|
Ndugu zangu watukufu, kwanza kabla hatujaingia ndani ya mikondo ya
maelezo na mafahamisho kuhusu umuhimu wa Hijaab kwa mwanamke wa Kiislamu,
nitapendelea kukuulizeni suali moja. Iwapo utaona chakula kimewekwa juu ya
meza ambayo juu yake kuna sahani mbili, na zote sahani hizo mbili chakula
ni kile kile isipokuwa sahani moja imefunikwa, na sahani ya pili iko wazi
ambayo chakula hicho haikufunikwa toka kilipopakuliwa.
Njaa imekushika na mwenyeji kishasema muanze kula. Na una hiyari ya kukaa
upande wowote kati ya zile sahani mbili. Jee! utachagua sahani gani
upunguze chakula… sahani iliokuwa imefunikwa au iliokuwa wazi?
Nafikiri sote tutachaguwa chakula kilichofunikwa ambacho kimestirika na
kuhifadhika kwa kufunikwa, kwani sahani iliyo wazi haitaacha kukaribisha
nzi, mende, vijidudu katika hewa, wadokozi na waonjaji waliokuwa
hawakukosha mikono yao. Kwa hivyo tunakubaliana kuwa chakula
kilichositirika ndicho chakula cha kuridhisha moyo na kisichokuwa na
ulakin ndani yake.
Chanzo cha maelezo haya ni kuhusu stara na hifadhi, ikiwa stara
hiyo ni ya chakula, ya mavazi au mwili, stara ya malazi, stara ya makazi,
stara ya kuwa mke wa watu au mume wa watu na mengineyo. Natumai kuwa sote
tunaamini na kukubali kuwa stara na hifadhi katika maisha ya Muislamu
akiwa mwanamume au mwanamke ni jambo la lazima na muhimu sana katika
mazingara ya maisha ya Kiislamu.
Uchi wa mwanamke ni mwili mzima, isipokuwa viganja vyake na uso wake ndio
si uchi kwake, yaani kwa shida anaweza kuonekana hizo sehemu tulizozitaja
kwa watu waliokuwa si mahram wake. Kwa umuhimu huu wa hishma na hifadhi na
matukuzo aliyopewa mwanamke itabidi maelezo yanayofuatia yawe kuhusu
hifadhi na utunzo wa mwanamke katika kivazi.
Kwa nini Mwanamke wa Kiislamu anavaa mavazi ya stara?
Mwamke wa Kiislamu anavaa kivazi chema na kujisitiri kwa sababu zafuatazo:
1-Kutii amri na maamrisho ya Dini yake tukufu.
2-Kuhifadhi nafsi yake na kutunza hadhi yake.
3-Kujitukuza nafsi yake na hishma yake.
4-Kujiepusha na shari za wadokozi.
5-Kujiepusha na macho maovu.
6-Kujiepusha na kuvunjiwa hishma.
7-kujistiri kwa kuvaa kivazi chema
Aya inayofuatia Mwenyeezi Mungu anamuamrisha Mjumbe wake Mtume Muhammad
(SAW) awapelekee ujumbe waja wake wafuate tabia njema, na kivazi cha
hishma na kujilinda na kujihifadhi na wasioneshe mapambo yao ambayo
yanaweza kuleta fitna na matamanio maovu.
æóÞõá áøöáúãõÄúãöäóÇÊö íóÛúÖõÖúäó ãöäú ÃóÈúÕóÇÑöåöäøó æóíóÍúÝóÙúäó
ÝõÑõæÌóåõäøó æóáóÇ íõÈúÏöíäó ÒöíäóÊóåõäøó ÅöáøóÇ ãóÇ ÙóåóÑó ãöäúåóÇ
æóáúíóÖúÑöÈúäó ÈöÎõãõÑöåöäøó Úóáóì ÌõíõæÈöåöäøó æóáóÇ íõÈúÏöíäó
ÒöíäóÊóåõäøó ÅöáøóÇ áöÈõÚõæáóÊöåöäøó Ãóæú ÂÈóÇÆöåöäøó Ãóæú ÂÈóÇÁ
ÈõÚõæáóÊöåöäøó Ãóæú ÃóÈúäóÇÆöåöäøó Ãóæú ÃóÈúäóÇÁ ÈõÚõæáóÊöåöäøó Ãóæú
ÅöÎúæóÇäöåöäøó Ãóæú Èóäöí ÅöÎúæóÇäöåöäøó Ãóæú Èóäöí ÃóÎóæóÇÊöåöäøó Ãóæú
äöÓóÇÆöåöäøó Ãóæú ãóÇ ãóáóßóÊú ÃóíúãóÇäõåõäøó Ãóæö ÇáÊøóÇÈöÚöíäó ÛóíúÑö
Ãõæúáöí ÇáúÅöÑúÈóÉö ãöäó ÇáÑøöÌóÇáö Ãóæö ÇáØøöÝúáö ÇáøóÐöíäó áóãú
íóÙúåóÑõæÇ Úóáóì ÚóæúÑóÇÊö ÇáäøöÓóÇÁ æóáóÇ íóÖúÑöÈúäó ÈöÃóÑúÌõáöåöäøó
áöíõÚúáóãó ãóÇ íõÎúÝöíäó ãöä ÒöíäóÊöåöäøó æóÊõæÈõæÇ Åöáóì Çááøóåö ÌóãöíÚðÇ
ÃóíøõåóÇ ÇáúãõÄúãöäõæäó áóÚóáøóßõãú ÊõÝúáöÍõæäó
Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho
yao, na
wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika.
Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila
kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto
wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au
wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafwasi wanaume
wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala
wasipige chini miguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni
nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa.
An Nur-31
Yaani tunafunzwa tabia njema na Mola wetu, tunaongozwa katika kheri na
tunaepushwa na shari, kwa hivyo ikiwa hatufuati basi inakuwa tunampinga
Mola wetu, Mtume wetu na wazee wetu. Sasa huo Uislamu wetu utakuwa na
msimamo gani?
Mwanamke wa Kiislamu aliyejitunza na kujitukuza nafsi yake kwa kuvaa
kivazi cha stara huwa amepata malezi mazuri ya Kiislamu, na anaongozwa na
imani yake. Muislamu huyo havai nguo za stara kwa sababu ni kivazi cha
mila na utamaduni alichokirithi kutoka kwa wazee wake, bali anatii amri ya
Mola wake na kutimiza wajibu wake.
Na hii hijaab ilivyokuwa ni amri ya Mwenyeezi Mungu, basi
hapana shaka Watume waliopita waliamrishwa vile vile kuwa wanawake
wajistiri na kujihifadhi kwa kivazi cha stara ambacho kitawatunzia hishma
yao na
kuwaepusha na kuudhiwa majiani.
Tukichukuwa mfano wa wanawake wanaotumika Makanisani (Christian Nuns)
utawakuta vivazi vyao vinakaribiana na vivazi vya wanawake wa Kiislamu,
kwa sababu hiyo ni amri kutoka kwa Mola wao, ambayo imepotea kote na
kubakia Kanisani tu.
Kulikuwa na mwanafunzi mmoja wa kike ambaye alipelekwa kusoma katika
Yunivasiti huko Syria. Tabia ya mwanafunzi huyu na kivazi chake kilikuwa
kikipendwa na wengi. Alikuwa akivaa nguo za stara kila siku na alikuwa
akipewa hishma na wanafunzi wenzake na walimu wake.
Siku moja alikuja muandishi wa magazeti katika hiyo Yunivasiti, macho yake
yakavutiwa na kupendekezewa na kivazi kizuri cha stara cha huyu mtoto wa
kike. Akamuuliza “mbona wewe peke yako katika hii klasi unavaa nguo za
aina ya peke yako” akaendelea kumuuliza “hizi nguo hazikufanyii joto
katika joto kali hili la kiangazi”
Yule mtoto wa kike akamjibu kwa Aya ya Qur’ani:
äóÇÑõ
Ìóåóäøóãó ÃóÔóÏøõ ÍóÑøðÇ áøóæú ßóÇäõæÇ íóÝúÞóåõæäó
“Moto wa Jahannam una joto zaidi laiti
(watu) wangelifahamu!”
At Tawba-81
‘Wa naam’Aina hii ya chipukizi za wanawake ndio watakaojenga
msimamo madhubuti wa nyumba zao na jamii zao, aina hii ya wanawake ndio
watakaokuwa katika msitari wa mbele wa kuunyanyua Uislamu kwa kuonesha
mfano mzuri na kuwapa malezi mema watoto wao na kusimama imara katika
jihadi ya kujilinda na kila sababu itakayompelekea kuteleza na kumuasi
Mola wake.
|