|
|
BIBI YUKABID
MAMA YAKE NABII MUUSAAA
(A.S) |
æóÞóÇáóÊú ÇãúÑóÃóÉõ ÝöÑúÚóæúäó ÞõÑøóÉõ Úóíúäò áöí æóáóßó áóÇ ÊóÞúÊõáõæåõ
ÚóÓóì Ãóäú íóäÝóÚóäóÇ Ãóæú äóÊøóÎöÐóåõ æóáóÏðÇ æóåõãú áóÇ íóÔúÚõÑõæäó(9) (
ÇáÞÕÕ : 9)
Qurratu `Ainin lii Wa Laka, Laa Taqtuluunhu
`Asaa an yanfa`anaa aw Nattakhidhahu waladan. (Surat L- Qasas : 9 ).
Firauni * alizindukana kimkumkum na
usingizi ukamruka akaa macho hadi mchana kweupe kuzim hakuna nyota. Hapo
asubuhi akapiga mbiyo ya mgambo, kwa Firauni kuna mambo, watakiwa makohani
wa majini na ng`ambo, wote wafike hapo wakasikiye mambo.
Kukakutanika makohani pamoja na wachawi na
waganga wakubwa wote kwa Firauni. Aliwayeleza kuwa yeye kawota ndoto mbaya
bila ya kiyasi hata hakupata usingizi tena, ukamruka wala asijuwe
ulipokwenda. Sasa kawayita hapa ili wamfasiriye maana ya ndoto yake hiyo.
Baada ya kuchemsha mbongo walimuweleza kuwa atazaliwa mwana wa kiyume katika
Bani Israaiil (Yahudi), ambaye ndiye atakayekuwa sababu ya mauti yake
Firauni. Mtoto huyo atamnyang`anya Firauni ufalme wake na nguvu zake zote
asaliye hohe hahe, hana mbele hana nyuma. Si hayo tu bali piya atamtowa
katika ardhi hii yeye pamoja na watu wake. Na hata dini hatayiyachiliya ila
atayibadilisha na ataleta dini nyengine. Alipouliza zama aw wakati wa
kuzaliwa mtoto huyo, alijibiwa kuwa hayo ni mambo yaliyofichika hawawezi
katu kuyajuwa. Kusikiya haya Firauni zilimpanda pomoni na akawa ni mwingi wa
wasi wasi. Alifinyangika hapo, na mwisho akatowa amri ya kuuwawa kila mtoto
wa kiyume anayezaliwa na tumbo la Bani Israaiil. Piya alijaza masikiyo na
maaskari waliowalaliya dago wana wa Israaiil, hata ilikuwa wenyewe Bani
Israaiil wakiziyogopa zile nguwo zawo wenyewe wanazozivaa, licha watu. Wengi
kati ya hawo majasusi hasa walikuwa wakunga na wazalishaji wapitawo
majumbani ili kuzalisha ; kwani wawo ndiwo hasa wanaoweza kujuwa nchi kadha
nani kazaa mtoto gani. Bila ya shaka na maaskari wengine piya walikuwemo
kazini.
Jitihada hayiondowi kudura. Alizaliwa Nabii
Muusaa (AS) kwa kificho kikubwa, baada ya Firauni kuteketeza na kuzichinja
zayidi ya roho sabiini elfu za Kibani Israaiil.
__________________________________________
*Hili jina la ni jina la cheo aw la mtawala
wa Misri , si jina la mtu maalum ; ni sawa na kusema Sultan,Mfalme aw
Raisi.
Bibi Yukabid; mke wa Imraan Yahudi ; Mame Muusaa. hapa baada ya kuzaa hakuwa
kama wazazi wengine. Kimaada wazazi huwa na furaha kuu kuwona matunda ya
taabu yake ya si chini ya miezi tisa. Mama Muusaa hakuwa hivyo ila alikuwa
yeye akichunga kila sehemu ya kiwiliwili chake kwa wingi wa hofu alizokuwa
nazo. Kuna wakati hata mtu kayini namna gani, seuze mwenye huruma na hasa
awe mwanamke, humjiya huruma aw tuseme ubinadamu. Hayo ndiyo yaliyomjiya
mkunga kuwona ule uso wa mtoto mchanga unaong`ara kama usiku wa LAILATU
LQADIR . Huruma zake zilimpeleka kwenda kinyume na ile dhamana aliyopewa na
Firauni nayo ni ya kupeleka habari ya kila mtoto wa Kibani Israaiil
azaliwaye. Si kimbaumbi cha chumba na ukumbi hicho kilichokuwepo ndani ya
moyo wa mkunga baina ya kuficha siri hii na kuitowa. Kila akumbukapo makali
ya kisu juu ya shingo ya kijichanga hichi pale pale humjiya sura yake yeye
mwenyewe - kama hakupeleka habari - kumfika haya, huzidi kufinyangika.
Mwisho alipiga moyo konde na kunena:- "Litakalokuwa na liwe. Siri hii
siitowi".
Hakuwahi mkunga kukiwuka kizingiti ila yale
majasusi ya Firauni yalimuwona. Hapo hapo wakayihujumu nyumba ili
wakamnyakuwe huyo aliyezaliwa kama yeye ni mtoto wa kiyume. Nusra wampate
huyo mtoto, lakini kuwa qudra na bahati nzuri dada mtu ndiye aliyewawona
hawo walinzi katika ufa wa mlango. Hakukasiri ila alijusurisha na
kumnong`oneza mama yake, mwili ulichunga sauti yake ilikuwa kama ile ya
sahani ya santuri yenye sindano mbovu. Alimnong`oneza mama, " Mama ! askari
waja. Wanfika hapo nla................." Mama Muusaa hakungoja kusikiya
mwisho wa maneno ila aliruka kuliko ndege na kumbakuwa Muusaa (AS)
akamfunika funika kwa matambara na akamtupa tanurini, bila ya yeye mwenyewe
kujuwa anafanya nini na kwa nini. Bahati nzuri humo tanurini hamukuwa na
moto. Hakuwahi hata kujitenga mbali na tanuri ila askari walikuwa wamejaa
nyumba pamoja na kuyipekuwa kila pembe kwa makini na uangalifu mkuu.
Hawakuwona mtu ila mama Muusaa kasimama thabiti, shuwari kombe kueleya na
ubavuni mwake yupo huyo mwanawe wa kike, kikiri kakara na kazi zake
akizifanya kwa upole kabisa, bila ya kuwonesha kuwa ndani ya nyumba kuna
kitu aw liko jambo lililotokeya.Askari waliipinduwa nyumba juu chini na
walisasambura sawa sawa.
Baada ya wawo kuwona kuwa hawawezi kuwona
kitu walimtikisa mame Muusaa sawa sawa na kumtaka awaelezee ukweli na bila
ya kificho kitu kilichomleta yule mkunga humu ; akisema uongo ataona cha
mtema kuni pamoja na kilichomtowa kanga manyoya.
Yeye aliwajibu moyo imara kuwa huyo
mzalishaji ni miongoni mwa wale waliosafiyana niya. Jambo liliomleta hapa ni
moja tu, nalo ni wazi kuwa hakujiya jambo lolote ila ni kuzungumza tu.
Askari waliondoka hapo mabega yamewashuka kwa kutopata ule mradi wawo.
Yukubid; mama Muusaa alikwisha zake na
wenzake kumtafuta Muusaa (AS) lakini ng`o hakumuwona. Baada ya kuemewa na
kukata tamaa ndipo aliposikia sauti ya kitoto kichanga upande wa tanuri
akamuwokowa mwanawe. Ilikuwa wazi kama muangaza wa mchana kuwa kumficha
mtoto ni jambo la muhali. Inawezekana kufanyika hivyo kwa muda tu. Hapo mame
Muusaa (AS) aliinama na kuvuta fikira zake zote. Baada ya kupita miezi
mitatu. Ilham (Ufunuzi) ya Mola ikamjiya kuwa amtiye mtoto ndani ya
kikakasi nacho akitupe baharini. Bahari kwa upande wake itamtupa hapa
ufukweni. Hapo atachukuliwa na adui wake na Wangu. Aw kama vile
inavyoelezewa katika Quran Tukufu katika aya hii ijayo:-
Ãóäú ÇÞúÐöÝöíåö Ýöí ÇáÊøóÇÈõæÊö ÝóÇÞúÐöÝöíåö Ýöí Çáúíóãøö ÝóáúíõáúÞöåö
Çáúíóãøõ ÈöÇáÓøóÇÍöáö íóÃúÎõÐúåõ ÚóÏõæøñ áöí æóÚóÏõæøñ áóåõ
.
An qdhiifihi fil Ttaabuuti ; Faqdhiifihi
Fii Yammi. Fal yulqihi l Yammu bis Saahili Yaakhudhuhu `Aduwwun lii wa Lahu
(Surat `Taaha : 39).
Mama mtu hakuwa na njiya nyengine ila
kufuwata ule wahy wa mbinguni na kufanya vile alivyoamrishwa na Muadiwa.
Kikakasi kilijazwa pamba pande zote kabla kutiwa kipenzi Muusaa (AS).
Alikuwa mguu nenda, mguu rudi akiyenda zake pwani kulitupa sanduku. Baada ya
kulitosa kasha baharini aliduwaa na kukaa hapo hapo pwani miguu hayiwezi
kwenda akiyatazama mawimbi ya maji yakipiga huku na huko, yakenda na kurudi.
Alihisi kuwa duniya yote ni hivi hivi na moyo wake bila ya shaka unapiga
kuliko hivi. Hakuondoka hapo ufukweni ila baada ya kukamata mkono na mwanawe
wa kike na kumongoza mpaka nyumbani.
Pwani walikuwepo watumishi wa kike wa
Firauni. Kukiyono tu kikasi walikivamiya na kukinyakuwa na kwenda nacho kama
BIARUSI hadi kwa bibi yawo Asiya, mke wa Firauni.
Kitoto kichanga baada ya kufunguliwa
kikakasi kilikuwa kimenyanyua uso wake mchesi wenye wingi wa bashasha na
unaong`aa na kumtazama Asiya. Moyo wa Asiya ulipasuka "ppaa" na kujaa furaha
kwa vile yeye hana mtoto na hii hapa qudra Illahiya imemleteya mtoto huyu
mzuri asiye kifani kuwa ni mwanawe. Akiwa akifikiriya hivi walimjiya askari
kumtaka huyo mtoto wakamchinje. Asiya akawambiya wakamwite bwana wawo. Kuja
Firauni Bibi Asiya akamuwomba asimuuwe mtoto huyu kwani yeye ni raha ya
macho yangu na yako. Usimuue, huenda akatufaa, aw tukamfanya mtoto wetu.
æóÞóÇáóÊú ÇãúÑóÃóÉõ ÝöÑúÚóæúäó ÞõÑøóÉõ Úóíúäò áöí æóáóßó áóÇ ÊóÞúÊõáõæåõ
ÚóÓóì Ãóäú íóäÝóÚóäóÇ Ãóæú äóÊøóÎöÐóåõ æóáóÏðÇ æóåõãú áóÇ íóÔúÚõÑõæäó (9)
Qurratu `Ainin Lil Wa Laka, Laa Taqtuluuhu `Asaa
an Yanfaanaa aw Nattakhidhuhuu Walada (Suratil Qasas: 9).
Firauni alikunja uso kama kipande cha papa
na kujibu kwa hamaki kuu, "Huyu mtoto mzuri kwako wewe. Mimi sina haja naye
katu " Pale pale aliruka na kumyakuwa huku akisema, "Laa ! Sivyo ! Haiwi !
Muhali ! Mtoto huyu hana haki ya kuwishi dakika moja zayidi. Huyu asije
kuwa ni katika Bani Israaiil. Haiyumkiniki! Ila hilo. Kumchinja tu. "Palikuwa
pata shika, nguwo chanika, chumba kikiruka vumbi na hali halikuwepo kwa
wingi wa kufagiliwa. Aibu mwanamke kushindwa katika lile alitakalo na hali
yakuwa kapewa kila silaha kali ya kupigana kuliko hizo Tommy gun na stun gun
. Asiya alishinda na Firauni akatoka yumo katika kunguruma na kulaani tu.
Hapo tena Asiya alipata kazi ya kutafuta mtu wakumyonyesha mtoto. Kwani
ilikuwa kila ziwa apewalo yeye halilitaki. Kwa vile alivyokuwa mama Muusaa
(AS) kamtowa mwanawe wa kike kutafuta habari zake, kwa kumfuata kwa mbali
alitokeya na yeye kufika hapa. Hapo alinena, "Jee, nikuelezeni mtu wa
kumtazama na kumshughulikiya kwa kumuoneya huruma na kumnasihi..?" Watu
waliokuwepo hapo walinena, "Wewe, bila ya shaka unawajuwa wazee wake. Kwa
nini basi ukasema kama hivi. Haya hayasemi ila yule awajuwaye watu wake mtu
vilivyo.
Dada yake Muusaa (AS) kwa bahati akaweza
kujirusha mbali na mtego huwo, kwa kunena , "Jambo ni wazi na jepesi
kuliko hivyo mnavyolifikiri ninyi. Hapana kitu zayidi ila kuwa nawajuwa kuwa
wawo ni watu wazuri na wenye tabiya njema na wana huruma
sana.
Sifa hizi na nyenginezo, zinamvutiya mtoto kuwapenda. Kupewa mwanawe
kumjaribu kumyonyesha watu wote hapo walipigwa na mshangawo kwa kumuwona
Nabiya Allah Muusaa (AS) alivyolivamiya ziwa na kulinyonya, na hali yakuwa
kabla ya hapo kila ziwa alilopewa hakulikubali.
Baada ya kuwonekana kuwa keshapatikana
myonyeshaji wa mtoto, walimchukuwa mpaka kwa Asiya * mke wa Firauni
kumnyonyesha huyo mtoto mzuri. Asiya alimwambiya mame Muusaa (AS) :- "Unaonaje,
si bora ukaye hapa petu ili umyonyeshe huyu mtoto mzuri hapa kuliko
kumchukuwa nyumbani kwako ..? Mame Muusaa (AS) akajibu :- "
Kama itakupendeza bibiye na kama
utanipa ruhusa, basi mimi naoneleya ni bora nimchukuwe kwangu nyumbani.
Naogopa watoto wangu wasije kuharibika kama mimi nitakuwa mbali nao.
MLEZI WA MTOTO NI MWANAMKE, USISIKIYE YA KUAMBIWA NA WATU WASIYOYAFAHAMU
MAMBO VIZURI..".
Baada ya mashindano marefu na pata shika
kubwa, mame Muusaa (AS) alipewa ruhusa ya kumchukuwa Muusaa (AS) nyumbani
kwake na kumleya pamoja na kumnyonyesha huko huko. Jambo hili la kukaa
pahala penye neema na kila raha na starehe na kutaka kwenda kwake na
kuhiyari kula ugali na chachu kuliko yale mabiriani na mabaqlawa, huwenda
likawastaabisha watu wengi. Wawo kama kidogo tu watazingatiya watajuwa kuwa
ule msimamo wake wa inadi ni wa maana kubwa na piya mshangao wawo wote
utaondoka pindi sisi tukikumbuka kuwa wanyonyeshaji wote walishindwa
kumnyonyesha Nabiyya Allahhi Muusaa (AS) isipokuwa ziwa hili la mama yake
mzazi tu ndilo alilolikubali. Kwa hiyo ilimfanya mame Muusaa (AS) awone na
kuhisi kuwa yeye ndiye mwenye nguvu hapa sasa kwa vile ajuavyo namna gani
Asiya anakipenda hichi kitoto kichanga, Muusaa (AS). Hali ni kama hivyo, kwa
nini basi hashiki kani ya kutaka kumchukuwa Muusaa ili huko apate
kumuwonesha mapenzi ya dhati ya Umama bila ya kuogopa kitu kwa vile hapana
wa kumpeleleza. Huko nyumbani yeye atakuwa mbali na macho ya majasusi wa
Firauni.
_____________________________________
*Asiya, mke wa Firauni, inasemekana kwamba
alikuwa Muislamu na ndiye aliemuomba Mola wake amjengee nyumba Peponi na
amuepushe na Firauni na amali zake mbaya
Uzuri wake ni kuwa yeye huku atakuwa na
uhuru kamili na hata wa kuyamimina mapenzi yake yote yaliyomo kifuwani mwake
kwa mwanawe.
Law kwamba yeye kasaliya kwa Firauni, basi
moja kati ya mawili lazima ingelimbidi kufanya, nayo yote ni magumu
hayatendeki :- Hapo ingelimlazimu kuyaficha mapenzi yake kwa mwanawe aw
ingalimpasa ayazike hasa ili watu wasimtiliye shaka baina yake na Muusaa
(AS). Nani, jamani, awezaye duniyani kuyaficha kikweli kweli mapenzi yake
kwa muda mrefu bila ya kujulikana na mtu ? Taabu ! Vipi tutamtarajiya mama
kuyaficha mapenzi yake juu ya mwanawe ? Muhali !
Ilivyokuwa si jambo jepesi mtu kuficha
mapenzi yake juu ya mtu fulani kwa watu ;kwa hivyo inaonesha lazima ayaweke
wazi, aw laa si hivyo, hawo watu anaowaficha watayagunduwa, kiyama chake !
Mapenzi yake yakiwa yanajulikana, watu watatiya shaka shaka kuwa huyu ni
mwanawe. Wakiwa na shaka watamchunguwa na watajuwa. Wakijuwa mauti tayari. |