Chochote katika wema unachokifanya kwa ajili ya nafsi yako, basi ujira (thawabu) wake mkubwa na zaidi utaukuta mbele ya Mwenyezi Mungu

KUWATEMBLEA WAISLAMU

Kwa uwezo wake Allahu Subhana Wataala, Jumuiya ya Istiqama imeweza kuwafikiwa Waislamu katika sehemu mbali mbali ili kutaka kujua hali zao na kuwafikishia ujumbe wa Daawa katika njia ya Allah kwa kuwapelekea Walimu na Mashekhe, moja katika safari hizo ni hii mnayoiona katika picha hii. Kuwatembelea kabila moja la Kimasai liloingia katika uislamu.

Jumuiya ya Istiqama huchukuwa juhudi hizi kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa Allah katika kuitangaza Dini yake. Na alhamdulilah faida zinazopatika zinaonekana na kila mtu, Na kama mnavyojua juhudi hizi husimamishwa na misaada ya Waislamu.

Kwa hivyo musiwache kujitolea katika njia za kheri kama hizi, Jiunge na Waislamu wenzako na Isaidie Jumuiya ya Istiqama katika kutangaza Dini ya Allah na kuwasaidia Waislamu.

 

KUCHIMBA VISIMA VYA WAQFU

Vile vile moja katika juhudi za Jumuiya ya Istiqama ni kuwachimbia Waislamu visima katika sehemu zinazokuwa na shida ya kupata maji ya kunywa na kutumia.

Alhamdulilah jumuiya imeweza kuchimba zaidi ya visima 50 vya maji katika sehemu mbali mbali kama Unguja, Pemba, Bara, Uganda Mali na  Ghana.

Ndugu Muislamu unaweza kusaidia au kutowa mchango wako katika juhudi hii ya kuchimba visima vya maji. Na taklifa yake si ghali kuanzia Dola 300 - hadi 2000 hutegemea na sehemu ilivyo. Mara nyengine huwa ni vigumu kuyafikia maji, lakini alhamdulilah kwa uwezo wake Allah hupatikana.

 

 

MADRASA ZA QURAAN

Kuwasomesha watoto kitabu cha Mwenyezi Mungu Qura'an ni katika jambo la kwanza liloanzwa na Jumuiya ya Istiqama. Madrasa hizi idadi yake inazidi 150 katika sehemu mbali mbali za unguja zanzibar na kisiwani Pemba na Bara katika wiliya zake nyingi na Uganda na Mali na Ghana na Ruwanda na Burundi. Vile vile Isiqama husaidia kupeleka walimu katika sehemu za mbali ili kupeleka mbele masomo ya Dini, watoto husomeshwa Quraan na Hadithi na Fiqhi pamoja na Lugha ya Kiarabu.

 

Mashekhe na Walimu kutoka Omani hutembele vyuo vya Istiqama na kufuatilia taasisi na misingi ya kusomesha watoto.

Ndugu Muislamu: Yote haya yanahitajia misaada yenu katika ujenzi wa vyuo hivyo na matayarisho yake.

        

 

KUJENGA MISIKITI

Kujenga Misikiti ni moja katika jambo la muhimu nilalotangulizwa na Jumuiya ya Istiqama. Zaidi ya Misikiti 50 imejengwa na Jumuiya au husaidiwa kifedha katika kusimamisha msingi wa mwazo, kuanzia unguja zanzibar kisiwani Pemba na sehemu nyengine tulizozitaja hapo nyuma.

Ndugu Muislamu: Wallahi ungelikuwa unajua furaha ya Waislamu wenzako pale wanapoona Msikiti unajengwa katika kijiji chao basi ungelitamani na wewe mali yako imeunga mkono pamoja na mali za Waislamu wanaojitolea katika kazi hii ya kuimarisha Nyumba za Mungu.

 

 

 ANUANI ZA JUMUIYA YA ISTIQAMA

Copyright ©2004  Uislam.net