SAUMU  ZA NAFILA

 

KUFUNGA YA MWEZI WA RAJAB:

Suala: Nini hukumu ya kufunga mwezi wa Rajab, na nini hukumu ya aliyetia nia kufunga Rajab kisha hakufunga?

Jawabu: Rajab ni kama miezi mingine ya mwaka, na aliye tia nia kufunga na haja funga basi haina neno isipokuwa ile siku aliye amka amefunga ana takikana akamilishe saumu au ailipe akifutari (akifungua). (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).

 

KUFUNGA MWEZI WA SHAABAN:

Suala: Zipi ni siku bora za kufunga katika mwezi wa Shaaban?
Jawabu: Hamna katika sunna siku maalumu inapendezewa kufunga katika mwezi wa Shaaban, na yaliyotajwa kuhusu kufunga siku ya kumi na tano katika mwezi wa Shaaban si kweli. Lakini lilo kubaliwa na la kweli ni kuwa Bibi Aisha amesema: kuwa Mtume (SAW) alikuwa akifunga sana (akikithirisha kufunga) Shaaban kupita miezi yote mingine baada ya mwezi wa ramadhani. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).

 

Suala: Je inajuzu kufunga miezi miwili kwa pamoja (mfululizo), kwa nia ya kujikaribisha na Mwenyezi Mungu?
Jawabu: Haikatazwi kujikaribisha na Mwenyezi Mungu kwa kufunga siku sitini (miezi miwili) kwa pamoja, kwani kufunga huku si kama kufunga mwaka mzima, kwani inakatazwa kufunga mwaka mzima. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).

 

KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAAL:

Suala: Nini neno (jawabu) lenu kuhusu kufunga siku sita za Shawaal, je ni lazima kuzifunga mara ikimalizika Eidd ya Al-fitri, au haina neno kuchelewesha mfano: kuanza kufunga katika siku kumi za mwanzo au kabla yake au baada yake? Je ni lazima kuzifunga kwa pamoja (mfululizo) au kufunga siku kisha ukala siku (kutenganisha siku) Na ikiwa mtasema ni lazima kufunga siku sita za Shawaal baada ya eid tu, nini maana al-atf (Bithuma)-KISHA katika hadithi( Atakae funga ramadhani kisha akafatilizia siku sita za Shawaal ni kama aliyefunga mwaka mzima) Na msingi ni kuwa Atf inakuwa kwa Altarakhi( pole pole)?

Jawabu: Hadithi hii ni Mutlaq (Imewachwa wazi) haijawekwa kwa haraka wala kufuatilizia (kufunga kwa pamoja. Kwa hiyo sioni haraj (kosa) kuchelewesha kuzifunga hizo siku sita au kuzitenganisha, na si juu ya ya neno (thuma)-KISHA, dalili ya kuchukua nafasi

 

Suala: Nini neno (jawabu) lenu kwa aliyefunga nafila ya siku sita za Shawaal, katika siku ya sita akasafiri na muda wa kuwa safarini ukawa ni mwezi. Nini juu yake?
Jawabu:Ikiwa alisha anza kuifunga hiyo siku ya sita na akafungua basi ailipe. Na ikiwa kinyume na hivyo basi hana kitu. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).

 

Suala: Mtu hajakamilisha kufunga siku sita za Shawaal kwa ajili ya safari aliyosafiri. Nini juu yake?

Jawabu: Funga za nafila mtu anakuwa ni amiri wa nafsi yake, akitaka ataendelea kufunga na akitaka atafungua. Na inajuzu kufunga siku sita za Shawaal bila ya kufuatilizia (yaani unaweza kufunga siku na ukafutari (ukafungua) siku mpaka ukamilishe siku sita)  (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).

 

Suala: Akitaka mtu kufunga siku sita za Shawaal, je afunge mwanzoni wa mwezi au katikati au mwishoni. Na azifunge hizo siku sita mfululizo(pamoja) au azitenganishe?

Jawabu: Inajuzu kufunga siku hizo mwanzo wa mwezi na katikati ya mwezi na mwishoni. Na inajuzu kuzifunga zote kwa pamoja au kuzifunga kwa kuzitenganisha (yaani unaweza kufunga siku na ukafutari (ukafungua) siku mpaka ukamilishe siku sita). (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).

 

Suala: Nini neno (jawabu) lenu, juu ya kufunga siku za tashreeq kwa aliyekuwa hayuko katika Hajj?
Jawabu: Siku za Tashreeq ni tarehe Kumi na moja, kumi na mbili na kumi na tatu za mwezi wa Dhul Hijja, na ni makruh (inachukiza) kufunga mtu akiwa katika Hajj na yeyote mwingine. (aliyekuwa hayuko katika Hajj). (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).

 

Suala: Nini hukumu ya kufunga saumu ya Tattawu (nafila) na huku unadaiwa saumu ya ramadhani?

Jawabu: Wanavyuoni wamekhitalifiana kuhusu jambo hili, na kuna waliosema: (asifunge mtu saumu ya tattawu (nafila) ikiwa anadaiwa saumu, kwa ajili kulipa saumu ni lazima), na kuna walio sema: (hai katazwi kufunga tattawu(nafila) kwa mwenye kudaiwa saumu ya ramadahni) na hili ndio lenye nguvu na inajulisha hilo kuwa Bibi Aisha Mke wa Mtume (SAW) alikuwa akichelewesha kulipa ramadhani mpaka ufike mwezi wa Shaaban, kuchukulia kuwa Mtume(SAW) alikuwa akipenda kufunga katika mwezi wa Shawaal, kwa hiyo alikuwa akipenda wafunge pamoja na Mtume (SAW). Na wala haingii akilini kuwa abakie Bibi Aisha (RA) muda wote wa mwaka hafungi tattawu(nafila) na kulinda kwake kufanya mema na kuwa yeye yuko ndani ya nyumba ya mtume (SAW) ambae alikuwa akifunga kupita kiasi. Juu ya hili inajulisha kuwa inajuzu kufunga tattawu (nafila) ikiwa mtu anadaiwa ramadhani. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).

 

KUFUNGA SIKU YA ARAFA:

Suala: Nini mnasema kuhusu kufunga arafa kwa aliyekuwa yukoHajj na asiyekuwa Hajj? Na nini dalili?

Jawabu: Inapendezewa kufunga siku ya arafa kwa ajili ya fadhila zake. Na imeonyesha Sunna na imehimiza (imependezea) watu wafunge siku hii isipokuwa yule aliye simama arafa, kwani aliye simama arafa bora kwake kutofunga siku hii, kwa ajili apate nguvu ya kusimama, na dalili ni kuwa Mtume(SAW): hajafunga siku ya arafa wakati wa Hajji pamoja na kuwa mtume alikuwa akipenda kufanya mambo mema.(Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).

 

Suala: Nini ina muajibikia aliyefungua katika kufunga saumu ya nafila bila ya sababu?
Jawabu: Wamesema Ulamaa ni juu yake ailipe siku hiyo, na haya ni maneno ya Ulamaa wa kiibadhi wa Maghrib, kuchukulia maneno ya Mwenyezi Mungu:(Wala msiharibu amali zenu), na wengine wakasema hai lipi siku hiyo kwa dalili ya hadithi:(Mwenye kufunga nafila ni amiri wa nafsi yake).(Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).

 

Suala: Mtu hajakamilisha kufunga siku sita za Shawaal kwa sababu ya safari. Nini juu yake?

Jawabu: Mwenye kufunga nafila anakuwa ni amiri wa nafsi yake, akitaka ata endelea kufunga na akitaka atafungua. Na inajuzu kufunga siku sita za Shawaal bila ya kufuatilizia (yaani unaweza kufunga siku na ukafutari(ukafungua) siku mpaka ukamilishe siku. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).