KUTOZA ZAKA

 

ALLAH (S.W.T) amejaalia Uislamu usimame katika nguzo tano kwa hikima zake. Nguzo hizi ni wajibu kwa mmoja wetu kwa uwezo wake.

 

NGUZO YA ZAKA:

Zaka imewajibishwa kuwa ni nguzo ya Uislamu kwa wale wote wenye uwezo, na ALLAH ndiye aliyewapa huwo uwezo. Elimu yake ALLAH haina mipaka, kwa hivyo inawafikia wote. Pia kwa hikima yake  ALLAH (S.W.T) amejaalia waja masikini na fukara. Kwa hakika zaka imetajwa mara nyingi katika Qur-aan kama ilivyotajwa sala ili tufahamu umuhimu wake.

JUKUMU LA JUMUIYA YA ISTIQAMA:

Kwa kuwa Jumuiya Istiqaama Al-Khairiya, na shughuli zake zote zimejifunga na sheria zote za Kiislamu, imeamua kushughulikia suala la zaka kikamilifu.Tayari Jumuiya inao uwezo na uzoefu wa muda mrefu katika kugawa zaka.

FAIDA YA KULETA ZAKA ISTIQAMA:

Inajulikana kuwa kila mwenye kutoa zaka anakuwa na jamaa zake na watu wake wa karibu nay eye. Lakini pia kama atagawa sehemu ya zaka yake na kupitisha Istiqama atapata faida kubwa, kwani zitachanganywa pamoja na watu wengi zaidi, na kurejea kwa faida kwa mtoaji kutatokea kila pembe.

Tunatanguliza na kutaraji mashirikiano mema katika kutimiza wajibu wetu na kupata malipo mema kutoka kwa ALLAH KARIMU.

 

AL ISTIQAMA AL KHAYRIA

 

Copyright ©2004  Uislam.net