|
Shukurani ni zake Mola Muumba,
Mfalme anayesifika kwa kila sifa za ukamilifu, aliyetakasika na kila sifa za
upungufu, Mmiliki na mwenye uwezo wa kila kitu, na ambaye akikiambia kitu
kuwa kinakuwa. Kisha rehma na amani zimshukie Mbashiri Muonyaji, Mhitimishi
wa Manabii na Mitume, pamoja aali zake, na sahaba zake, na waliowafuatia kwa
wema hadi Siku ya Malipo.
Mwenyezi Mungu (SWT)
anatwambia katika suratul-Baqarah aya ya pili :
(Ðóáößó ÇáúßöÊóÇÈõ áÇó ÑóíúÈó Ýöíåö åõÏðì áøöáúãõÊøóÞöíäó)
“Hiki ni Kitabu
kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wamchao Mwenyezi Mungu”
(Albaqara,
aya-2)
Ndani
ya Qur’an upo uwongofu ulio kamilika kwa walioamini, wakawa tayari kuitafuta
kweli, na wakajikinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu Duniani na Akhera.
Ndugu
muislamu:
Ukitaka kujua kama wewe kweli unakiamini
Kitabu cha Mwenyezi Mungu, basi naomba ujiulize
nafsi yako: Qur’ani imetuamrisha tufanye kadha na kadha na imetukataza
kufanya kadha na kadha. Je mimi nayafuata hayo kwa ukamilifu? au nafuata
baadhi yake na mengine nayadharau au najiletea hoja mbali mbali?
AFA
LA RIBA
Miongoni
mwa maafa makubwa ambayo yamewafika wengi katika waisilamu mpaka wamekuwa
hawana raha katika maisha yao ni kosa la
Riba¹
- deni
(lililo-laaniwa), nalo ni katika
Madhambi Makubwa (Kabair).
►NINI
MADHAMBI MAKUBWA (KABAIR)?
Dhambi kubwa
ni kosa lolote ambalo kama mwenye kulifanya hakuliacha na kutubia hutosha
kuwa sababu ya yeye kunyimwa neema ya kuingia Peponi na badala yake
kuadhibiwa Motoni.
Mwenyezi
Mungu ametupa dhamana katika kitabu chake kitakatifu kuwa mtu atakae
jiepusha na madhambi makubwa basi atamfutia madhambi madogo (Saghair) na
atamuingiza Peponi. Dalili ya hilo ni kauli yake Subhaanahu:
(Åöä ÊóÌúÊóäöÈõæÇú ßóÈóÂÆöÑó ãóÇ Êõäúåóæúäó Úóäúåõ äõßóÝøöÑú
Úóäßõãú ÓóíøöÆóÇÊößõãú æóäõÏúÎöáúßõã ãøõÏúÎóáÇð ßóÑöíãÇð)
“Mkiyaepuka
makubwa mnayo katazwa, tutakufutieni makosa yenu madogo, na tutakuingizeni
mahali patukufu”
(An-nisaa, aya - 31)
Aya imetuwekea sharti moja kwa mambo mawili: (1) kufutiwa
makosa madogo na (2) kuingizwa mahali patukufu. Sharti moja lenyewe ni
kuepuka makubwa tunayokatazwa. Na mahali patukufu si
pengine ila ni Peponi.
RIBA NI DHAMBI KUBWA; YAINGIZA MOTONI
Katika
Qur’ani Mola amesema :
( ÇáøóÐöíäó íóÃúßõáõæäó
ÇáÑøöÈóÇ
áÇó íóÞõæãõæäó ÅöáÇøó ßóãóÇ íóÞõæãõ ÇáøóÐöí
íóÊóÎóÈøóØõåõ ÇáÔøóíúØóÇäõ ãöäó ÇáúãóÓøö
Ðóáößó ÈöÃóäøóåõãú ÞóÇáõæÇú ÅöäøóãóÇ ÇáúÈóíúÚõ ãöËúáõ
ÇáÑøöÈóÇ æóÃóÍóáøó Çááøåõ ÇáúÈóíúÚó
æóÍóÑøóãó ÇáÑøöÈóÇ
Ýóãóä ÌóÇÁåõ ãóæúÚöÙóÉñ ãøöä ÑøóÈøöåö ÝóÇäÊóåóìó Ýóáóåõ ãóÇ ÓóáóÝó
æóÃóãúÑõåõ Åöáóì Çááøåö æóãóäú ÚóÇÏó
ÝóÃõæúáóÜÆößó ÃóÕúÍóÇÈõ ÇáäøóÇÑö åõãú ÝöíåóÇ ÎóÇáöÏõæäó)
“Wale
wanaokula riba hawasimami ila kama anavyosimama aliye pandwa na Shet'ani kwa
wazimu. Hayo ni kwa kuwa wamesema: ‘Biashara ni kama riba tu’, wakati
Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na kaiharamisha riba. Hivyo
aliyefikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake akaacha [kula riba], basi ni
chake kilichotangulia, na hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Ama wenye
kurudia basi hao ndio watu wa Motoni, humo
watadumu”
(Albaqara, aya-275)
Wenye ilmu wanasema aya inatupa taswira ya wanaokula riba
watapokuwa wanatoka makaburini mwao siku ya kiyama ya kwamba watakuwa
wakitapatapa, wanasimama wakianguka kama mtu aliyeingiwa na shetani.
MLA RIBA HAWI MUUMINI
:
Mwenyezi
Mungu amebainisha kuwa kula riba na imani
hayakubaliani:
(íóÇ ÃóíøõåóÇ ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇú ÇÊøóÞõæÇú Çááøåó æóÐóÑõæÇú
ãóÇ ÈóÞöíó ãöäó ÇáÑøöÈóÇ Åöä ßõäÊõã ãøõÄúãöäöíäó)
”Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi
Mungu, na acheni kilichobaki katika riba, ikiwa nyinyi ni Waumini”
(Albaqara,
aya-278)
Kwa hivyo
ikiwa sisi ni waumini kweli basi
tumche¹
Mwenyezi Mungu na tuache riba.
SIYEACHA RIBA KATANGAZIWA VITA NA
MWENYEZI MUNGU :
Mwenyezi
Mungu amesema baada ya aya iliyotangulia:
.(
ÝóÅöä áøóãú ÊóÝúÚóáõæÇú
ÝóÃúÐóäõæÇú ÈöÍóÑúÈò ãøöäó Çááøåö æóÑóÓõæáöåö
æóÅöä ÊõÈúÊõãú Ýóáóßõãú ÑõÄõæÓõ ÃóãúæóÇáößõãú áÇó ÊóÙúáöãõæäó æóáÇó
ÊõÙúáóãõæäó)
“Na kama hamtafanya [hivyo],
basi jueni kwamba mtakuwa na vita na Mwenyezi Mungu
na Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilmali zenu.
Msidhulumu wala msidhulumiwe”
(Albaqara, aya-279)
Vita
vya Mwenyezi Mungu si vya risasi au mabomu, lakini vita vya Mwenyezi Mungu
hapana mtu ambaye anaweza kuvikimbia. Miongoni mwa vita vya Mwenyezi Mungu
ni kupatwa na maafa mengi kama vile dhiki au mtu kutokuwa na raha katika
maisha yake hata akiwa na mali nyingi. Kwani Mwenyezi Mungu huondoa baraka
katika mali ya riba::
(íóãúÍóÞõ
Çááøåõ ÇáúÑøöÈóÇ æóíõÑúÈöí ÇáÕøóÏóÞóÇÊö æóÇááøåõ áÇó íõÍöÈøõ ßõáøó ßóÝøóÇÑò
ÃóËöíãò)...
“Mwenyezi
Mungu huifutia
baraka [mali ya] riba, na huzibariki [mali zinazotolewa] sadaka. Na Mwenyezi
Mungu hampendi kila mwenye kukana [amri Zake], mtenda dhambi”
(Albaqara, aya-276)
Huwenda
ukamuona mtu masikini lakini akawa yumo katika furaha kuliko huyo anayekula
riba. Sababu ya huyu kuwemo katika furaha ni ahadi ya Mwenyezi Mungu
aliyoahidi ya kuwa Mu’umini yeyote atakaetenda mema (mke au mume) basi
atamhuisha maisha mazuri na atamlipa malipo mazuri akhera:
(ãóäú Úóãöáó ÕóÇáöÍÇð ãøöä ÐóßóÑò Ãóæú ÃõäËóì æóåõæó ãõÄúãöäñ
ÝóáóäõÍúíöíóäøóåõ ÍóíóÇÉð ØóíøöÈóÉð æóáóäóÌúÒöíóäøóåõãú ÃóÌúÑóåõã ÈöÃóÍúÓóäö
ãóÇ ßóÇäõæÇú íóÚúãóáõæäó)
“Mwenye kutenda
mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, tutamhuisha maisha mema;
na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda”
(An Nah’l, aya-97)
Lakini atakae pinga amri za Mwenyezi
Mungu basi atakuwa na dhiki hapa duniani na siku ya kiyama atafufuliwa
kipofu:
(æóãóäú
ÃóÚúÑóÖó Úóä ÐößúÑöí
ÝóÅöäøó áóåõ ãóÚöíÔóÉð ÖóäßÇð
æóäóÍúÔõÑõå
íóæúãó ÇáúÞöíóÇãóÉöÃóÚúãóì)
“Na
atakayeacha kufuata mawaidha yangu, basi kwa yakini atakuwa na maisha ya
dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu”
(Ta’ha, aya-124).
Bila ya shaka hapana mtu aliye tayari kufufuliwa
kipofu,
kisha aingizwe motoni. Kwa hivyo hapana budi ila tuyapokee mawaidha ya Mola
wetu.
►Na katika hadithi za mtume
Muhammad (SAW):
(áóÚóäó
Çááøóåõ
Âßöáó ÇáÑøöÈóÇ þ þæóãõæßöáóåõ æóÔóÇåöÏóíúåö æóßóÇÊöÈóåõ ÞóÇáó
æóÞóÇáó ãóÇ ÙóåóÑó Ýöí Þóæúãò ÇáÑøöÈóÇ æóÇáÒøöäóÇ ÅöáøóÇ ÃóÍóáøõæÇ
ÈöÃóäúÝõÓöåöãú ÚöÞóÇÈó Çááøóåö ÚóÒøó æóÌóáø)ó
“Mwenyezi Mungu
amemlani mwenye kula riba (mwenye
kuchukua ziada juu ya deni), na mwenye kuitoa iliwe (k.v. anayekopa
akalipishwa zaidi ya alichokopa), na mashahidi wake wawili na mwenye
kuiandika (mkataba wake), na akasema (SAW) haitaenea riba na zina kwa watu
isipokuwa watajisababishia kushukiwa na adhabu ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka”.
Na kutoka kwa Jabir bin Abdullahi (Radhi
za Mola zimfikie) amesema:-
(áóÚóäó
ÑÓæá
Çááøóå
(Õáì
Çááå Úáíå æÓáã)
Âßöáó ÇáÑøöÈóÇ þþæóãõæßöáóåõ æóÔóÇåöÏóíúåö æóßóÇÊöÈóåõ,
óÞóÇáó"åã
ÓæÇÁ").
“Mtume
wa Mwenyezi Mungu (SAW)
amemlani¹ mwenye kula
riba, na mwenye kuitoa iliwe, na mashahidi wake wawili na mwenye
kuiandika (mkataba wake), na akasema: “hao wote ni sawa” yaani katika dhambi.
Na Abu Bakar (Radhi za Mola
zimfikie) amesema:
(ÇáÒÇÆÏ
æÇáãÓÊÒíÏ
Ýí ÇáäÇÑ
)
“Muengezaji na mwenye kuengezewa wote motoni.” Makusudio
yake kuwa mwenye kukopesha (kwa faida) na mwenye kukopeshwa (akalipa kwa
faida) basi wote ni sawasawa na malipo yao ni
kuingizwa motoni”
Kuna watu
wanasema hii ni sharia ya nchi, sisi hatuna budi kuifuata; wenye kuchukua
jukumu hilo ni wakubwa wa nchi (serikali) walioweka sharia hii. Na wengine
husema huwezi kuishi bila ya mkopo wa Benki n.k. Ewe ndugu yangu hebu
turudiye katika Qur’an ili tuone onyo la Mwenyezi Mungu:
(íóæúãó ÊõÞóáøóÈõ æõÌõæåõåõãú
Ýöí ÇáäøóÇÑö
íóÞõæáõæäó íóÇ áóíúÊóäóÇ ÃóØóÚúäóÇ Çááøóåó æóÃóØóÚúäóÇ
ÇáÑøóÓõæáÇ)
“Siku
ambayo nyuso zao zitapinduliwa pinduliwa katika
Moto. Watasema: Laiti tungali mt'ii Mwenyezi Mungu, na tungali
mt'ii Mtume!”(Al-Ahzaab,
aya-66).
(æóÞóÇáõæÇ ÑóÈøóäóÇ ÅöäøóÇ ÃóØóÚúäóÇ ÓóÇÏóÊóäóÇ æóßõÈóÑóÇÁäóÇ
ÝóÃóÖóáøõæäóÇ ÇáÓøóÈöíáÇ)
“Na
watasema: Mola wetu! Hakika sisi tuliwat'ii bwana zetu na wakubwa wetu; nao
ndio walio tupoteza njia”
(Al-Ahzaab,
aya-67).
(ÑóÈøóäóÇ ÂÊöåöãú ÖöÚúÝóíúäö ãöäó ÇáúÚóÐóÇÈö æóÇáúÚóäúåõãú
áóÚúäÇð ßóÈöíÑÇð).
“Mola
wetu! Wape wao adhabu mara mbili, na uwalaani laana kubwa”
(Al-ahzaab, aya-68).
Siku hiyo udhuru huo na dua hizo
hazitatusaidia kitu, na Mwenyezi Mungu atatwambia:
(Èóáóì ÞóÏú ÌóÇÁÊúßó ÂíóÇÊöí ÝóßóÐøóÈúÊó ÈöåóÇ
æóÇÓúÊóßúÈóÑúÊó æóßõäÊó ãöäó ÇáúßóÇÝöÑöíäó).
"Bali
ndio! Bila ya shaka zilikujia aya zangu, nawe ukazikadhibisha, na ukajivuna,
na ukawa miongoni mwa makafiri!”
(Azzumar, aya-59)....
►Nasiha:
Ndugu yangu Muislamu kama umejizamisha
katika riba basi rudi kwa mola wako na tubia haraka kabla wakati haujapita,
kwani Mwenyezi Mungu anasema:
(æóÇáøóÐöíäó ÅöÐóÇ ÝóÚóáõæÇú ÝóÇÍöÔóÉð Ãóæú ÙóáóãõæÇú ÃóäúÝõÓóåõãú ÐóßóÑõæÇú
Çááøåó ÝóÇÓúÊóÛúÝóÑõæÇú áöÐõäõæÈöåöãú æóãóä íóÛúÝöÑõ ÇáÐøõäõæÈó ÅöáÇøó
Çááøåõ æóáóãú íõÕöÑøõæÇú Úóáóì ãóÇ ÝóÚóáõæÇú æóåõãú íóÚúáóãõæä)
“Na ambao pindi wafanyapo uchafu
[kwa kutenda dhambi kubwa] au wakajidhulumu nafsi zao [kwa dhambi ndogo]
humkumbuka Mwenyezi Mungu na wakamwomba msamaha kwa dhambi zao - na nani
anaye futa dhambi isipokuwa Mwenyezi Mungu? - na wala hawaendelei na waliyo
yafanya na hali wanajua”
(Al-Imran, aya-135).
(ÃõæúáóÜÆößó ÌóÒóÂÄõåõã ãøóÛúÝöÑóÉñ ãøöä ÑøóÈøöåöãú
æóÌóäøóÇÊñ ÊóÌúÑöí ãöä ÊóÍúÊöåóÇ ÇáÃóäúåóÇÑõ ÎóÇáöÏöíäó ÝöíåóÇ æóäöÚúãó
ÃóÌúÑõ ÇáúÚóÇãöáöíäó)
“Hao
malipo yao ni msamaha kwa Mola wao, na Bustani zipitazo mito kati yake,
wadumu humo, na ni mwema ulioje ujira wa watendao [mema]”
(Al-Imran, aya-136).
►UTANABAHISHO MUHIMU: Elewa
ndugu muislamu kuwa faida itolewayo na benki ya riba kwa rasilimali ya mteja
ni riba. Hii ni kwasababu rasilimali za wateja huingia katika mikopo ya riba
itolewayo na benki hio na riba ya mikopo hio hugawiwa kwa wateja.
►UKUMBUSHO:
Kumbuka kuwa
kitu chochote cha halali kina tabu kukipata na kinataka subira na jitihada,
lakini jambo la haramu ni wepesi na rahisi sana kulipata. Hii yote ni
mitihani ya Mwenyezi Mungu kwetu sisi waja wake ili wapate kujulikana nani
ni wacha Mungu (wenye kumuamini, kumtii na kumuogopa). Mwenyezi Mungu
amewaahidi wale wamchao kuwa atawafungulia njia na atawaletea riziki kwa
namna ambayo hawakuitarajia:
(æóãóä
íóÊøóÞö Çááøóåó
íóÌúÚóá áøóåõ ãóÎúÑóÌÇð. æóíóÑúÒõÞúåõ ãöäú ÍóíúËõ áÇ íóÍúÊóÓöÈõ æóãóä
íóÊóæóßøóáú Úóáóì Çááøóåö Ýóåõæó ÍóÓúÈõå)
.
....................................
“Na mwenye
kumcha Mwenyezi Mungu [akashika amri
zake na akaepuka makatazo yake] atamjaalia njia ya kutokana na kila dhiki.
Na atamtengezea sababu za kupata riziki kwa pande ambazo hata hazimpitikii
katika fikra zake. Na mwenye kumwachia mambo yake yote Mwenyezi Mungu basi
Yeye ni Mwenye kumtosha, [hana haja ya mwengine]”
(Al-talaaq, aya-2&3).
Pia kasema:(
æóãóä
íóÊøóÞö Çááøóåó
íóÌúÚóá áøóåõ ãöäú ÃóãúÑöåö íõÓúÑÇð)
“Na mwenye
kumcha Mwenyezi Mungu, [akatimiza
hukumu zake] Mwenyezi Mungu atayawepesisha mambo yake”
(Al-talaaq, aya-4).
Na amewaahidi wacha Mungu kuwafutia madhambi yao na
kuwalipa ujira mkubwa akhera:
(æóãóä
íóÊøóÞö Çááøóåó
íõßóÝøöÑú Úóäúåõ ÓóíøöÆóÇÊöåö æóíõÚúÙöãú áóåõ ÃóÌúÑÇð)
“Na mwenye
kumcha Mwenyezi Mungu [akahifadhi
hukumu zake] humfutia makosa yake, na
atampa ujira mkubwa”
(Al-talaaq, aya-5).
Suala:-
Nifanyeje ili na mimi nimiliki halali?
Jawabu:-
Dunduliza (changa) pesa zako au shirikiana na ndugu
zako wa Kiisilamu mufanye upatu ili lengo lenu liwe la kusaidiana, na
Mwenyezi Mungu atakuwafikisheni kwa fadhila zake, kwa sababu mutakuwa
miongoni mwa wale walio mcha Inshaallah.
Mwisho, namalizia kwa shairi la (Imam Shaafi):
Ewe binaadamu Ulizaliwa na mama yako na huku unalia na
watu wamekuzungukia wamefurahi wanacheka.
Basi ifanyie nafsi yako ili wakikulilia Siku ya mauti yako unacheka
na umefurahi.
Çááåã
ÃÍííäÇ Úáì ÇáÅÓáÇã æÃãÊäÇ Úáíå ¡ Çááåã æÇÑÒÞäÇ ÚãáÇð ÕÇáÍÇð ãÊÞÈáÇð ¡
æÇáÊæÈÉ ÞÈá ÇáãæÊ ¡ æÇáÔåÇÏÉ ÚäÏ ÇáãæÊ ¡æÇáÚÝæÉ
æÇáÊíÓíÑÚäÏ ÇáÍÓÇÈ ¡ æãÑÇÝÞÉ ÇáÃäÈíÇÁ æÇáÕÇáÍíä Ýí ÇáÌäÇä íÇ ÃÑÍã ÇáÑÇÍãíä
¡æÕáì Çááå æÓáã Úáì äÈíäÇ ãÍãÏ æÚáì Âáå æÕÍÈå ÃÌãÚíä
Ndugu yenu: Masoud Al Gheithy.
|