|
|
BIBI MARYAM
MAMA YAKE
NABII IISAA (AS) |
ÞóÇáóÊú Ãóäøóì íóßõæäõ áöí ÛõáóÇãñ æóáóãú íóãúÓóÓúäöí ÈóÔóÑñ æóáóãú Ãóßõäú
ÈóÛöíøðÇ(20) ÞóÇáó ßóÐóáößö ÞóÇáó ÑóÈøõßö åõæó Úóáóíøó åóíøöäñ
æóáöäóÌúÚóáóåõ ÂíóÉð áöáäøóÇÓö æóÑóÍúãóÉð ãöäøóÇ æóßóÇäó ÃóãúÑðÇ ãóÞúÖöíøðÇ(ãÑíã
20-21)
Qaalat Annaa yakuunu li ghulaamun walam
yamsasni Basharun walam aku baghiyyaa?! Qaala kadhaaliki qaala Rabbuki huwa
`Alayiya hayyimun , wa linaj-`alahu aayatan linnasi wa Rahamatan Minnaa, wa
kaana amran maqdhiyya. (Surat Maryam : 20-21 )
Mwanamke ye yote, hata mnyama aw mti, hawezi
kuzaa bila ya mwanamume. Hapana ubishi. Kwa qudra Yake Mwenyewe Mola, Nabiya
Llaahi Iisaa (AS) kazaliwa bila ya baba wa aina ye yote ile itakavyomkinika.
Bibi Maryam katukuzwa na kusifiwa na Muumba kutokana na kila aina ya uchafu.
Huku kumzaa Iisaa (AS) ni miongoni mwa miujiza Yake Mwenyewe Mwenye enzi
Mungu.
Kazaliwa Maryam
katika nyumba ya dini na ya utawa sana. Mama yake aliposhika mimba aliweka
nadhiri kuwa hicho kitakachozaliwa kutoka tumboni mwake atakitowa kitumikiye
dini huko katika Sinagongi (Msikiti wa Kiyahudi na wala si kanisa la
Kinasara). Alipozaa akanena, :Ewe Mola wangu nilichozaa ni mtoto wa kike na
mwanamke si sawa sawa na mwanamume ; na mimi nimemwita Maryam. Nakuomba Mola
wangu umuwepushe yeye na vizazi vyake na shetani. " Mola akamtakabaliya, aw
kama vile ilivyoeleza Quran Tukufu.
ÅöÐú ÞóÇáóÊú ÇãúÑóÃóÉõ ÚöãúÑóÇäó ÑóÈøö Åöäøöí äóÐóÑúÊõ áóßó ãóÇ Ýöí ÈóØúäöí
ãõÍóÑøóÑðÇ ÝóÊóÞóÈøóáú ãöäøöí Åöäøóßó ÃóäúÊó ÇáÓøóãöíÚõ ÇáúÚóáöíãõ(35)
ÝóáóãøóÇ æóÖóÚóÊúåóÇ ÞóÇáóÊú ÑóÈøö Åöäøöí æóÖóÚúÊõåóÇ ÃõäúËóì æóÇááøóåõ
ÃóÚúáóãõ ÈöãóÇ æóÖóÚóÊú æóáóíúÓó ÇáÐøóßóÑõ ßóÇáúÃõäúËóì æóÅöäøöí
ÓóãøóíúÊõåóÇ ãóÑúíóãó æóÅöäøöí ÃõÚöíÐõåóÇ Èößó æóÐõÑøöíøóÊóåóÇ ãöäú
ÇáÔøóíúØóÇäö ÇáÑøóÌöíãö(36)ÝóÊóÞóÈøóáóåóÇ ÑóÈøõåóÇ ÈöÞóÈõæáò ÍóÓóäò
æóÃóäúÈóÊóåóÇ äóÈóÇÊðÇ ÍóÓóäðÇ æóßóÝøóáóåóÇ ÒóßóÑöíøóÇ ßõáøóãóÇ ÏóÎóáó
ÚóáóíúåóÇ ÒóßóÑöíøóÇ ÇáúãöÍúÑóÇÈó æóÌóÏó ÚöäúÏóåóÇ ÑöÒúÞðÇ ÞóÇáó íóÇãóÑúíóãõ
Ãóäøóì áóßö åóÐóÇ ÞóÇáóÊú åõæó ãöäú ÚöäúÏö Çááøóåö Åöäøó Çááøóåó íóÑúÒõÞõ
ãóäú íóÔóÇÁõ ÈöÛóíúÑö ÍöÓóÇÈò (37) ((ÇáÚãÑÇä 35-37))
Idh Qaalat Mraatu `Imraana Rabbi inni
nadhartu laka maa fii batni muharraran, fataqabbal minnii innaka Ssamii`u
L`aliim. Falammaa wadhaathaa untha qaalat Rabii Inni wadha `utuhaa unthaa wa
Llaahu A`alamu bima waghaat-ha wa Laisa dhdhakaru Kal unthaa wa inni
samaituhaa Maryam. Wa Inni U`idhuhaa bika wa Dhurriyyatahaa mina
Sh-shataani Rrajiim. Fataqabbalahaa Rabbuhaa biqabuulin hasanini.
Waanbatahaa nabaatan hasanan………(Surat aali `Imraan : 35-37).
Baada ya kifo cha baba yake, Bwana `Imraan,
na Maryam yungali mtoto mchanga, hapa palikuwa pata shika nguwo chanika.
Ugomvi uliyendeleya juu ya nani wa kumleya Maryam. Kutaka kukomesha ugomvi
wakakubaliyana, na kura ikapigwa pale pale. Matokeyo yake, ilikuwa kura
ilimuangukiya Bwana Zakaria, mume wa haloo yake ; mama yake mdogo : Maryam.
Maryam alitumiya utoto wake katika Sinagogi
akiyhabudu na kutumika. Haya yalikuwa kwa ajili ya kutekeleza ile nadhiri ya
mama yake ya kukitowa kiliomo tumboni mwake, wakati alipokuwa na mimba,
kitumikiye sinagongi- yaani msikiti wa Mayahudi.
MARYAM ALIFANYA KAZI HII NA KUYENDELEYA NAYO
KWA BIDII HADI ILE DAKIKA YA MWISHO, WAKATI AMBAWO YEYE ALIPOCHAGULIWA NA
MUABUDIWA NA KUPEWA ILE SIRI KUBWA KABISA,YA HIZO SIRI KUBWA.IMEZIDI SIRI
ZOTE. APAKUCHAGULIWA MWANAMKE MWENGINE YE YOTE YULE WA KUPEWA SIRI HIYO ILA
YEYE TU MWENYE YALE MALEZI TULIYOYATAJA HAPO JUU. KALELEWA KIDINI NA YEYE
KALELEKA. NANI TENA ALIYELELEKA KAMA YEYE, HATA AACHWE MARYAM NA KUPEWA HUYO
MWINGINE. SIRI HII HAWEZI KUYICHUKUWA MTU ILA MWENYE MALEZI MEMA NA YA DINI.
Bibi Maryam akiwa kakaa peke yake
akitafakuri hapo alisikiya sauti ikitoka ndani huku ikinena : "Mweye enzi
Mungu akuleteya maneno ya bishara na ya matumaini mema; nayo ni utazaa YESU
BIN MARYAM ambaye ndiye atakayekuwa mtu mtukufu hapa duniyani na kesho
Akhera; naye atakuwa miongoni mwa hawo L- Muqarabiina "Kusikiya maneno haya
Maryam alisituka bila ya kiyasi na alipigwa na mshangao usio na kifani.
Kinyume nasi lewo. Mtu lewo angeliona fahari.
Baada ya kuchemsha bongo na kuvuta fikira
Maryam aliuliza na kuhoji ili apate kujuwa. Hoja yake ilikuwa vipi yeye
ataweza kuzaa na hali hakuwonana na mtu wala hakuwa mtu mchafu..? Akajibiwa
:- "Amri ya Allah hayifutiki. Hivi ndivyo atakavyo Mola na ndivyo
aamrishavyo. Vyengine hayiwezi kuwa. Na huyu mwanawe atakuwa ni miyujiza
na piya ni rehema kutokana na Mwenye enzi Mungu ; aw kama vile.
Hapo Maryam hakuwa na njiya ila kusalimu
amri na kukaa kungoja hiyo amri ya Mola:-
æÃÐÇ
ÞÖì
ÃãÑÇ ÝÇäãÇ íÞæá áå ßä Ýíßæä
Alikaa hata akahisi kuwa mtoto tumboni naye
anataharuki humo tumboni. Aliyona ayibu gani hii, mwari kuzaa ! Akakimbiya
na kutafuta mahali mbali pa kujificha na kujisitiri.
Wakati wa uchungu wa kuzaa ulipomjiya,
aliyomba du`aa akatike vipande vipande na afilie mbali ili asahauliwe,
astirike na asiayibike katu. (wakati wetu huu wa lewo mtu angelikamatiwa ye
yote akabandikwa mimba hiyo, japo watu wanajuwa kuwa hii si mimba yake. Kwa
kutaka kujidanganya- eti wawo wanajistiri kumbe wamo huwogeleya katika
bahari ya haramu).
Inafika hadi maadui si wa Unasara tu bali
wa dini zote kujusurisha na kunena :
Kwanza lazima nistghafiru kabla sijasema
nini wa wanamsingiziya Mtume wa Mwenye enzi Mungu Iisaa (AS). Wanasema (Astaghfiru
Llaah) kwamba Bibi Maryam alitembea na Yusuf Seremala - Najjar (Carpenter)
ndiwo akazaliwa Nabii Iisaa (AS). Huu ni mwisho wa ujeuri kumsingiziya Mtume
kuwa ni mtoto wa haramu.
Barnabas anasema katika Biblia yake (The
Gospel of Barnabas).
"Alikuwepo mwanamke bikira mtakatifu jina
lake Maryam anayetokana na Daud, aliogopa alipojiwa na Malaika Jibril
aliyemwambia, "Usiogope Mola wako kakupenda na kukuchaguwa wewe uwe mama wa
Mtume atakayepelekwa kwa Mayahudi ili awawongoze katika njiya ya Mungu.
Msichana Maryam akauliza :-
"Vipi itayumkinika nizaye na hali ya kuwa
simjuwi mwanamume ? " Jibril
akajibu :-
"Ewe Maryam, Mungu kaumba mtu bila ya mke,
Yeye anaweza kumfanya ndani yako mtu bila ya mume, kwani hapana kitu muhali
kwake Yeye".
Maryam kuogopa wakati mimba itakapokuwa
kubwa, watu wakijuwa watampiga mawe kama ni adabu ya uzinifu, hapo atamtaka
Yusuf amuwowe. Yusuf alipoona mimba pevu aliogopa lawama ya Mungu akamtenga
mkewe. Usiku akajiwa na Malaika kumwambia :- Usiogope huyu bikira atazaa
mtoto jina lake Iisaa naye hatakunywa mvinyo na vinywaji vikali na wala
hatakula nyama isiyokuwa safi, kwani yeye ni mtakatifu wa Mungu kutoka
katika tumbo lake. Yeye ni Mtume wa Bani Israaiil (Mayahudi).
Kukaa Yusuf akakaa na mkewe milele.*
Tukisoma Agano Jipya tutawona Luka (Luke) na
Matthayo (Matthew) wananasema maneno karibu sawa na ya Barnabas. Ama Marko
(Mark) na Yohana (John) hawataji kitu kuhusu uzazi wa Iisaa (AS). Matthayo
anasema:-
"Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi
:- "Yesu, mama yake alipokuwa anaposwa na Yusuf kabla hawajakaribiyana,
aliyonekana ana mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Naye Yusuf, mumewe kwa
vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumuayibisha, aliazimu kumuacha kwa
siri. Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama Malaika wa Bwana alimtokeya
katika ndoto akisema : "Yusuf mwana wa Daud, usihofu kumchukuwa Mariamu
mkewo, maana mimba yake ni kwa uwezo wa Roho Mtakatifu."
Hayo tuliyonukulu hapo juu yanaonesha wazi
namna gani Uislamu unavyokubaliana na baadhi ya mafunzo ya Unasara. Si ajabu
hayo kwani Mayahudi wanamuamini Mtume Muusaa (AS) tu na Wanasara wanamuamini
Iisaa (AS) na Muusaa (AS), ama Uislamu unawaamini Mitume ya Allah yote laki
moja na kitu bila ya ubaguzi. Muislamu akimbaguwa Mtume mmoja tu basi kesha
koseya.
Pale aliposhikwa na uchungu alijitenda kando
mbali na watu. Baada ya kupasuwa chupa aliyamrishwa autikise mtende ili
tende mbichi zianguke na apate kula. (wanaume chungu nzima hawawezi
kuutikisa mtende ; kwani mtende ni sawa na mnazi ; sembuze mwanamke). Kwa
qudra Zake Mola akawutikisa na zikaanguka tende mbichi akala.
Kuliya kitoto ng`aa walikuja watu wake ili
kumchukuwa na huku wakimmiminia wingi wa lawama ya kumlaumu kwamba jambo
hili katu halikuwahi kutokeya upande wawo, juu ya kuwa wote wale wanamjuwa
kuwa yeye si mchafu wala hapendi uchafu. Hapo hapakuwa na kazi ila kurembeya
makombora juu ya makombora ya laana na malawama.
_________________________________________
* Uislamu unasema Maryam alikuwa bikira bila
ya kuolewa.
ÝóÃóÔóÇÑóÊú Åöáóíúåö ÞóÇáõæÇ ßóíúÝó äõßóáøöãõ ãóäú ßóÇäó Ýöí ÇáúãóåúÏö
ÕóÈöíøðÇ (29) ÞóÇáó Åöäøöí ÚóÈúÏõ Çááøóåö ÂÊóÇäöí ÇáúßöÊóÇÈó æóÌóÚóáóäöí
äóÈöíøðÇ (30) æóÌóÚóáóäöí ãõÈóÇÑóßðÇ Ãóíúäó ãóÇ ßõäÊõ
ýæóÃóæúÕóÇäöí
ÈöÇáÕøóáóÇÉö æóÇáÒøóßóÇÉö ãóÇ ÏõãúÊõ ÍóíøðÇ (31)óÈóÑøðÇ ÈöæóÇáöÏóÊöí æóáóãú
íóÌúÚóáúäöí ÌóÈøóÇÑðÇ ÔóÞöíøðÇ (32) æóÇáÓøóáóÇãõ Úóáóíøó íóæúãó æõáöÏúÊõ
æóíóæúãó ÃóãõæÊõ æóíóæúãó ÃõÈúÚóËõ ÍóíøðÇ (33)
Fa Ashaarat Ilaihi Qaaluu:
“Kayfa
Nukallimu Man Kaana Fil Mahdi Sabiyyaa “Qalaa:
Inniy `Abdu Llaahi; Aataaniuya L-Kitaaba, Wa Ja`Alaniy Nabiyyaa; Wa Jaalaniy
Mubaarakan Ayna Maa Kuntu, Wa Awsaany Bi `Ssalaati Wa Zzakaati Maa Dumtu
Hayyaan, Wa Barran Bi Waalidatiy Wa Lam Yaj-Alniy Jabbaran Shaqiyyaa. Wa
Isalaamu `Alaiyya Yawma Wulidtu Wa Yauma Ub`Athu Hayyaan.
Bibi Maryam aliwapa ishara ili wamsemeze
huyu mtoto mchanga. Wawo wakasema:
“Vipi
tumsemeze huyu mtoto mchanga aliopo katika mlezi? Isa`a akawajibu: Mimu ni
mja wa Mwenye enzi Mungu. Kanipa kitabu na kanijaaliya kuwa ni Mtume.
Akanifanya kuwa ni mwenye baraka po pote pale nitakapokuwa; na akaniwusiya `Salaa
na kutowa Zakaa maadamu mimi ni hayi. Na niwe mwema kwa mama yangu, wala
hakunifanya niwe jeuri jabari na mwingi wa kiburi. Salama na amani
ziniteremkiye mimi pale nilipozaliwa, na wakati wa kufa na pale
nitakapofufuliwa ni hayi”
(Maryam: 29-32)
Yote haya aliyapokeya kimya, moyo shuwari,
hana hila. Hii ni amri ya Mwenye enzi Mungu. Vitabu vikubwa vya Umisheni (Ukristo)
vinaeleza shida alizozipata Bibi Maryam. Alistahamili ukomo wa stahamala ;
na hata aliposhindwa kuvumiliya ilimjiya fikira ya kugura nchi. Alikimbiliya
yeye na mtoto wake - Nabiya Llahi Iisaa (AS) na kwenda naye huko Misri ili
ajiyepushe na maudhi yaliyokuwa kwa wingi.
Hata huko Misri mambo hayakuwa mazuri sana.
Vipi mtoto wa kike aliyehama kwawo kwenda huko ugenini asipomjuwa mtu, huko
hana mbele wala nyuma atawezaje kuleya mtoto kwa raha ? Maisha hapo, bila ya
shaka yalikuwa ni ya shida, ingawa kitu kimoja nacho ni cha maudhi
kilipunguwa.
Kutaka kuendesha maisha ilimbidi kufanya
kazi ya kusokota katani, aw ya kuvuna mazawo ya watu kwa ujira na huku Nabii
Iisaa (AS) yu mbavuni mwake. Yote haya na mengineyo aliyafanya kwa kutafuta
tonge na gwanda ya chongo yake moja.
Mama ni mwenye kushughulikiya habari ya
masomo ya mwanawe. Ilipofika wakati wa kupelekwa kusoma, Maryam hakuchelewa
hata dakika moja, ila aliharakiza kumpeleka Iisaa (AS) kwa mwalimu ambaye
alimfunza kusoma na adabu njema. Baada ya miyaka kumi na mbili kupita, sisi
tunamuwona Maryam na kijana wake Iisaa (AS) wakifunga virago vyawo na mguu
nipate. Hawakusimama na mguu na njiya ila wawo wapo Baitil Maqdis. Hapo tena
walisita na walituwa na kufanya mastakimu yawo kati ya mji wa Nnaasira. Sasa
hapa maisha hayakuwa mabaya kama vile yalivyokuwa katika mazingira ya kabla
; kwa hivyo wawili wawo waliweza kuwishi mpaka Seyyidna Iisaa (AS) akawa mtu
mzima wa kutegemewa.
Taabu zote hizo alizozipata Nabii Iisaa (AS)
hazikuwa ila ni kule kutayarishwa na kupokea Risala ya mbinguni. Alipopewa
Utume, mama yake ndiye aliyekuwa msaidizi wake nyumbani na ndiye hasa
aliyekuwa akimuelezea yale mambo makuu yaliyokuwa yakimfika aliokuwa
akiyawona. Huruma za mama hapo ndipo mahali pake na ndiwo wakati wake wa
kufanya kazi. Kazi kubwa hasa aliyokuwa nayo ni ya kumliwaza, kumtia nguvu
na kumpa moyo wa kuendeleya na ile kazi yake pevu aliopewa na Muabudiwa.
Jukumu hili Tukufu, lazima yule apewaye apate nguzo za kweli za kutegemewa.
Ala ! Tazameni mambo haya jamani ! Huyu
kijana wa miyaka thelathini aliyesimama na huyu bibi makamo hapa juu ya hili
Jabali Zaitun ni nani ? Hawa ni Bibi Maryam pamoja na Nabii Iisaa (AS).
Wamekuja kuchuma zaituni yeye na mama yake, Nabii Iisaa (AS) ilimjiya Ru`yaa
na kujuwa kuwa yeye ni Mjumbe aliyeletwa kwa Bani Israaiil. Hapo hakujijuwa
ila aliona anageuka kuliya kwake na kumuelezea mama yake Maryam, maneno
yenye maana ifuatayo :-
"Tokeya lewo inanibidi zinifike shida mimi
na taabu nyingi sana kwa ajili ya Mwenye enzi Mungu. Baada ya lewo itaniwiya
vigumu na wala sitaweza tena kuwishi pamoja nawe na wakati huwo huwo niwe
naweza tena kutekeleza wajibu wangu wa deni lile la kukutumikia, kwa ule
wingi na ukubwa wa jukumu na dhamana nilizonazo..".
Mama mtu kusikiya haya alinena :-
"Ewe mboni ya macho yangu, mimi
nalitanabahishwa juu ya hayo kabla ya kuzaliwa kwako. Mungu akubariki na
piya akusaidiye juu ya hiyo dhamana yako. Amina".
Iisaa tokeya siku hiyo akatengana na mama
yake ili ashughulikie mambo na mafunzo yake ya dini, baada yakuwa naye kwa
muda wa miyaka thelathini. Wakati wote huwo alikuwa akitayarishwa kwa hilo
jukumu Takatifu. Ingawa hapo juu tulisema kuwa walitengana lakini kwa qudra
na kwa miujiza Yake Mwenyewe Mola walikuwa wakikutana na kuwonana.
Quran imesema kwa wazi kabisa :-
æÌÚáäÇ ÇÈä ãÑíã æÃãå Âíå
Wajaalna bna
Maryam wa Ummah Aayatan
Tumemjaalia mtoto
wa Maryam na mama yake ni miujiza
æÌÚáäÇåÇ æÃÈäåÇ ÂíÉ ááÚÇáãíä
Waja`alnahaa na bnahaa
Aayatan lilamiin.
Tukamjaaliya yeye na mwanawe ni mfano na aya
kwa walimwengu.
|