KUCHELEWESHA KULIPA SAUMU

 
Suala: Imeniwajibikia juu yangu kulipa siku arubaini ya ramadhani mbali mbali (nyingi) kisha nikazilipa, na sijalipa kafara, je inaniwajibikia kafara kwa ajili ya kuchelewesha kulipa hizo siku?
Jawabu: Kulipa saumu ni wajibu, na juu ya kafara kuna khilafu, ikiwa ata chelewesha aliyefungua kulipa saumu mpaka ikaingia ramadhani nyingine. Lenye nguvu ni wajibu wa kulipa kafara, nako ni kulisha maskini mmoja kwa kila siku aliyofungua, na inajuzia kutoa nusu ya S’saa (kilo moja na ishirini gram) kwa kila maskini mmoja. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Mtu amesafiri katika ramadhani akafungua siku tano, akarejea kutoka safarini, ukaisha mwezi wa ramadhani, na hajalipa siku hizo mpaka ikaingia ramadhani nyingine, nini juu yake?
Jawabu: Atakae fungua katika safari au kwa maradhi kisha akarejea kwake au akapona maradhi yake na hajalipa siku anazodaiwa mpaka ikaingia ramadhani nyingine. Inamuajibikia juu ya kulipa siku hizo alishe maskini mmoja kwa kila siku aliyofuturu kwa kuchelewesha kwake kulipa hizo siku. Na haya ni kwa dalili ya hadithi alioitoa Al-Daarqatni kwa njia ya Abi Huraira (RA), na riwaya ikatolewa na Al-Bukhari. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala: Inaruhusiwa kuchelewesha kulipa siku unazodaiwa za ramadhani? Na je inajuzu kuzi gawanya siku za kulipa kafara (kuto zilipa zote kwa pamoja)?
Jawabu: Ikiwa atalazimika kechelewesha kulipa ramadhani basi hamna kitu juu yake, lakini ana amrishwa kulisha maskini mmoja kwa kila siku aliyochelewesha kuilipa, kuwa ni ihtiyaatt (akiba) ikiwa imeingia ramadhani nyingine. Ama saumu ya kafara ni lazima kuzilipa zote kwa pamoja, isipokuwa kwa dharura kama maradhi au hedhi au nifas, na pia safari. Baada ya kuondoka hayo (maradhi au hedhi au nifas, au safari) inamua jibikia aendeleze kulipa bila ya kusita. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)

 

Suala:  Nini neno (jawabu) lenu kukusanyisha pamoja siku za kulipa za ramadhani na siku sita za Shawaal kwa nia moja?
Jawabu: Hamna budi kutenganisha baina ya saumu ya kulipa ramadhani na saumu ya nafila (siku sita za Shawaal).  (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)