KULISHA MASKINI

 

Suala: Je kafara Mughladha ni kulisha maskini tu?
Jawabu: Kafara Mughladha inaweza ikawa ni kuachia uhuru mtumwa au kufunga miezi miwili kwa pamoja na inaweza ikawa ni kulisha maskini sitini. Na huenda ikawa kuhama baina yake (ukatoka) kwenye kuachia uhuru mtumwa, mpaka kufunga kisha kulisha maskini ni khiyari ya mtu au inaweza ikawa ni kwa mpangilio (Kuachia uhuru mtumwa ukikosa ufunge miezi miwili kwa pamoja ukishindwa ulishe maskini sitini). Na kafara Mughladha inakuwa ni kwa sababu ya ku uwa mtu kwa makosa      (si kwa kukusudia), nayo ni kuachia uhuru mtumwa, akiwa hajapata mtumwa, afunge miezi miwili kwa pamoja (mfululizo). Na pia inakuwa ni wajibu kwa alie apa juu ya mkewe kuwa ni kama mgongo wa mama yake, kabla hawajakutana kimwili(hawaja ingiliana) kwa nassi ya Qur’aan, nayo ni kuachia uhuru mtumwa, akiwa hajapata mtumwa, afunge miezi miwili kwa pamoja (mfululizo), akiwa hawezi kufunga miezi miwili kwa pamoja, basi alishe maskini sitini. Na pia inamuajibikia aliyefungua kwa makusudi (bila ya sababu) mchana wa ramadhani, nayo ni kuitekeleza kafara hiyo kwa taratibu zilizotajwa kabla katika kujibu suali hili. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Nini neno (jawabu) lenu kwa aliyezidisha kiwango cha chakula akampa kila maskini S’saa kamili (kilo mbili na arubaini gram), je kuna makosa yeyote yale kufanya hivyo?
Jawabu: Juu ya kila maskini ni nusu ya S’saa na ina kadiriwa kuwa ni kilo moja na ishirini gram, na atakae zidisha Mwenyezi Mungu ana mzidishia. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Nini neno (jawabu) lenu katika kulipa pesa badala ya kulisha maskini, hasa kwa mwenye kumiliki chakula na anahitajia pesa?
Jawabu: Asili ni kutoa chakula kwani ndilo lilo thibiti kwa sunna, na wala isiendewe kutoa pesa isipokuwa ikiwa maskini watakataa kupokea chakula. Katika hali hii itatolewa kima (kiwangocha pesa) cha chakula kinacho takikana kutolewa, wala kiwango cha pesa kisiwekwe kwa kadiri ya fedha kwa sababu chakula kina panda bei na kushuka na pia kina pia chakula kinatafautiana kwa muda wa wakati na pahala.  (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)