Madhambi ya ulimi

KUSEMANA

Kasema Mwenyezi Mungu Katika Suratil Hujuraat Aya ya (12):

( íóÇÃóíøõåóÇ ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇ ÇÌúÊóäöÈõæÇ ßóËöíÑðÇ ãöäú ÇáÙøóäøö Åöäøó ÈóÚúÖó ÇáÙøóäøö ÅöËúãñ æóáóÇ ÊóÌóÓøóÓõæÇ æóáóÇ íóÛúÊóÈú ÈóÚúÖõßõãú ÈóÚúÖðÇ ÃóíõÍöÈøõ ÃóÍóÏõßõãú Ãóäú íóÃúßõáó áóÍúãó ÃóÎöíåö ãóíúÊðÇ ÝóßóÑöåúÊõãõæåõ æóÇÊøóÞõæÇ Çááøóåó Åöäøó Çááøóåó ÊóæøóÇÈñ ÑóÍöíãñ)

Maana yake: “Enyi mlioamini jiepusheni sana na kuwadhania watu dhana mbaya, kwani kuwadhania watu dhana mbaya ni dhambi. Wala musipeleleze habari za watu. Wala baadhi yenu wasiwasengenye (wasiwaseme) wengine. Jee! Mmoja wenu anapenda kula nyama ya nduguye aliyekufa? Laa hampendi, basi na haya musiyapende. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Bila shaka Mwenyezi Mungu ni mwenye kupokea toba na mwingi wa kurehemu”.

Ndungu yangu Muislamu tazama ubaya wa kitendo hiki, mpaka Mwenyezi Mungu akakifananisha na kumla nyama mwenzako. Yaana wewe anapokaa ukamsema mwenzako kwa ubaya, basi ni sawa na kumla nyama yake mbichi. Kitendo ambacho kimeharamishwa katika Sheria za Mwenyezi Mungu. Na ni katika madhambi makubwa yanayochumwa na ulimi. Khasa pale wanapokutana watu katika vikao vyao. Na Mtume (S.A.W) kabainisha wazi wazi ubaya wa jambo hili, na akawafafanulia watu ili wajue katika hali gani mtu huwenda akachuma dhambi hii. Katika Hadithi iliyotolewa na Imam Muslim na Tirmidhi na Ahmad na wengineo kwa njia ya Abu Hurairah. Kasema Bwana Mtume (S.A.W):

 ( ÃóÊóÏúÑõæäó ãóÇ ÇáúÛöíÈóÉõ ÞóÇáõæÇ Çááøóåõ æóÑóÓõæáõåõ ÃóÚúáóãõ ¡ ÞóÇáó: ÐößúÑõßó ÃóÎóÇßó ÈöãóÇ íóßúÑóåõ ¡ Þöíáó: ÃóÝóÑóÃóíúÊó Åöäú ßóÇäó Ýöí ÃóÎöí ãóÇ ÃóÞõæáõ ¡ ÞóÇáó: Åöäú ßóÇäó Ýöíåö ãóÇ ÊóÞõæáõ ÝóÞóÏö ÇÛúÊóÈúÊóåõ æóÅöäú áóãú íóßõäú Ýöíåö ÝóÞóÏú ÈóåóÊøóåõ )

Maana yake: “Mnajua nini maana ya (Al Ghayba)? Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake ndie Wajuwae. Akasema (S.A.W): Kumsema ndugu yako kwa yale anayoyachukia. Akaulizwa: Unaonaje ikiwa ndugu yangu anayo kweli yale ninayomsema. Akasema (S.A.W): Ikiwa kweli anayo unayoyasema juu yake ndio hiyo ghaiba (ni kumsema) na kama hana yale unayoyasema juu yake ndio utakuwa umemzuliya uwongo mkubwa.”

Kwa hivyo hata kama kweli ndugu yako Muislam ana sifa fulani si nzuri, wewe wajibu wako kumsitiri wala usimfedheheshe mbele za watu. Kwa mfano mtu kilema au ana upungufu katika maumbile fulani, basi ni haramu kukaa mkamsema kwa sifa zake hizo alizoumbiwa na Mola wake. Jee wewe unamtoa makosa Muumbaji. Jee wewe unaweza kuumba?

Katika Hadithi iliyotolewa na Imam Ahmad ya kwamba: “Mwanamke mmoja aliingia kwa Mtume (S.A.W) na bibi Aisha yupo. Alipotoka yule mwanamke. Bibi Aisha akasema: Mfupi! Mtume (S.A.W) akahamaki sana na kumwambia bibi Aisha: (Umeshamsema). Bibi Aisha akasema: Sikutaja ila sifa aliyonayo. Hapo Mtume (S.A.W) akasema: Ndio, lakini umetaja ile sifa mbaya aliyonayo.”

Watu lazima watahadhari na mambo kama haya. Wengi wetu hatujali nini tunachokisema wala kulifikiria neno. Maisha ya wengi wetu yamejaa maneno kama haya. Kuna wengine hufungua kinywa asubuhi wanapoamka kwa kula nyama za wenziwao. Sikilizeni hii Hadithi kutoka kwa Mtume (S.A.W) kisha tujuwe kwamba kweli wengi wetu wanawasema watu. Hadithi hii iliyopokelewa na Jabir bin Abdillahi Radhi za Mola juu yake kasema:

“Ulipiga upepo unao hafuru  mbaya wakati wa Mtume (S.A.W). Akasema: Kuna watu wanafiki wanawasema waumini, kwa hivyo ndio upepo huu wenye harufu mbaya ukaja”

Waliulizwa Maulamaa ya kwamba mbona upepo kama huu siku hizi haupo tena. Akasema: Upo lakini watu hawauhisi, kwa sababu pua zao zimeshakufa. Kama vile unapoingia katika nyumba inayoanikwa ngozi na kuchunwa. Wewe mgeni utahisi, lakini wale wenyewe hata habari hawana.

Kwa hivyo hii inamaanisha wazi wazi ya kuwa watu wamebobea katika kusemana. Roho zimekuwa chafu. Dhana mbaya imezidi baina ya watu. Waislamu wamekuwa hawana mapendano baina yao. Kila mmoja anamuona mwenzake kama adui. Kusaidiana hawataki, kila mmoja anajitenga na wenzake. Ndio tukafika hali ya kudhalilishwa tukawa wa mwisho hatuna letu moja. Damu yetu imekuwa rahisi katika mikono ya Mayahudi. Hawasemi kitu wakakubaliana. Mambo yao hayendi mbele yakadumu. Maisha yao hayana baraka. La hawla wala Quwata ila billahi. !

Waislamu amkeni. Rudini katika utukufu wenu aliokutakieni Mola wenu. Msipupe huku na kule kama mliokuwa hamna muongozo unakuongozeni.

Turudieni kwa Mola wetu. Tupendane na tuwe kitu kimoja. Ndio tutawashinda Makafiri na kurudisha haki zetu. Tuwache kusemana na kulana nyama baina yetu.

Ewe mwenye kula nyama ya mwezio hukusikia Hadithi ya Mtume. Iliyotolewa na Imam Al Bukhari na Abu Daud. Kasema Mtume (S.A.W):

( áóãøóÇ ÚõÑöÌó Èöí ãóÑóÑúÊõ ÈöÞóæúãò áóåõãú ÃóÙúÝóÇÑñ ãöäú äõÍóÇÓò íóÎúãõÔõæäó æõÌõæåóåõãú æóÕõÏõæÑóåõãú ÝóÞõáúÊõ ãóäú åóÄõáóÇÁö íóÇ ÌöÈúÑöíáõ ÞóÇáó åóÄõáóÇÁö ÇáøóÐöíäó íóÃúßõáõæäó áõÍõæãó ÇáäøóÇÓö æóíóÞóÚõæäó Ýöí ÃóÚúÑóÇÖöåöãú )

Maana yake: “Nilipopandiswa mbinguni niliwapitia watu wana makucha na shaba, huku wakijipara nyuso zao na vifua vyao. Nikamuuliza Jibril, nani hawa? Akasema Jibril: Hawa ni wale watu waliokuwa wakila nyama za watu (wanawasema) na kuwatukana wenziwao.”

WATU WANAOFAA KUWASEMA:

Kuwasema watu ni haramu tena inaleta chuki baina yao. Kwai hatoridhika mwenye kusemwa kama atasikia. Lakini kuna wakati ni lazima kuwatahadharisha wenzako kama kuna shari au jambo la kuwadhuru. Kwa hivyo ikiwa kuna mtu kazi yake kusambaza bidaa au mambo machafu. Lazima watu watahadharishwe na shari ya mtu huyo ili wapate kumjuwa. Lakini isiwe kumsema huko katika sifa za maumbile kama sura yake au nguo zake au kitu kinachomuhusu alichoumbwa nacho. Isipokuwa zisemwe zile sifa zake ili watu waepukane nazo. Na walisema wanavyuoni ya kwamba watu watatu inafaa kuwasema nao ni: Kila mfalme mwenye kudhulumu. Na Mtu aliye Fasik mtenda maasi mbele za watu. Na mwenye kuzuwa bidaa. Katika Hadithi iliyopokelewa na Imam … Kasema Mtume (S.A.W):

 (ÃÐßÑæÇ ÇáÝÇÌÑ ÈãÇ Ýíå áßí íÍÐÑå ÇáäÇÓ)

Maana yake: “Mtajeni mtu mbaya kwa yale mabaya yake. Ili watu watahadhari naye”.

Na kuna Maulamaa wengine wamesema ya kuwa inaruhusiwa kumsema mtu ikiwa mutashitakiana ikiwa kakudhulumu haki yako, kwa hivyo inajuzu kumsema mbele ya hakimu au mfalme kwa ile dhulma aliyokufanyia ili upate haki yako.

Ndugu zangu Waislamu hebu kila mmoja kati yetu ajiulize mara ngapi tunawasema watu au tunashirikiana katika kuwasema watu. Na unatakiwa uwondoke katika vikao kama hivyo, kwani kukaa kwako ndio kusikiliza. Lazima watu watahadhari. Haya ni maradhi makubwa yamewapata Waislamu. Tunamuomba Allah atuondoshee maradhi haya mabaya na izipatanishe nyoyo za waja wake wema wawe wanapendana na kusikilizana katika kila jamabo lao (Amin).

 

Copyright ©2005  Uislam.net