|
|
HUKUMU ZA
USIKU WA KUAMKIA TAREHE 10 DHUL-HIJA |
Kulala
Muzdalafa baada kuondoka Arafaat.
Katika
sunna ni kuchanganya sala mbili: ya magharibi na isha huko Muzdalafa
kutokana na hadithi ya Mtume - rehema za Allah na amani zimshukie:
“Kuwa yeye - rehema za Allah
na amani zimshukie - alifika Muzdalafa akachanganya magharibi na isha kwa
adhana moja na iqama mbili na hakusali cho chote baina yao.”Ameipokea Nasaaiy, Abu Daud, Ibnu Maajah na Ibnu Abi
Shaiba.
Muzdalafa
yote ni pa kusimama isipokuwa ‘Waadi Muhas-sir’, kutokana na kauli yake -
rehema za Allah na amani zimshukie:
“Muzdalafa yote ni pa kusimama na msikae
kwenye Muhas-sir.” Imepokewa na Ahmed. Muhas-sir
ni njia ya maji bina ya Muzdalafa na Mina na ni karibu zaidi na Muzdalafa (ni
eneo alipofikwa na adhabu Abraha).
Imeruhusiwa
kwa wanawake, watoto na wachungaji kuondoka Muzdalafa usiku baada ya kutua
kwa mwezi.
Ni lazima kulivuka bonde
la Muhas-sir kabla kuchomoza kwa jua ila kwa dharura.
Kuomba
dua kwenye ‘Al-mash-ar Al-haram’ (Muzdalafa) ni wajibu, na inatosheleza dua
yo yote au kutamka ‘Laa ilaha illa LLah’ au kuhimidi au kutamka talbia.
Akifanya lo lote kati ya hayo wajibu umeshamuondokea, na asipofanya lo lote
kabisa itamuwajibikia kuchinja.
|