|
Hapa katika
Tanzania hawezi mtu kumaliza (au kufanya) jambo la rasmi na lisilokuwa rasmi
ila mpaka atoe baadhi ya mali (Rushwa) kwa wenye kuhusika, na (pia hata)
wafanya kazi wadogo (wa ngazi ya chini) nao pia wanasema: Tupeni na sisi
walaukuwa kitu kidogo nasi tule!!!!…….Jee! nini hukumu ya kitendo hiki?
JAWABU:
Kitendo hiki asili yake haijuzu ila katika
jambo la dharura, maana hii ni rushwa iliyoharamishwa ambayo imetaja hadithi
kwamba wamelaaniwa wenye kufanya hivyo katika kauli ya Mtume (S.A.W) kasema:
“Mwenyezi Mungu amewalani mtoaji rushwa na mpokeaji rushwa” na kwa hakika
katika hali ya dharura (iliyokuwa haina budi) mtoaji (Rushwa) anakuwa hana
dhambi isipokuwa mpokeaji ndiye mwenye dhambi, (mtoaji anafanya hivyo kutoa
rushwa) kalazimika bila ya kupenda nafsi yake kwa ajili ya kuzuia madhara ya
jambo lake au kurudisha haki yake isipotee, au ili kufanya maslaha
yaliyokuwa hana budi nayo, katika sababu zote hizo (mwenye shida kama hizo
za lazima) inawezekana (kutoa mali kwa ajili ya kutengenekewa mambo yake)
kwa sharti asiruke mipaka ya haki yake tu anayostahiki, kwa sababu jambo
lake limo mikononi mwa watu wabaya ambao hawamwogopi Mwenyezi Mungu Mtukufu
wala khofu yoyote, inakuwa jambo litapotea au halipati mpaka atoe kitu.
Basi hapana dhambi kuwapa chochote ili kadiri ya kuepukana na madhara na
kupata mahitaji yako yenye maslaha… Na katika hadithi imejuzu haya kwa njia
ya Imam Abi Sha’atha’a radhi za Allah ziwe juu yake Jabir bin Zeid, kwamba
Mtume (S.A.W) alipotaka kupatana na washirikina kwa ajili ya kuutetea mji wa
madina katika kisa cha Ahzab ila kwa kutoa thuluthi ya matunda kuwapa,
ingalikuwa si kufanya hivyo ndio ikawa kupata nguvu Waislamu ikawa ushindi
na nusura ya Allah kwa Waislamu, Na Allah ndiye ajuaye.
|