِبَاسٌ لَّكُمْ وَأَنتُمْ لِبَاسٌ لَّهُنَّ
عَلِمَ اللّهُ أَنَّكُمْ كُنتُمْ تَخْتانُونَ
أَنفُسَكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ وَعَفَا عَنكُمْ
فَالآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُواْ مَا كَتَبَ
اللّهُ لَكُمْ وَكُلُواْ وَاشْرَبُواْ حَتَّى
يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الأَبْيَضُ مِنَ
الْخَيْطِ الأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ثُمَّ
أَتِمُّواْ الصِّيَامَ إِلَى الَّليْلِ وَلاَ
تُبَاشِرُوهُنَّ وَأَنتُمْ عَاكِفُونَ فِي
الْمَسَاجِدِ تِلْكَ حُدُودُ اللّهِ فَلاَ
تَقْرَبُوهَا كَذَلِكَ يُبَيِّنُ اللّهُ آيَاتِهِ
لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ (187)
سورة البقرة
(Aya ya 183 – 187
ya sura Al-Baqarah)
Enyi Mlioamini
mmelazimishwa kufunga (Saumu) kama
walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate
kumcha Mungu (183) Siku chache tu (kufunga huko).
Na atakayekuwa mgonjwa au katika safari (akafunga
baadhi ya siku) basi atimize hisabu katika siku
nyingine. Na wale wasioweza, watoe fidia kwa
kumlisha masikini. Na atakayefanya wema kwa
radhi ya nafsi yake, binafsi ni bora kwake. Na
huku kufunga ni bora kwenu ikiwa mnajua (haya
sasa basi fuateni) (184) (Mwezi huo mlioambiwa
mfunge) ni Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa
katika (mwezi) huo hii Qur'an ili iwe uongozi
kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongozi na
upambanuzi (wa baina ya haki na batili).
Atakayekuwa katika mji katika huu mwezi (wa
Ramadhani) afunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au
safarini, basi (atimize) hisabu (ya siku
alizowacha kufunga) katika siku nyingine.
Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala
hakutakieni yaliyo mazito, na pia (anakutakieni)
kumtukuza Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongozeni,
ili mpate kushukuru (185) Na waja wangu watakapo
kuuliza hakika yangu (waambie kuwa) Mimi niko
karibu nao. Naitika maombi ya mwombaji
anaponiomba. Basi na waniitikie na waniamini,
ili wapate kuongoka (186) Mmehalalishiwa usiku
wa Saumu kuingiliana na wake zenu. Wao ni (kama)
nguo kwenu (zilizokugandeni mwilini) na nyinyi
ni (kama) nguo kwao. Mwenyezi Mungu anajua
kwamba mlikuwa mkizihini nafsi zenu. Kwa hivyo
amekukubalieni toba yenu na amekusameheni. Basi
sasa changanyikeni nao na takeni
aliyokuandikieni Mwenyezi Mungu. Na kuleni na
kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa Alfajiri
katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu
mpaka usiku. Wala msichanganyike nao, na hali
mnakaa Itikafu msikitini. Hiyo ni mipaka ya
Mwenyezi Mungu, basi msiikaribie. Namna hivi
Mwenyezi Mungu anabainisha hoja zake kwa watu
ili wapate kumcha (187).
Na anasema Mtume (Salallahu
Alayhi Wasalam) :
( من صام رمضان إيمانا واحتسابا
غفر له ما تقدم من ذنبه و من قام رمضان إيمانا و
احتسابا و من قام ليلة القدر غفر له ما تقدم من
ذنبه )
Anaefunga Ramadhani
hali yakuwa anaamini (wajibu wa kufunga Mwezi
huu na kuwa ni faradhi juu yake) na atarajia
malipo mazuri (kwa Mwenyezi Mungu) basi
hughufiriwa madhambi yake yote yaliyopita, na
anaesimama (kusali Sala za usiku katika mwezi wa)
Ramadhani hali ya kuwa anaamini na atarajia
malipo mazuri na anaesimama (kufanya ibada)
usiku wa Al-Qadar (Laylatu Al-Qadari)
hughufiriwa madhambi yake yote yaliyopita.
Maana ya
إيمانا
yaani anaamini kuwajibika kwa kitendo hicho
alichokifanya (hapa ni Saumu).
Maana ya
احتسابا
yaani atiye niya kuwa anafanya kitendo hichi kwa
ajili ya Mwenyezi Mungu tu atarajia kwa kitendo
hicho thawabu yake tu bila ya kuwa na lengo
lingine.
Na iwapo
atachanganya niya hiyo pamoja na niya nyingine
haitakuwa
احتسابا
kwa mujibu ya kauli yake Subhanahu Wa Taalah
katika hadithi Qudisiy:-
( من عمل عملا أشرك فيه غيري فهو
له و أنا أغنى الشركاء )
Mwenye kufanya
jambo akamshirikisha ndani yake aliyekuwa
mwengine sie mimi (Mwenyezi Mungu (Subhanahu Wa
Taalah)) basi hilo (jambo) ni lake yeye (huyo
aliyemshirikisha) na mimi sina haja na washirika
(mwenye kutohitajia washirika) na hili ni
shuruti la kwanza na shuruti la pili la
kughufiriwa madhambi (masharti haya mawili
yanayomuwajibikia anayefunga na anaye simama
usiku mwezi wa Ramadhani ili aghufiriwe madhambi
yake yote aliyoyafanya kabla) ni kuwa mwenye
kufunga na mwenye kusali usiku asiwe anaendelea
kufanya dhambi kubwa katika haki za Mwenyezi
Mungu (Subhanahu Wa Taalah) (kama kuacha kusali,
kutoa Zaka au kunywa pombe etc) au kuwadhulumu
waja wake kwani wako wanaofunga na kusali Qiyamu
alleyl na hali bado ameshikilia kufanya madhambi
makubwa na kwadhulumu waja wa Mwenyezi Mungu (binaadamu
wenzake) basi hadithi hiyo juu ya kughufuriwa
madhambi haimkhusu yeye kwa sababu hadithi hii
siyo kwa kila anayefunga na kufanya ibada usiku
na ikiwa hivyo itakuwa kinyume na aqiida ya
Kiislamu ili sahihi.
Na katika hadithi
nyingine inayotoa dalili ya kuwajibika kwa Saumu
ya Ramadhani ni ile hadithi aliyoitoa Salman Al-Faarisiy
R.A. amesema: Ametuhutubia Mtume (Salallahu
Alayhi Wasalam) katika siku ya mwisho wa Mwezi
wa Shaabani akasema:-
(يا أيها الناس قد أظلكم شهر عظيم
شهر مبارك شهر فيه ليلة خير من ألف شهر جعل الله
صيامه فريضة و قيام ليلة طوعا و من تقرب فيه
بخصلة من الخير كان كمن أدى فريضة و من أدى فريضة
فيه كان كمن أدى سبعين فريضة فيما
سواه و هو شهر الصبر , و الصبر ثوابه الجنة , و
شهر المواساة و شهر يزاد فيه رزق المؤمن , من فطر
فيه صائما كان مغفرة لذنوبه و عتق رقبته من النار
, و كان له مثل أجره من غير أن ينقص من أجره شئ ,
قلنا يا رسول الله ليس كلنا يجد ما يفطر به الصائم
فقال رسول الله صلى الله عليه و سلم يعطي الله هذا
ثواب من فطر صائماً على مذقة لبن أ, تمرة أو شرب
من الماء , و من أشبع صائما سقاه الله من حوضي
شربه لا يظمأ حتى يدخل الجنة و هو شهر أوله رحمة و
أوسطه مغفرة و أخره عتق من النار و من خفف عن
مملوكه فيه غفر الله له ما و أعتقه من النار
“Enyi Watu
kimewafunika kivuli cha mwezi mtukufu, mwezi
wenye baraka, mwezi ndani yake kuna usiku ulio
bora kuliko miezi elfu (yaani “Laiylatul Qadri”),
Mwenyezi Mungu amejaalia kuufunga (huo mwezi) ni
faradhi na kusali Sala za usiku (Qiyaamul leyl)
jambo la kujitolea kulifanya (lina malipo mazuri)
na anaejikaribisha kwa jambo la kheri ni kama
aliefanya faradhi na aliyefanya faradhi katika
mwezi huu ni kama aliyefanya faradhi sabiin
katika miezi mingine, nao ni mwezi wa subira na
subira thawabu yake ni Pepo (Al-Jannah) na ni
mwezi wa maliwaza, mwezi inaongezwa ndani yake
riziki ya Muumini, anaemfuturisha ndani yake
mwenye kufunga hughufiriwa madhambi yake na
hukombolewa shingo yake (yaani yeye mwenyewe)
kutoka Motoni na hupata malipo kama malipo yake
(huyo aliyefuturishwa) bila ya kupungua kitu
katika malipo yake, tukasema ewe Mtume wa
Mwenyezi Mungu sio kila mmoja wetu anacho cha
kumfuturishi aliyefunga akasema Mtume (Salallahu
Alayhi Wasalam) : Anampa Mwenyezi Mungu thawabu
hii anaemfuturisha aliyefunga kwa muonjo wa
maziwa au tembe ya tende au funda la maji na
anaemshibisha aliyefunga Mwenyezi Mungu
atamnywesha katika Hodhi langu kinywaji ambacho
(kitamfanya) hatapata kiu mpaka aingie Peponi,
na mwezi mwanzo wake ni Rehema na kati kati yake
ni Maghufira na mwisho wake ni kukombolewa
Motoni na yule anaempunguzia mtumwa wake
Mwenyezi Mungu humghufiria na kumkomboa Motoni”.
Sababu ya kuileta
hadithi kwa kirefu ni kupata faida na huenda
Mwenyezi Mungu (Subhanahu Wa Taalah) akajaalia (miongoni
mwa wasomaji) atakayetekeleza yaliyomo humo na
nitapata mimi sehemu katika hayo malipo kwa
sababu anayeionyesha kheri ni kama yule
aliyoifanya kheri hiyo.
|