زيارة سماحة الشيخ أحمد بن حمد الخليلي إلى جمهورية بروندي  من تاريخ (14- فبراير إلى 18- فبراير 2007)م

Msafara wa Samahat Sheikh Ahmed Al-Khalili (Mufti Mkuu wa Oman) katika nchi ya Burundi tarehe 14/2/2007

Baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumtakia rehma Bwana Mtume S.A.W hii ni takriri kamili ya msafa wa Mufti Mkuu wa Oman Sheikh Ahmed bin Hamed Al-Khalili katika nchi ya (BURUNDI)

Katika tarehe 14 Februari 2007 Alifika Samahat Sheikh Al-Khalili uwanja wa ndege Mjini Bujumbura mji mkuu wa Burundi, baada ya kupata mualiko kutoka kwa waomani wanaoishi huko. Alhamdulilah mapokezi yalikuwa mazuri na katika mapokeleo ya hali ya juu kwa kuwafikiana na uheshimiwa wa Mufti na wale waliofuatana nae.

 

 

President wa SENATE wa Burundi ndie aliempokea Samahat Sheikh uwanja wa ndege mjini Bujumbura.

 

رئيس مجلس الشيوخ البروندي في مقدمة مستقبلين سماحة الشيخ في مطار العاصمة  -  بوحومبورا

 

UFUGUZI WA MASJID ISTIQAMA (Bujumbura)

Masjid Al-Istiqama ni msikiti ambao uliojegwa katika Mwaka wa 1942 na Waomani waliokuwa wakiishi katika mji huo wa (Bujumbura) na ulikuwa ni msikiti mdogo hauna haduma za kisasa. Alhamdulilah baada ya juhudi za watu wa hapo wakaujenga upya msikiti huu, pamoja na kuukuzisha ukaweza kusali zaidi ya watu mia tatu (300) ndaini yake. Na Samahat Sheikh akapata Mualiko wa kwenda kuufungua msikiti huu kirasmi katika terehe 16/2/2007. Pamoja na Msikiti huu kuna Maktaba vikiwemo vitabu mbali mbali ndani yake, maktaba ina nafasi ya kutosha kwa wale wanaotaka utafiti wa elimu.

 

 

Samahat Sheikh Akitembelea  Maktaba ya Msikiti wa Bujumbura

سماحة الشيخ   يتجول في مكتبة مسجد الاستقامة - بوجومبورا

إفتتاح مسجد  المرحوم ( محمد بن حمدان الشرجي ) رمونجي

UFUNGUZI WA MSIKITI WA   MAREHEMU MOHAMMED BIN HAMDAN AL-SHARJI  (ROMONGE)

Msikiti huu umejengwa mwaka 1971 na mwenyewe Marehemu kwa idhini ya Allah Mohammed bin Hamdan Al-Sharji. Kisha ukajengwa upya na watoto wake katika mwaka 2006 na kufunguliwa Rasmi na Samahat Sheikh Ahmed bin Hamed Al-Khalili Mufti Mkuu wa Oman.

 

Sheikh akizungumza na Waislamu katika msikiti wa Romonge

Sheikh akitembelea Maktaba ya Msikiti bado imo katika matayarisho

Matembezi ya Sheikh katika Chuo cha Mayatima (Bujumbura)

   

 

 ANUANI ZA JUMUIYA YA ISTIQAMA

Copyright © 2007 www.uislamu.net