|
|
HUKUMU ZA
SIKU YA 8 DHUL-HIJA (MINA) |
Mfanya
hija ya qiraanu au ifraadu ataelekea Mina na ihramu yake, na
mfanya tamattuu atahirimia hija pahala alipofikia au po pote katika
eneo la Haram.
Kukithirisha talbia na
dua wakati wa kuelekea na anapokuwapo huko Mina .
Mwenye kuhiji atasali
Mina sala zote tano yaani adhuhuri, alasiri, magharibi, isha na alfajiri ya
siku ya tarehe 9 kwa kupunguza rakaa za sala ya rakaa nne, kutokana na
hadithi iliyothibiti kutoka kwa Mtume - rehema za Allah na amani zimshukie:
“kwamba alitoka
kwenda Mina siku ya Tarwiya (8 Dhul-hija) akasali huko sala tano.”
Imepokewa kwa maafikiano. Bora kusali kila sala kwa wakati wake.
Kuwapo Mina usiku wa kuamkia tarehe 9 Dhul-hija ni sunna
iliyowajibika; atakaelala kwengineko itamlazimu kuchinja, ila akiwa katika
wenye udhuru hatawajibikiwa na kitu, lakini amekosa ujira mkubwa. Dalili ya
hili ni hadithi ya Urwa bin Mudharris amesema:
“Nimekuja kwa Mtume - rehema za Allah na amani
zimshukie - nikamwambia nimekujia kutoka Milima miwili ya Tay-i,
nimekichokesha kipando changu na kuitaabisha nafsi yangu; hakuna mlima wo
wote ila nimesimama juu yake, je basi, nitakuwa nina hija? Akasema: Mwenye
kusali nasi sala ya alfajiri hapa na hali alifika Arafa kabla ya hapo
atakuwa amesharuhusiwa kujisafisha na hija yake imetimia.”
Imepokewa na Ahmed na Wenye sunan na akaisahihisha Tirmidhiy.
MAZINGATIO:
Inasihi kwa aliyehirimia
hija kwenda Mina siku ya Tarwiya (8 Dhul-hija) asubuhi au baada ya jua
kupindukia (adhuhuri); kinachosuniwa kwake ni kusali sala tano zote huko
Mina.
Hakuzuiwi kutangulia
kuhirimia hija kabla siku ya Tarwiya (8 Dhul-hija), vilevile hakuzuiwi
kulala Mina usiku wa kuamkia siku ya Tarwiya, lakini sunna ni vile
ilivyotangulia kutajwa.
|