|
KUSEMA UWONGO
Kusema
uwongo ni katika sifa mbaya itakayomfanya mwenyewe atoke katika kundi la
watu waumini. Kwani huwenda Muumini akawa na fisa nyengine kama za ubakhili
au woga. Lakini akishakuwa ni muwongo basi si Muumini tena. Imani hutoka
katika moyo wake akawa miongoni mwa kundi jengine la wasemao uwongo. Yote
haya yamebainishwa katika Quraan na Hadithi za Bwana Mtume (S.A.W). Kasema
Mwenyezi Mungu katika Suratin Nahal Aya ya (105):
(ÅöäøóãóÇ íóÝúÊóÑöí ÇáúßóÐöÈó
ÇáøóÐöíäó áóÇ íõÄúãöäõæäó ÈöÂíóÇÊö Çááøóåö æóÃõæúáóÆößó åõãú ÇáúßóÇÐöÈõæäó)
Maana yake:
“Wanaozuwa uwongo ni wale wasioziamini Aya ya Mwenyezi
Mungu, na hao ndio waongo”.
Na akasema
tena katika Sura hiyo hiyo ya Nahal Aya ya (116):
( æóáóÇ ÊóÞõæáõæÇ áöãóÇ ÊóÕöÝõ
ÃóáúÓöäóÊõßõãú ÇáúßóÐöÈó åóÐóÇ ÍóáóÇáñ æóåóÐóÇ ÍóÑóÇãñ áöÊóÝúÊóÑõæÇ Úóáóì
Çááøóåö ÇáúßóÐöÈó Åöäøó ÇáøóÐöíäó íóÝúÊóÑõæäó Úóáóì Çááøóåö ÇáúßóÐöÈó
áóÇ
íõÝúáöÍõæäó ).
Maana yake:
“Wala msiseme, kwa sababu ya uwongo usemao ndimi zenu.
(Hii ni halali na hii ni haramu), msije mkamzuliya Mwenyezi Mungu uwongo.
Hakika wale wanaomzulia Mwenyezi Mungu uwongo hawatafaulu.”
Na katika
Hadithi iliyotolewa na Imam Malik na Adarami:
( Þöíáó áöÑóÓõæáö Çááøóåö Õóáøóì
Çááøóåã Úóáóíúåö æóÓóáøóãó Ãóíóßõæäõ ÇáúãõÄúãöäõ ÌóÈóÇäðÇ ÝóÞóÇáó äóÚóãú
ÝóÞöíáó áóåõ Ãóíóßõæäõ ÇáúãõÄúãöäõ ÈóÎöíáðÇ ÝóÞóÇáó äóÚóãú ÝóÞöíáó áóåõ
Ãóíóßõæäõ ÇáúãõÄúãöäõ ßóÐøóÇÈðÇ ÝóÞóÇáó áóÇ )
Maana yake:
“Aliulizwa Mtume (S.A.W) jee eti mtu Muumini huwa moga?
Akasema ndio. Akaulizwa tena eti Muumini huwa bakhili, akasema ndio. Kisha
akaulizwa tena, mtu Muumini huwa muwongo. Akasema Laa. (Muumini hawi muwongo)”.
Kwa hivyo
akishakuwa mtu ana sifa ya kusema uwongo, basi hata ushahidi wake
haukubaliwi. Tena itabidi watu waepukane nae, kwani huyo ni mtu wa hatari.
Na Akhera ana adhabu kali kama alivyoeleza Mwenyezi Mungu katika Suratil
Baqarah Aya ya (10):
( Ýöí ÞõáõæÈöåöãú ãóÑóÖñ ÝóÒóÇÏóåõãú
Çááøóåõ ãóÑóÖðÇ æóáóåõãú ÚóÐóÇÈñ Ãóáöíãñ ÈöãóÇ ßóÇäõæÇ íóßúÐöÈõæäó)
Maana yake:
“Nyoyoni
mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi, na watakuwa na
adhabu iumizao kwa sababu ya kule kusema kwao uwongo”.
Na Mtume
kaeleza hayo hayo katika Hadithi iliyotolewa na Imam Al Bukhari na wengineo:
( Åöäøó ÇáÕøöÏúÞó íóåúÏöí Åöáóì
ÇáúÈöÑøö æóÅöäøó ÇáúÈöÑøó íóåúÏöí Åöáóì ÇáúÌóäøóÉö æóÅöäøó ÇáÑøóÌõáó
áóíóÕúÏõÞõ ÍóÊøóì íóßõæäó ÕöÏøöíÞðÇ æóÅöäøó ÇáúßóÐöÈó íóåúÏöí Åöáóì
ÇáúÝõÌõæÑö æóÅöäøó ÇáúÝõÌõæÑó íóåúÏöí Åöáóì ÇáäøóÇÑö æóÅöäøó ÇáÑøóÌõáó
áóíóßúÐöÈõ ÍóÊøóì íõßúÊóÈó ÚöäúÏó Çááøóåö ßóÐøóÇÈðÇ)
Maana yake:
“Kwa hakika ukweli unapeleka katika ucha Mungu. Na
ucha Mungu unapeleka Peponi. Na mtu husema ukweli mpaka aandikwe kuwa yeye
ni Mkweli.
Na hakika uwongo unapeleka katika
upotofu (madhambi) na madhambi hupeleka Motoni. Na mtu huzoweya kusema
uwongo mpaka aandikwe kwa Mwenyezi Mungu kuwa yeye ni Muongo.”
Tunamuomba
Mola atuepushe na sifa kama hii. Ukishaandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu ya
kuwa wewe ni msema uwongo unataka nani tena akusaidie. Hakuna ila kuwacha tu
sifa kama hiyo na kurudia upesi kwa Allah na kufanya tawba na kuomba msamaha
kwake
Na kusema
uwongo ni katika sifa kubwa za watu wanafik., ambao hawana bahati yoyote
katika Uislamu. Bali wao wanaitwa watu wenye nyuso mbili. Katika Hadithi
iliyotolewa na Imam Al Bukhari na Muslim. Kasema Mtume (S.A.W):
( ÃóÑúÈóÚñ ãóäú ßõäøó Ýöíåö ßóÇäó
ãõäóÇÝöÞðÇ ÎóÇáöÕðÇ æóãóäú ßóÇäóÊú Ýöíåö ÎóÕúáóÉñ ãöäúåõäøó ßóÇäóÊú Ýöíåö
ÎóÕúáóÉñ ãöäó ÇáäøöÝóÇÞö ÍóÊøóì íóÏóÚóåóÇ ÅöÐóÇ ÇÄúÊõãöäó ÎóÇäó æóÅöÐóÇ
ÍóÏøóËó ßóÐóÈó æóÅöÐóÇ ÚóÇåóÏó ÛóÏóÑó æóÅöÐóÇ ÎóÇÕóãó ÝóÌóÑó )
Maana yake:
“Mtu mwenye hizi sifa nne huwa ni munafiki wa kweli.
Na atakaekuwa na sifa moja tu kati ya hizi basi huwa na sifa ya unafiki
mpaka aiwache. Atakapo pewa amana hukhuni. Na atakaposema husema uwongo. Na
atakapotowa ahadi hatekelezi. Na atakapogombana huzidisha ugonvi ukawa
hawishi (wakapatana)”.
Je uko
tayari ufufuliwe na wanafiki siku ya Kiama. Kwani ukifa na sifa hizi basi
utafufuliwa na wenzako wenye sifa kama hizi za unafiki. La hutaki na
unaogopa basi jirekebishe kabla wakati haujesha.
Na Uislamu
kama ulivyokazata sifa hii mbaya, basi ukaamrisha kusema ukweli katika kila
jambo. Kwani kusema ukweli ni katika sifa kubwa za Waumini. Basi lazima kila
Muislamu aulazimishe ulimi wake katika kusema ukweli ili awe miongoni mwa
wanaosifika na sifa kama hii tukufu. Mtume (S.A.W) alikuwa akiwafundisha
wazazi kusema ukweli hata katika malezi ya watoto wao wadogo. Katika Hadithi
iliyotolewa na Imam Ahmad ya kuwa huyu bawana Abdillahi bni Amir kasema:
“Sikumoja nilipokuwa bado mdogo alinita mama yangu na Mtume (S.A.W)
alikuwepo akishuhudia. Mama yangu akaniambia njoo nikupe kitu. Mtume (S.A.W)
akamuuliza mama yangu. Ulitaka kumpa nini? Mama yangu akajibu: nilitaka
kumpa tende. Basi hapo Mtume (S.A.W) akamwambia: Ama lau kaja na hukumpa
kitu basi ungeliandikiwa kuwa umesema uwongo.”
Kwa hivyo
hata mtoto mdogo asizoweshwe hadithi za uwongo na udanganyifu. Bali
azoweshwe mambo mema na kusema ukweli.
Na uwongo
uko wa ina nyingi kila mmoja ana njia yake ya kudanganya watu. Na zote ni
haramu, haifai kusema uwongo katika hali yoyote ile. Japo kuwa ruhusa ipo
ikiwa kuwasuluhisha watu waliogombana ili mapenzi yao yarudi. Na vile vile
katika kuulinda Uislamu ikiwa kuna vita baina ya Waislamu na makafiri, basi
hujuzu uwongo kama kutumia hila mbele ya maaduwi.
Lakini
kukaa vikaoni ukawachekesha watu kwa uwongo. Hayo ni haramu. Mtume (S.A.W)
kasema katika Hadithi iliyotolewa na Imam Ahmad:
( áóÇ íõÄúãöäõ ÇáúÚóÈúÏõ ÇáúÅöíãóÇäó ßõáøóåõ ÍóÊøóì
íóÊúÑõßó ÇáúßóÐöÈó Ýöí ÇáúãõÒóÇÍö æóÇáúãöÑóÇÁó æóÅöäú ßóÇäó ÕóÇÏöÞðÇ )
Maana
yake: “Hatokuwa na Imani kamili mja mpaka awache
uwongo katika maskhara na awache kujadiliana hata katika ukweli.
Sifa hizo
mbili hazimpendezi Muislamu, anatakiwa aziwache na kujepusha nazo katika
maisha yake. Ndugu zangu Waislamu tuchukuwe mifano mizuri katika wale
waliotangulia ambao wamesifika na kila sifa njema. Mpaka wakawa wakutajwa
katika Qura’an. Huyu Sayyidna Abu bakar Radhi ya Mwenyezi Mungu zimfikie.
Akisifika na sifa ya ukweli mpaka akaitwa (Sidiyq) yaani ni Mkweli.
Mara moja
Bwana huyu na Mtume (S.A.W) walipokuwa wakikimbia kutoka Makkah na kuelekea
Madina. Wakati ambo Makafiri wa Kikureshi wanamtafuta Mtume (S.A.W) wamuuwe.
Bali walitoa ngamia mia moja atakaekuja na kichwa cha Bwana Mtume (S.A.W)
lakini Mola alimlinda. Wakati wapo njiani wanakwenda, aliwatokea mtu fulani
ambaye anamjua Abu Bakar lakini hamjui Mtume. Yule mtu akamuuliza Abu Bakar,
nani huyu unayefuatana naye? Hapa Sayidina Abu Bakar akisema kuwa huyu ni
Muhammad, huwenda yakawa matatizo. Lakini kwa hekima akasema: “Huyu ni
muongozi ananiongoza njia.” Yule bwana kafahamu kuwa ni nji ya Madina.
Lakini Abu Bakar anakusudia njia iliyonyooka ya kwenda Peponi. Nayo ndio
kazi ya Mtume (S.A.W). Hivi ndivyo Waislamu khalisi walivyokuwa wakiishi
katika maisha yao, amani na usalama ukawepo na Mwenyezi Mungu akawafungulia
milango ya kila kheri.
Ewe
Mwenyezi Mungu zitoharishe ndime zute na kusema uwongo (Amin).
|