|
|
Jumuiya ya Istiqaama ya Kiislam ya Kimataifa |
Ni Jumuiya
isiokuwa ya kiserikali wala ya kibashara ambayo malengo yake ni kuendeleza
utamaduni, uchumi, elimu na afya kwa jamii chini ya maadili ya Kiislam.
Nchi mbali
mbali imeona iko haja kuwepo taasisi na Jumuiya binafsi ambazo malengo yake
kutoa huduma bora kwa jamii.
Hivyo
serikali za nchi hizo zinatathmini sana pamoja na kuzitambua huduma
zitolewazo na Jumuiya za kibinafsi zenye malengo ya kuinua hali ya jamii na
kujenga Taifa kwa jumla.
Chochote katika wema unachokifanya kwa ajili
ya nafsi yako, basi ujira (thawabu) wake mkubwa na zaidi utaukuta mbele ya
Mwenyezi Mungu.
Udugu wa kweli sio ududgu wa damu, bali ni
udugu wa kiislam, udugu wa dini. Mtume wa Mwenyezi Mungu (S A W) alisema:
"Muislamu katika mapenzi yao na kuhurumiana ni kama mwili, sehemu yoyote au
kiungo chochote kikiumwa, mwili mzima unapata maumivu"
Mtume (S A W) amepigania Uislamu kwa hali na
mali. Masahaba wake pia wamefuata nyayo zake wametupa vyote vilivyomo katika
milki yao (mali) ili kuuhami uislamu kwa kuwa utufikie sisi tukiwa katika
hali ya kutochafuliwa (safi na nadhifu ).
Baadaye wakaja wafuasi (Taabiy) na
wapiganaji wa kiislamu (Mujahidiin) ambao walitumia mali na kutoa muhanga
maisha yao kwa ajili ya kuutangaza na kulingania Uislamu na neno
(KALIMAH)(kushuhudia kuwa hapana mola anayestahiki kuabudiwa isipokuwa
Mwenyezi Mungu) la Mwenyezi Mungu (ALLAH) walipata heshima na ushindi katika
dunia na malipo yao akhera ni pepo.
Enyi ndugu wa kiislamu (wake kwa waume)
tumewaita ili muwe pamoja na watu hao wema.
"… pamoja hao Mwenyezi Mungu amewaweka
miongoni mwa Mitume
,wachaMungu , mashahidi, waaminifu na hao
ndio marafiki wema".
Ikiwa kweli unataka kuwa miongoni mwao na
kutafuta njia itakayokuongoza kufikia huko, basi sisi Jumuiya ya Kiislamu ya
Istiqaama ya kimataifa tunakualika ujiunge nasi kwa kusaidia chochote
ambacho Mwenyezi Mungu (S W T) amekukirimu (amekupa) na uchangie katika
miradi ifuatayo:- Kama kutoa elimu, kuhifadhi Qur - an tukufu, malezi ya
watoto kulingana na tabia, maadili , misingi na silka za kiislamu.
Mtume (S A W) alisema:
" Yule anayetumia katika njia ya kiislamu
analipwa mara mia saba:
"Utajiri haupungui kwa sababu ya kutumia
katika njia ya sadaka.
|