KULIPA SAUMU NA KULISHA MASKINI

 

Suala: Je ni sharti kufuatilizia siku katika kulipa saumu?

Jawabu: Ni wajibu kufuatilizia siku katika kulipa saumu, isipokuwa kwa dharura kama kusafiri, au maradhi au udhaifu wa hali.(Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).

 

Suala: Nini neno (jawabu) lenu juu ya yule anedaiwa kulipa ramadhani kwa ajili ya maradhi aliyo pata katika mwezi wa ramadhani. Na akataka kuzilipa siku hizo lakini hawezi kuzilipa zote kwa pamoja (kwa kufutilizia siku)?
Jawabu: Atakae kuwa ni tabu juu yake kuilipa ramadhani yote kwa pamoja (kwa kufuatilizia siku), basi hana haraj (neno) kuzilipa kwa kuka tika (yaani kulipa siku maalumu kisha unapumzika kisha unalipa siku na kuendelea).(Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).

 

Suala: Nini neno (jawabu) lenu, juu ya anaedaiwa siku mbili kwa pamoja za mwezi wa ramadhani, akazilipa kwa kutenga siku baina yake (yaani amefunga siku kisha akafungua siku ndio akamalizia siku ya mwisho)?
Jawabu: Ni lazima azilipe siku zote mbili kwa pamoja (kwa kufuatilia siku baada ya siku), isipokuwa kwa dharura anaweza akazilipa mbali mbali. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).

 

Suala: Mtu anadaiwa siku za saumu ya ramadhani, akazigawanya makundi mawili (nyakati mbili), kwa ajili ya ujahili wake juu ya sharti la kulipa siku zote kwa pamoja?

Jawabu: Kutokana kuwa yeye amelipa siku alizokuwa akidaiwa sioni kuwa arejee kuzifunga tena siku hizo, hata kama amefanya makosa ya kuto zilipa kwa ujumla hizo siku. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).
 

ATAKAE SADIFIA KUWA SAUMU YAKE NI SIKU YA EID NA ATAKAE SILIMU (ATAKAE INGIA KWENYE UISLAM) MCHANA WA RAMADHANI

Suala: Mtu anadaiwa kulipa siku za ramadhani akafunga baadhi ya hizo siku, na wakati analipa saumu zake ikaingia Eid kubwa (Eid Al-Adh’a), je aendelee kufunga hizo siku katika siku za Tashreeq (11,12,13 Dhul Hija)?

Jawabu: Atakae kuwa anadaiwa kulipa siku za ramadhani, basi ni juu yake afunge siku ambazo hazi ingiliani na siku zinazo katazwa kufunga, kwa kuwa mtu akiwa analipa saumu ni lazima (wajib) kulipa siku hizo kwa pamoja si kwa kutenganisha siku, na hili limekubaliwa na Ulamaa wengi. Allahuma isipokuwa kwa dharura kama vile maradhi au safari, na kuna baadhi ya Ulamaa wanaona kuwa safari si dharura. Ama kufunga siku za tashreeq ni makruuh kufunga na ibada inatakikana itekelezwe katika nyakati ambazo si makruuh kufanya ibada hizo. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Nini hukumu ya aliesilimu mchana wa ramadhani, je ailipe siku hiyo?
Jawabu: Atakae silimu mchana wa ramadhani, ajizuie na vyote vinavyo futarisha (funguza) siku hiyo ambayo amesilimu, kisha ailipe tena? (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Atakae silimu katikati ya mwezi wa ramadhani, je ina mlazimikia azilipe siku zilizompita za ramadhani kabla haja silimu?
Jawabu: Katika jambo hilo kuna khilafu, kutokana na khilafu juu ya ramadhani je ni faridha moja au kila siku moja ya ramadhani ni faridha ya peke yake? Juu ya khilafu ya mwanzo ina muajibikia kuzilipa siku hizo,na khilafu ya pili hai muajibikii kuzilipa siku hiyo na hili ndilo lenye nguvu (bora). (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Nini neno (jawabu) lenu, juu ya aliyefunga akasukutua mdomo wake na maji si kwa kutawadha, yakaingia (yakateleza) baadhi ya maji ndani ya koo (tumbo), bila ya kukusudia, je ni juu yake ailipe siku hiyo au asiilipe?
Jawabu: Wame khitalifiana Ulamaa katika kuingia maji ya kusukutua ndani ya mwili (kuteleza) ikiwa kwa uchache au kwa wingi bila ya kukusudia wakati mtu amefunga, je inamuajibikia kulipa au kutolipa siku hiyo? Lilo kuwa bora ni kulipa hiyo siku ikiwa umemeza hayo maji nnje ya udhu (yaani, ikiwa si wakati unatawadha udhu wa sala) (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)