|
Anayedaiwa
anatakiwa atokane na deni analodaiwa ili aje kwa Allah akiwa ametakasika na
kila jukumu. Likishindikana kwake hilo, asiondoke ila wakimruhusu wanaomdai,
na ausie madeni wanayomdai. Haya iwapo deni umefika wakati wake wa kulipwa.
Ama ikiwa haujafika wakati wake wa kulipwa, itamjuzia kuondoka bila ruhusa
yao kwa sharti ausie wanachomdai. Na haya kwa hali yo yote ni kwa yule aliye
nacho cha kulipa; ama asiyekuwa na cha kulipa asiondoke kwenda hija mpaka
atokane na kila deni analodaiwa, na Allah ni Aula wa kuukubali udhuru wake.
MDAIWA DENI LA RIBA
Huyu hali
yake ni ngumu mno kuliko aliyetangulia. Ni juu yake kwanza ajitakase na kila
muamala wa riba; kwani Allah Mtukufu hawapokelei ila watu wacha-Mungu; na
mwenye kuingia katika riba hayumo kabisa katika ucha-Mungu. Inatosha kuwa
yeye yumo vitani dhidi ya Allah na Mtume Wake - rehema za Allah na amani
zimshukie.
MAZINGATIO:
� Kukopa
kwa ajili ya kuhiji hakuna haja, kwasababu mwenye kuhiji hutakiwa atokane na
majukumu yote kabla hajasafiri na miongoni mwa hayo ni madeni.
� Wengi
kati ya watu huchelewesha hija mpaka wakifikia umri mkubwa huusia wafanyiwe
hija iliyowalazimu. Hili ni kinyume na amri ya Allah Mtukufu Mtakasika,
kwani wasia hauwi badala ya hija. Mwenye uwezo anawajibika kuharakiza kuhiji
mwenyewe; na kuusia ni kuchukua tahadhari tu yasije mauti yakamfika ghafla
kabla ya kuhiji.
� Kuhiji
hakuombewi msaada wa kifedha maana ni fardhi kwa mwenye uwezo wa nafsi na
mali. Akifanya hilo kisha baadae akapata uwezo
ni bora kwake na salama zaidi arudie hija yake.
� Haimlazimu
mtoto kuwahijia wazazi wake waliokufa maadamu hawakuusia. Akiwahijia itakuwa
ni wema aliowafanyia anaolipwa thawabu na ni utiifu kwa Allah; na wao
wanatarajiwa kupata thawabu wakiwa katika watu wa kheri.
� Anayesafiri
kwenda Maka au Madina au kwengineko inamwajibikia kupunguza sala za rakaa
nne ziwe rakaa mbili asiposali nyuma ya imamu mkaazi. Kuisali kila sala kwa
wakati wake ni bora, na kuchanganya sala mbili kunajuzu hususan kwa ambaye
yumo njiani katika safari.
�
Hija ni nguzo na fardhi
mojawapo ya Uislamu. Uwajibikaji wake na utekelezwaji hautegemei kuoa na
kuolewa au ukubwa wa umri, kama wanavyodhani
wengi kati ya watu. Bali kuhiji ujanani ni bora zaidi ili mtu aweze
kuitekeleza kama ipasavyo kisheria.
|