|
|
LENGO NA MADHUMUNI YA
JUMUIYA |
Lengo kubwa la Jumuiya ni kujenga na
kuendeleza sekta zake ili kufikia kwenye dhamira yake ya kujenga Taifa imara.
Kwa kutekeleza jukumu hilo, Jumuiya ya
Istiqama International imepania kutumia uwezo wake wote kutekeleza:
a.
Kujenga itiqadi na upeo wa elimu ya utamaduni na silka njema.
b.
Kutilia mkazo umuhimu wa elimu pamoja na kuongeza viwango vya
elimu.
c.
Kusidia na kubuni njia za kuongeza ajira kwa wananchi.
d.
Kusaidia hali
mali kuendeleza sekta za afya kwa jumla na hasa kwa mama na
watoto.
e.
Kupunguza umasikini.
f. Kumuendeleza
mwanamke katika jamii.
Madhumuni ya Jumuiya:
Pia Jumuiya Ina madhumuni mengine kama
ifuatavyo:
1. Kueneza (kufanya daawa) taaluma juu ya
ukweli wa dini ya kiislamu.
2. Kuwaita watu katika njia ya Mwenyezi Mungu
kwa kuwaelimisha juu ya dini yao.
3. Kushirikiana na Jumuiya nyengine za
kiislamu katika kuwasaidia maskini na wahitaji:
"Kushirikiana na kusaidiana katika kumcha na
kumuogopa Mwenyezi Mungu"
|