KUIPOKEA RAMADHAN

Hakika hamna kosa katika anuani hii,kwani watu wanagawanyika katika makundi mengi katika kuuaga mwezi mtukufu wa ramadhani kwa walivyo chukulia umuhimu wa mwezi wa ramadhani juu yao:

1) Kundi la mwanzo wana uaga mwezi huu mtukufu kwa moyo ulio na huzuni na nafsi yenye kuogopa. Watu hawa wana mategemeo kuwa huenda ALLAH atawakubalia amali zao zote  nzuri walizo zifanya katika mwezi huu.

2) Kundi la pili wanamajuto kwa muda walio upoteza katika mwezi huu bila ya kuutumia katika kufanya ibada na kufanya kheri kama vile wao walivyokuwa wakitegemea.

3) Kundi la tatu ni kundi la watu waliofurahi kwa kumalizika mwezi wa ramadhani, ili warudi katika matamanio ya nafsi zao na maasi waliokuwa wamezuilika kuyafanya katika mwezi wa ramadhani.

4) Kundi la nne ni kundi ambalo kuingia kwa ramadhani au kwisha kwake ni kama mchezo kwao hawajali na wala hawalindi mipaka ya ALLAH katika mwezi huo hawafuati walioamrishwa wala hawa achi waliokatazwa.

JE WEWE UKO KATIKA KUNDI GANI UKIJIPIMA NA RAMADHANI YA MIAKA ILIYOPITA? NA JE UNACHAGUA UWE KATIKA KUNDI GANI KATIKA RAMADHANI INAYOKUJA?

Ndugu waislamu, suala la kujiuliza ni:

JE,  SISI TUNAUJUA KWA UHAKIKA HUU MWEZI WA RAMADHANI NI NINI  NA KWA NINI TUNA UFUNGA?

Watu wengi hawajafahamu makusudio ya mwezi huu wa ramadhani ni nini. Watu wengi wame ubebesha mwezi huu mambo ambayo umeshindwa kuyabeba. Waka upa uhai usiku wake kwa mambo ambayo hayamridhishi Mola na wakaupa uhai mchana wake kwa mambo ambayo hayatakikani kuyafanya, na huku ALLAH anasema katika kitabu chake kitukufu Qur'aan katika Surat Al-Baqara (aya#183 mpaka 185):

* قال الله تعالى:  يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ* أَيَّامً مَّعْدُودَاتٍ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ فَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ وَأَن تَصُومُواْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ  * شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِيَ أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ يُرِيدُ اللّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلاَ يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُواْ الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُواْ اللّهَ عَلَى مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ .

Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu (183). Mfunge siku maalumu za kuhisabika. Na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hisabu katika siku nyengine. Na wale wasio weza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. Na atakaye fanya wema kwa kujitolea, basi ni bora kwake. Na mkifunga ni bora kwenu, kama mnajua (184). Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi.

Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru (185).

Ndugu zangu waislamu: Mwezi wa ramadhani ni nguzo ya nne katika nguzo za uislam, na ni jambo la kumuabudu Mola. Mwenyezi Mungu akatufanyia mwezi huu kuwa ni faridha juu yetu, anasema Mtume (SAW):

 {بني الإسلام على خمس: وصوم رمضان}

Saumu inatufundisha kumuogopa Mola na kuwa na ikhlas katika kufanya amali (ibada) kwa ajili saumu ni siri baina ya mja na Mola wake:

{الصيام لي و أنا أجزي به – حديث قدسي شريف}

 Saumu ni kinga inayotukinga tusifanye maasi na inatengeneza tabia zetu na inalinda nafsi zetu na matamanio:

{الصيام جُنة فإذا كان يوم صيام أحدكم فلا يفسق و لا يرفث، و إن سابّه أحد أو شاتمه فليقل إني امرؤ صائم – حديث شريف}

 Saumu ni afya ya mwili na pia inaipa mwili nguvu:

{صوموا تصحوا – حديث شريف}

Saumu ni mapumziko ya mwaka mzima ya tumbo, kwani tumbo ni mfanyakazi anaeipenda kazi yake katika mwaka mzima. Basi ni haki ya huyu mfanyakazi maskini apate mapumziko angalau mchana wa mwezi mmoja katika mwaka. Basi ni juu yetu tupunguze kula  ili tulipumzishe hili tumbo na machofu ya kazi nzito ya mwaka mzima.

{ما ملأ ابن آدم وعاء شرّ من بطنه – حديث شريف}

Saumu ni chakula bora cha roho: Kupunguza  kwetu kula, kunakupa nafasi roho (moyo) kupata nguvu na kulainika baada ya kupata chakula cha roho amabcho ni kufanya ibada tofauti kama vile sala,kufunga,kusali usiku,kusoma Qur'aan na kutembelea wazazi na arhaam. n.k

Saumu ni rehama na kuoneana huruma na kukamatana na kuzidisha udugu kwa kuhisi vipi watu wanaohitajia au waliofukuzwa makwao au wanaokosa chakula mwaka mzima. Vipi wanaweza kuishi ikiwa sisi tunaokosa chakula mchana wa ramadhani tu tuna kuwa kama hivi.

 Saumu ni ushindi na kuwa izza ya nafsi na karama ya mtu, kwani katika mwezi huu waislamu walishinda vita vingi na uislamu ukapata jina katika mwezi huu.

 Saumu inayo faida nyingi nyingine, kutoka kwenye faida ya kimwili na         ki imani (roho) mpaka kufikia faida ya kiafya na kimali na economic.

FAIDA GANI ZINAPATIKANA KATIKA MWEZI HUU WA RAMADHANI AMBAZO SI RAHISI KUPATIKANA KATIKA MIEZI MINGINE YA KAWAIDA:

Thawabu za amali njema katika mwezi huu zinakuwa mara dufu:

{الصيام لي و أنا أجزي به } {من صلى فيه نافلة كان كمن صلى فريضة و من صلى فريضة كان كمن صلى 70 فريضة )

Kutaarishwa roho kiibada na kumtii Mola na kuiweka nafsi tayari kuongeza juhudi na kufanya ibada kwa wingi.

Usiku wa LAILAT AL-KADR: usiku ambao ni bora kushinda miezi elfu. Na ujira wa kusali na kuamka usiku na kusoma Qur'aan na dua katika usiku huo unakuwa ni sawa na ujira wa zaidi ya miaka 83:

 {ليلة القدر خير من ألف شهر}

 Umra katika mwezi huu ni sawa na Hajj

{العمرة في رمضان تعدل حجة معي – حديث شريف}

Kufunguliwa milango ya pepo na kufungwa milango ya moto na kufungwa kwa mashetani:

{إذا جاء رمضان فتحت أبواب الجنان و أغلقت أبواب النيران و صفدت الشياطين – حديث شريف}

Kurahisishwa njia ya toba na kuacha maasi, kama vile kuvuta sigara,kulewa ulevi na kutumia madawa ya sumu, kupoteza sala, kutizama mambo ambayo hayafai, kusikiliza nyimbo na michezo ambayo haina maana(karata) n.k

Urahisi wa kuacha baadhi ya tabia mbaya kama vile kulala sana, kula sana,kutokuwa na bashasha kuchelewa kusali na kupoteza nyakati zake, kudhereu kazi n.k

kukamatana jamaa na majirani na kuwa kitu kimoja na kukamatana kwa taqwa na amali njema na wakawa ni wenye kutiana nguvu katika kutekeleza ibada za mchana na za usiku.

VIPI TUJITAARISHE KUOPOKEA MWEZI WA RAMADHANI UNAOKUJA NA NINI TUNAWEZA TUKAFANYA KATIKA MWEZI HUO:

Hakika mtu yeyote akitaka kupasi mtihani ni lazima ajitaarishe kwa makini juu ya mtihani huo kwa kusoma usiku na mchana. Kwani wanafunzi wengi wanajitaarisha na mitihani hiyo kwa kusoma na kuhifadhi masomo yao nyakati za usiku ili wapate kujitaarisha vyema na mtihani huo ndio maana wanapasi vizuri mwisho wa mwaka. Na tukitaka kuchambua zaidi jambo hili hembu tutizame timu za mipira vipi zina jitaarisha na mechi zao mpaka inafika kusafiri nchi mbali mbali ili wajitaarishe vizuri kimwili na kifikra na mechi hizo na wapate kushinda na kupewa vikombe na kama hawatafanya hivyo basi watashindwa na kikombe kuchukuliwa na timu nyingine. Ikiwa haya ndiyo masharti muhimu kwa  mwanafunzi au timu ya mpira wayatekeleze ndio watafuzu kwenye mitihani ya masomo au mechi zao za mipira hapa duniani. Vipi pepo ya ALLAH je haitaki mataarisho na kukesha usiku na mchana ili tufaulu na tuingie peponi ambayo upana wake ni baina ya mbingu na ardhi iliyotaarishwa kwa wenye kumuogopa ALLAH. Basi ni mashindano gani yanayostahiki kujitaarisha nayo, mashindano ya kidunia au ya kiakhera. Basi ni bora tuamue lipi ni la mwanzo kulitenda na nini tufanye ili tupasi katika mwezi huu mtukufu wa ramadhani unaokuja.

Imethibiti kuwa Mtume (SAW) alikuwa akizidisha kufunga katika mwezi wa SHAABAN na ikafika hadi masahaba wakawa hawajui lini Mtume(SAW) ameamka amefunga na lini ameamka hajafunga kwa kuthirisha kwake kufunga katika mwezi huu wa Shaaban. Na Mtume (SAW) alikuwa akizidisha kutembelea arhaam zake na kutoa sadaka na kufanya kila aina ya mambo mema. Alikuwa akifanya yote haya kwa kujitaarisha na mwezi mtukufu wa ramadhani, ili iwe ni rahisi kwake kufanya haya mambo unapoingia mwezi mtukufu wa ramadhani.

{ولكم في رسول الله أسوة حسنة – القرآن الكريم}

Ndugu zangu waislamu: Hizi ni baadhi ya fikra kwa uwezo wa ALLAH zitatuwezesha kuufunga mwezi wa ramadhani unaokuja kwa ukamilifu. Anza kujizowesha kufanya mambo haya na itaarishe nafsi yako kuyafanya kuanzia mwezi huu wa Shaaban:

* Weka azima kuwa mwezi wa ramadhani unaokuja uwe ndio mwezi bora utakaofunga kushinda miezi yote ya ramadhani iliyopita maishani mwako.

* Weka plan yenye uhakika itakayo kufanyisha uweze kufaulu katika mwezi huu. Mfano, andika baadhi ya vitu vya kheri ambavyo utaweza kuvifanya katika mwezi huu. Ujuwe ikiwa huweki plan ya kufaulu basi unaweka plan ya kutofaulu.

* Jizoweshe kufunga nafila anza kujizowesha kufunga baadhi ya siku katika mwezi huu wa Shaaban kama vile nafila ili uizoweshe nafsi yako.

* Jikaribishe zaidi na Qur'aan: Anza kujizowesha kusoma Qur'aan katika mwezi wa shaaban na uweke wakati maalumu wa kuhifadhi na kutekeleza amri zake.

* Jizoweshe kusali sala za usiku katika mwezi huu kwa kusali sala fupi kabla huja lala au kabla sala ya al-fajiri au ukiweza nusu ya usiku.

* Ongeza nyakati na rakaa za sala za usiku na usijilazimishe kuamka muda mrefu usiku ili usichoke na kumbuka kuwa wewe unapata ujira kwa haya unayoyafanya.

* Tembelea wazee wako na arhaam zako katika mwezi huu wa shaaban.

* Jizoweshe kutoa ulichokuwa nacho na kutoa sadaka. Na weka baadhi ya mali ili utoe sadaka katika mwezi wa ramadhani na kumbuka jamaa zako wa karibu ndio bora kuwafanyia umaarufu (wema)

{و ما تنفقوا من خير فلأنفسكم، و ما تنفقون إلا ابتغاء وجه الله، و ما تنفقوا من خير يوف إليكم و أنتم لا تظلمون - البقرة} {ما نقص مال من صدقة – حديث شريف}.

* Futarisha watu waliofunga: Jitahidi ualike mtu aliyefunga nyumbani kwako.

{من فطّر مسلما كان له أجر صيامه من غير أن ينقص من أجره شيئا}

- Chagua nani utamualika na weka siku ya kumualika.

- Unaweza kualika watu wako wa karibu au jirani zako au waislamu wenzako au wanafunzi wageni wanaoishi mtaani kwako.

- Unaweza kualika ndugu zako waislamu wageni katika nchi yako ili uwapunguzie unyonge wa kuwa mbali na familia zao na wapate kujuwa umoja wa waislamu na udugu wao.

- Pia unaweza kuwaalika wasiokuwa waislamu ili wajuwe vipi waislamu wanafunga na kwa nini waislamu wanafunga huwenda wakapata imani na wakaingia ndani ya dini kwa walio yaona, ukawa wewe ni sababu ya wao kuingia katika uislamu:

{لأن يهدي الله بك رجلا خير لك من الدنيا و ما فيها}.

*Linda wakati wako: Jaribu kulinda wakati wako katika mwezi wa ramadhani usipoteze hata sekunde katika mwezi huu isipokuwa kwa kufanya ibada na kumtaja Mola (Tasbih au tahlil)

* Mwezi wa Qur'aan: kwa ajili mwezi wa ramadhani ni mwezi ulioshushwa ndani yake Qur'aan basi ni juu yako kila wakati ujitahidi kusoma Qur'aan:

- Weka wakati maalumu wa kuhifadhi Qur'aan.

- Weka wakati wa kufahamu maana ya aya za Qur'aan na kutekeleza maamrisho yake na kuwacha makatazo yake.

- Weka wakati wa kujifundisha kusoma Qur'aan kwa Tajwid na kuisoma sawa bila ya makosa.

- Weka wakati uwasomeshe wasiojuwa kusoma Qur'aan.

- Nunuwa Tafsiri ya Qur'aan kwa lugha yeyote ile na mpe muislamu asiyefahamu kiarabu

{بلغوا عني و لو آية – حديث شريف}

- Jiunge katika vikundi vya watu wanaosoma Qur'aan kila siku au wiki mara moja

* Toba weka nia ya kutubu kwa ALLAH kwa kujitahidi kuwacha madhambi uliyokuwa ukiyafanya kabla kwa kujishughulisha na kufanya mema na kuusemesha moyo wako.

* Tafuta rafiki mwema ili akupeleke katika mema na epukana na rafiki wabaya.

* Jaribu kuzishinda tabia zako mbaya kwa kuzikusanya tabia hizo na kuzitafutia dawa na kuzibadilisha na tabia nyingine njema. Mfano:

- Kula kwingi kwa israf na kununua vivazi ambavyo si muhimuàß kula kiasi na kutofanya israf katika kula na kivazi.

- Kujizowesha kuishi bila ya kunywa kahawa na vinginevyo ambavyo ni halaliàß kutosheka na kidogo hata kama ni halali.

- Kuvuta sigara na maasi mengineàßKutubu juu ya ALLAH kwa kutorejea kuvuta sigara na kufanya tena hayo maasi.

- Kulala sana na uvivuàß Lala mapema ili uamke mapema na kuwa na hima katika maisha yako.

- Kukesha usiku na kutizama TVàß Lala mapema na amka usiku ili usali sala za usiku na usome Qur'aan.

- Kupuuza sala na kukithirisha kuunga salaàß Jitahidi kusali sala katika nyakati zake na kungojea sala baada ya sala.

- Kusengenya na kusema uongo na kusema hovyoàß Kumuogopa ALLAH na kukithirisha kumtaja ALLAH na kutosheka kusema yanayofaa kusema.

*Kuomba msaada na kujikinga kwa ALLAH na kutawakul juu yake

والــســلام عـلـيـكـم ورحـمـة اللّه وبـركــاتــ