|
Ni kuizunguka Kaaba kuanzia kwenye Jiwe Jeusi
na kumalizia hapo hapo ili utimie mzunguko wa mwanzo, na hurudiwa mara saba
pamoja na kutamka “SubhaanaLLah walhamduliLLah, walaa ilaaha illa-LLah
waLLahu akbar” na kuomba dua.
VIPI KUTUFU:
*
Tawafu huanza kwa
kulibusu Jiwe Jeusi ikiwezekana; isipowezekana atatosheka na kuligusa au
kuliashiria kwa mkono wake pamoja na kutamka “Allahu Akbar” wakati wa
kulishika.
è Ataanza kutufu na hali
ameifanya Nyumba ya Allah iwe kushotoni kwake.
è
Ataomba dua atakazo
wakati wa kutufu na atasoma “Albaaqiyaatu-ssaalihaatu” yaani “SubhaanaLLah
walhamduliLLah, walaa ilaaha illa-LLah waLLahu akbar”
è
Anapokuwa sawa na Pembe
ya Yamani ataigusa ikiwezekana na hataiashiria
kama hakuweza kuigusa.
è Akifika kwenye Jiwe
Jeusi mzunguko wa kwanza unakuwa umemaliza, na atanza mzunguko wa pili
kama alivyofanya mwanzo mpaka atimize mizunguko
saba.
SUNNA ZA TAWAFU:
1. “Ramal”:
Nayo ni kutembea kwa haraka na hatua zinazokaribiana
bila kwenda mbio na kuchupa; hili linasuniwa katika mizunguko mitatu ya
mwanzo.
2.
“Idh-tiba`u”:
Nayo ni kupitisha sehemu ya kati ya shuka
anayojifunika chini ya bega la kulia kwenye kwapa na kuzitupia ncha zake juu
ya bega lake la kushoto, yaani aweke wazi bega lake la kulia. “Idh-tiba`u”
huwa katika mizunguko yote saba.
Tanbihi:
“Ramal” na “Idh-tiba`u” haziwi ila katika tawafu ya “quduum” tu (tawafu ya
mwanzo akifika Maka).
3.
Rakaa mbili
za tawafu: Nazo ni rakaa
mbili zinazosaliwa nyuma ya Maqam ya Nabii Ibraahim - amani imshukie - au po
pote itapowezekana baada ya tawafu. Dalili ya hilo ni hadithi ya Ibnu Umar
Allah amridhie iliyoko kwa Bukhari anasema:
Alikuja Mtume - rehema za Allah na amani zimshukie -
akaizunguka Nyumba ya Allah mara saba kisha akasali
nyuma ya Maqam rakaa mbili kisha akatoka kwenda kwenye Safa,
na Allah Aliyetukuka amesema:
)
لَقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ
اللَّهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ(
{Bila
shaka katika Mtume wa Allah mmekuwa na kigezo kizuri}
[Al-ahzaab 21].
MAZINGATIO
¨
Mwenye kutufu akawa na shaka katika idadi ya mizunguko
aliyozunguka ataendelea kutoka idadi iliyo ndogo kati ya idadi mbili
anazozifikiria, na akiirudia upya tawafu baadae ni vyema.
¨
Mwenye kuingia manukato
anapoligusa Jiwe Jeusi na Pembe ya Yamani bila kukusudia kupata mabaki ya
manukato hayo humo itampasa ayaoshe mwilini na hakitamlazimu kitu kingine.
¨
“Ramal”
kama ilivyo kwa wajao Maka kutoka nje vilevile huwa kwa
wakaazi wa Maka.
¨
Inajuzu kusali rakaa
mbili za tawafu baada ya sala ya alfajiri kabla ya kuchomoza jua na baada ya
sala ya alasiri kabla ya kuchwa jua kwa kauli iliyopewa uzito na wenye ilmu,
kwasababu hiyo ni sala yenye sababu iwapo atatufu katika nyakati mbili hizi.
¨
Rakaa mbili za tawafu
huakhirishwa iwapo ni wakati usioruhusiwa kusali, nao ni nyakati za
kuchomoza jua, kuchwa jua na kuwa katikati ya mbingu kwa jua katika kipindi
cha joto kali isipokuwa siku ya Ijumaa.
¨
Inajuzu kutufu Nyumba
Takatifu wakati imamu anahutubu Ijumaa lakini bora kusubiri.
¨
Mtu asitufu kwenye
tabaka ya pili ya jengo ila isipowezekana kutufu kwenye tabaka ya chini.
¨
Haimlazimu mwenye kutufu
kuvua viatu vyake na anaruhusiwa kuvichukua mkononi au chini ya kwapa vikiwa
nadhifu.
¨
Haitakiwi kutufu juu ya
sakafu ya Msikiti - yaani tabaka ya juu kabisa – kwasababu hawi katika usawa
na Nyumba Takatifu.
¨
Haijuzu kutufu ndani ya
ule ukuta mfupi wa “alhatiim” kwasababu ni sehemu ya Kaaba.
¨
Inajuzu kwa mwenye
kuhiji au kufanya umra anapotufu au anaposai kupumzika katika ibada hizo
akihitaji hilo.
¨
Akitufu au kusai
akaongeza mzunguko mmoja au miwili bila kukusudia hapana kosa juu yake
lakini inapendelewa arudie upya ili kuondoa wasi wasi.
KUSAI BAINA
SAFA NA MARWA
1.
Akikaribia kwenye Safa atasoma
kauli Yake Aliyetukuka:
)
إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن
شَعَآئِرِ اللّهِ(
{Hakika Safa na Marwa ni katika alama za
kuadhimisha dini ya mwenyezi Mungu}
[Albaqara, 158].
2. Atapanda
juu yake mpaka aione Nyumba Takatifu, atakabir mara tatu kisha atamhimidi
Allah, na anapendelewa aseme mara tatu:
"لا
إله إلا الله وحده لا شريك له ، له الملك وله الحمد وهو على كل شيء قدير، لا
إله إلا الله وحده ، أَنْجزَ وعده ونَصَرَ عبده ، وهزمَ الأحزابَ وحده"
“Laa ilaaha il-la-llaahu wa`hdahu laa
shariika lahu, lahul-mulku walahul-`hamdu wa huwa `alaa kulli shay’in Qadiir.
Laa ilaaha il-la-llaahu wa`hdah, anjaza wa`adah, wa nasara a`bdah, wa
hazamal-a`hzaaba wa`hdah”
(Hapana anayestahiki kuabudiwa ila Allah peke
Yake hana mshirika. Ufalme ni wake na Yeye ndiye wa kushukuriwa na Muweza
juu ya kila kitu. Hapana anayestahiki kuabudiwa ila Allah peke Yake.
Ametimiza ahadi Yake, akamnusuru mja Wake na akayashinda makundi ya
washirikina peke Yake).
Kisha ataomba dua atakazo.
3.
Kisha atashuka kuelekea Marwa
huku anamdhukuru Allah Mtukufu, mpaka akifika baina ya alama mbili za rangi
ya kijani atatembea kwa haraka zaidi, na anapendelewa aseme:
"رب
اغفر وارحم، إنك أنتَ الأعزُّ الأكرم"
“Rabbi-ghfir war-`ham, innaka
antal-aa`z-zul-akram”
(Mola wangu samehe na urehemu; hakika Wewe
ndiye Mwenye uwezo mkuu na ukarimu wa juu).
Wanawake haiwapasi kutembea kwa haraka.
4.
Kisha atatembea taratibu huku anamdhukuru
Allah na kumuomba kheri ya duniani na ya akhera mpaka akikaribia Marwa
atasimama juu yake na kufanya kama alivyofanya
juu ya Safa, na kwa hayo atakuwa ameshamaliza duru moja.
5.
Kisha atafanya duru ya pili kutoka Marwa hadi
safa na atafanya kama alivyofanya katika duru
ya mwanzo mpaka atimize duru saba kwa kumalizia kwenye marwa.
6.
Inajuzu
kusai pasina tohara lakini anapendelewa awe katika tohara.
MASHARTI YA SAI:
1)
Iwe baada ya tawafu.
2)
Iwe duru saba.
3)
Ianzie kwenye Safa, imalizie
kwenye Marwa.
MAZINGATIO:
v Wanazuoni
wamehitalifiana kuhusu hukumu ya sai: kuna kauli ni fardhi na kuna kauli ni
sunna. Kwa kauli ya kwanza, atakayeiacha basi hija yake hubatilika, na kwa
kauli ya pili hija yake haibatiliki lakini atawajibika kuchinja, nayo ndiyo
kauli ya wengi wa wanazuoni wa Madhehebu hii.
v
Mwenye kusai kuanzia
marwa na kumalizia Safa kisha akatokana na ihramu itamlazimu arejee kwenye
ihramu yake na atimize sai yake kwa kutoihisabu duru ya mwanzo ambayo
alianzia Marwa hadi Safa, kisha atawajibika kuchinja mara mbili.
v Haikatazwi
kusai upande mmoja kutoka Safa hadi Marwa kwenda na kurudi, kwani ugawaji wa
eneo la sai ni kwa ajili ya kuwepesisha, jambo ambalo halikuwapo hapo kabla,
lakini bora kufuata nidhamu ya mwendo iliyowekwa ili kuondoa msongamano.
v Mwenye
kusai chini ya duru saba na hakukumbuka ila baada ya kutokana na ihramu
itampasa arejee ihramu yake na atimize sai yake kisha itamwajibikia kuchinja.
v Kupanda
juu ya vilima viwili vya Safa na Marwa kunasuniwa kwa wanaume kwa kadri ya
mmoja wao kuiona Kaaba sio kwa wanawake.
v Iwapo
mwenye kusai hakuweza kuisoma dhikri iliyopokewa juu ya vilima viwili vya
safa na Marwa haikatazwi kwake kuisoma wakati anapotembea baina yake.
KUTOKANA
NA IHRAMU YA UMRA:
· Akimaliza
mwenye kufanya umra sai yake atanyoa au kupunguza nywele zake. Kunyoa ni
bora kuliko kupunguza, na izingatiwe kwamba kupunguza lazima kuenee kichwa
chote.
· Baada
ya kunyoa au kupunguza nywele atakuwa ameshatokana na ihramu yake akiwa
mfanya Tamat-tuu. Ama akiwa mfanya Qiraanu hatanyoa ila siku ya kuchinja
kule Mina.
· Yanamhalalikia
mwenye kufanya umra baada ya kutokana na ihramu kila yanayomharamikia
muhrimu isipokuwa kuwinda katika Eneo Takatifu (Al-Haram).
· Mfanya
Tamat-tuu bora kwake kupunguza nywele baada ya kufanya umra, na kunyoa baada
ya kulipiga Jamra Kuu la Aqaba na kuchinja ikiwa nywele zake fupi baina ya
umra na hija.
MAZINGATIO:
¡ Mwenye
kuhirimia hija au umra kisha akavaa nguo iliyoshonwa baada ya kukamilisha
ibada hizo lakini kabla ya kunyoa au kupunguza nywele atalazimika kuchinja.
¡ Hakatazwi
mtu kujinyoa au kujipunguza nywele mwenyewe kwa ajili ya kutokana na ihramu,
lakini inachukiwa kufanya hivyo uchukivu wa kiutakaso akiwapo wa kumfanyia
hayo kati ya wasio wahirimu.
¡ Hazuiwi
muhrimu kumnyoa au kumpunguza nywele muhrimu mwengine, kwani hapana dalili
ya kuzuia, na kuzuia hili kutaleta usumbufu mkubwa, lakini bora yule ambaye
ameshatokana na ihramu amtoe katika ihramu aliye muhrimu.
¡ Mwenye
kutanguliza kunyoa kabla ya kuchinja na kupiga Jamra, kuna kauli kuwa
atayefanya hivyo kwa sahau au kutokujua hana kosa, na kauli hii ndiyo
inayofuatwa katika fatwa, na kuna kauli kuwa atayefanya lo lote kati ya hayo
atalazimika kuchinja.
¡ Haisihi
kwa mfanya Tamat-tuu kutokana na ihramu yake ya hija kabla ya kuchinja
mnyama wake. Ikiwa hakuweza kuchinja siku ya kuchinja (10 Dhulhija) atabaki
na ihramu yake mpaka achinje.
¡ Halitoshi
wanalofanya wengi kati ya watu zama hizi - la kukata nywele kidogo kwa
mwanamme, bali wajibu kupunguza sehemu zote za nywele mpaka ijulikane kuwa
mtu huyo amepunguza nywele zake.
|