|
|
BIBI HAAJIR (I)
MAMA YAKE SEYYIDNA ISMAAIIL ( A. S
) |
Bibi Saara, Mke wa Seyyidna Ibraahiim
(Khalilu Rrahman, Alaihi Ssalam), alikaa na mumewe miyaka mingi sana bila
ya wawo kuruzukiwa mtoto : kwa vile alivyokuwa ni tasa. Alikuwa akimpenda
mumewe hadi na akitamani aruzukiwe mtoto.
Baada ya kuchemsha bongo lake sana
aliyoneleya ni bora amtunukiye mumewe huyu mjakazi wake alyetoka naye katika
safari zake za Misri na kwengineko. Hii ilikuwa ni hatuwa iliobarikiwa
kikweli, kwani ndiwo iliokuwa sababu ya kizazi kitukufu kuja hapa duniyani.
Seyyidna Ibraahiim alipokeya tunza hii kwa
furaha kuu na kwa moyo mkunjufu, na hakuchukuwa muda ila Haajir alishika
mimba na Seyyidna Ismaaiil akazaliwa.
Kedi ya kike haishindiki na mwanamke
asiyekuwa na wivu juu ya kitu si mwanamke aw kimeshachujuka kitu hicho.
(Nyuki mkali kwa asali yake).
SAARA BIBIYE, KAKAA NA MUMEWE MIYAKA NENDA
MIYAKA RUDI BILA YA KUZAA.LEWO HICHI KIJAKAZI UKURUTU KIMEWEZA KUPATA KITU
ALICHOKUWA AKIKITAMANI AKIPATE YEYE PAMOJA NA MUMEWE. MAISHA GANI HAYA...!
HERI YA KUWISHI MOTONI KULIKO MAISHA HAYA..!
Nani awezaye kustahamili madhila kama haya
? HAPANA
Bibi Saara wivu ulimfunika vitanga vya macho
na akasahawu kuwa yeye mwenyewe ndiye aliyemtunukiya mwenye Seyyidna
Ibraahiim huyu bibi Haajir na akazaliwa Seyyidna Ismaaiil (AS), Saara
alimsimamiya mumewe kidete ili kumhamisha Haajir pamoja na mwanawe. Hila
zake zote Ibraahiim (AS) zilikwisha. Hapana salama ila tulipomuona Seyyidna
Ibraahiim (AS) anaondoka huko L- Khaliil Filastin (Palestine) na kuyelekeya
kusini na nyuma yake kufuatwa na Bibi Haajir kabeba mtoto wake mgongoni.
Safari yawo hii ya kwenda msitu na nyika ilisita walipofika Makka. Makka
wakati huwo hapakuwa na kitu cho chote ila jangwa lisiloota kitu.
Pahala hapa palikuwa pakipitiwa wakati
fulani na wachunga wanyama na wakati mwengine maharamiya wakipita huku na
huko.
Seyyidna Ibraahiim (AS) alipokuwa anakwenda
zake Haajir ilimjiya hofu akawa anampembejeya asimuwache peke yake hana mtu
ila hichi kitoto kichanga tu kati ya jangwa lenye wingi wa vitisho kwa vile
halina kitu aw watu.
Mwanamume ana sifa ya ukatili na kutokuwa
na huruma. Hatukumuwona Seyyidna Ibraahiim (AS) ila kageuza uso na kakaza
mwendo bila ya kugeuka nyuma ili isije roho yake ikalayinika na kuonesha
huruma pindi akiwatazama usoni. Uso umeumbwa na haya. Kumjibu piya hakuweza
kwa vile isije sauti yake ikawonesha kitetemeshi, na kwa hivyo Haajir huenda
akafichuwa ile siri iliyomo moyoni mwake ; na ni kuwa Ibraahiim (AS) hafanyi
hivi kuwa yeye hampendi. Yeye anafanya hivyo kwa sababu nyengine kabisa.
Katika kukaza kwake mwendo huku alimsikiya
Haajir akisema:"Je!!, Mwenye enzi Mungu ndiye aliyekuamrisha haya..?
Kwa wingi wa majonzi yaliyomjaa yeye alimjibu bila ya kufikiriya aw kuhisi
aw kuzingatiya nini kasema, "Naam..!.
Kusikiya hivi, Bibi
Haajir ilimtoka :- "Kama ni
hivyo, basi Mungu si mtovu". Hapo
aliyinama chini kimya na vile ilivyokuwa kayinama hakuweza kumuwona Seyyidna
Ibraahiim (AS) kanyanyua mikono juu kwa unyenyekevu mkuu na huku akiomba
du`aa na mwili mzima umeelekeya kwa Muumba viumbe vyote.
æóÅöÐú ÞóÇáó ÅöÈúÑóÇåöíãõ ÑóÈøö ÇÌúÚóáú åóÐóÇ ÇáúÈóáóÏó ÂãöäðÇ æóÇÌúäõÈúäöí
æóÈóäöíøó Ãóäú äóÚúÈõÏó ÇáúÃóÕúäóÇãó (35) ÑóÈøö Åöäøóåõäøó ÃóÖúáóáúäó
ßóËöíÑðÇ ãöäú ÇáäøóÇÓö Ýóãóäú ÊóÈöÚóäöí ÝóÅöäøóåõ ãöäøöí æóãóäú ÚóÕóÇäöí
ÝóÅöäøóßó ÛóÝõæÑñ ÑóÍöíãñ (36)
Rabbi J-`al haathaa L-Balada Aaminaan, Wa
Jnuubni wa baniyya ana Na`abuda L-Asnaama. Rabbi Innahunna Adhlalna
Kathiiran Mina Nnaasi, Faman Tabi`any Fainnahu Minniy, Wa man `Asaany
Fainnaka Ghafurrun R`ahiim.
" ............ Mola wangu ! Uujalie mji huu
( wa Makka) uwe wa amani. Na uniepushe mimi na wanangu kuabudu masanamu.
Mola wangu ! Hakika (masanamu) hawa wamepoteza watu wengi. Basi
aliyenifuata ni wangu mimi (utamlipa mema kama ulivyotuahidi) ; na
aliyeniasi (unaweza kumsamehe na usimtese) kwani Wewe ni Mwingi wa msamaha
na Mwingi wa Rehema" (Quraan, Surat Ibraahiim 35-36).
"Ewe Mola nimewaweka
baadhi ya vizazi vyangu mahali pasipoota kitu katika nyumba Yako Tukufu.
Yaa, Rabbi wajaalie wawe wakidumisha `Salaa na uzifanye baadhi ya nyoyo
zinavutika kwawo. Bwana wangu, piya uwaruzuku baadhi ya vyakula na matunda
ili huenda wakakushukuru." aw kama inavyoeleza aya ifuatayo :-
ÑóÈøóäóÇ Åöäøöí ÃóÓúßóäÊõ ãöäú ÐõÑøöíøóÊöí ÈöæóÇÏò ÛóíúÑö Ðöí ÒóÑúÚò ÚöäúÏó
ÈóíúÊößó ÇáúãõÍóÑøóãö ÑóÈøóäóÇ áöíõÞöíãõæÇ ÇáÕøóáóÇÉó ÝóÇÌúÚóáú ÃóÝúÆöÏóÉð
ãöäú ÇáäøóÇÓö Êóåúæöí Åöáóíúåöãú æóÇÑúÒõÞúåõãú ãöäú ÇáËøóãóÑóÇÊö áóÚóáøóåõãú
íóÔúßõÑõæäó (37) ((ÇÈÑÇåíã -37)).
Rabbana inni askantu mindhurriyyatii biwadin
ghairi dhii zarain `inda baitika l Huharrami. Rabbanaa liyuqiimuu `Ssalaata
; faj`al af-idatan mina nnasi tahawii ilaihim Warzuqhum mina ththamaraati
la`allahum yashkuruun (Ibrahiim : 37 )
Baada ya hapo akaongoza njiya ya kwenda zake
kwa mkewe wa pili : Saara.
Hapo Bibi Haajir akawa anajishughulisha na
mwanawe ili apate kujipumbaza na kujitowa majonzi aliyonayo. Kwa njiya hii
hakuhisi ule upweke aliokuwa akiishi ndani yake.
Starehe hii ya mbwa kukaliya mkiya wake
iliendeleya kwa muda tu. Taabu ilikuwa imemkaliya meno wazi. Baada ya
kumalizika chakula tu na maji, na hasa ule wakati Ismaaiil (AS) mchanga
aliposhikwa na kiw ndipo alipoiyona duniya nyeusi.
Haajir hakuwa na jambo jingine wakati huu
ila ni kunyanyuka tu na kuhangayika kutafuta maji. Alipochoka bila ya yeye
kupata kitu alioneleya ni bora apande juu ya jabali, asaa akawona maji aw
dalili ya maji. Kutazama akawona hapana jabali lililo karibu naye ila lile
la `Safaa. Akenda mbiyo na kurudi bondeni mbiyo na akijiuliza, " Jee pana
mtu ? aw nasikiya sauti ya mtu “Baada ya kuwona hapana. Kenda mbiyo Marwa,
kwa tamaa yakuwa hapo ataona alama yo yote ile ya maisha na uhayi. Kumbe :
Ng`ngoo ! ! !
Kusita hapasitiki,
kukaa hapakaliki kwa kukiyona kijitoto kichanga namna kinavyochachatika na
kuhaha kwa wingi wa kiw. Jambo hili lilimfanya Haajir ayende mbiyo na kurudi
baina ya `Safaa na Marwa mara saba ; mbiyo ya mtu aliyeishiwa na kuemewa
hajuwi nini la kufanya. Zilipomkaa na kumpaa pumzi, alianguka juu ya mchanga
mbele ya mwanawe Ismaaiil (AS) huku akingojeya matokeyo ya mwisho yenye
wingi wa huzuni.
ÑóÈøóäóÇ Åöäøóßó ÊóÚúáóãõ ãóÇ äõÎúÝöí æóãóÇ äõÚúáöäõ æóãóÇ íóÎúÝóì Úóáóì
Çááøóåö ãöäú ÔóíúÁò Ýöí ÇáúÃóÑúÖö æóáóÇ Ýöí ÇáÓøóãóÇÁö (38) ÇáúÍóãúÏõ
áöáøóåö ÇáøóÐöí æóåóÈó áöí Úóáóì ÇáúßöÈóÑö ÅöÓúãóÇÚöíáó æóÅöÓúÍóÇÞó Åöäøó
ÑóÈøöí áóÓóãöíÚõ ÇáÏøõÚóÇÁö(39) ÑóÈøö ÇÌúÚóáúäöí ãõÞöíãó ÇáÕøóáóÇÉö æóãöäú
ÐõÑøöíøóÊöí ÑóÈøóäóÇ æóÊóÞóÈøóáú ÏõÚóÇÁö(40) ÑóÈøóäóÇ ÇÛúÝöÑú áöí
æóáöæóÇáöÏóíøó æóáöáúãõÄúãöäöíäó íóæúãó íóÞõæãõ ÇáúÍöÓóÇÈõ(41) ((ÇÈÑÇåíã
38-41))
Rabbanaa Innaka Ta`alamu Maa Nukhfii, wa maa
Nu`ulinu, Wa Maa Yakhfaa `Ala Llaahi Min Shay-in fil Ardhi Walaa fis Samaa:
Al`Hamdu Lillaahi Lladhii Wahaba Lii `Alaal Kibari Ismaa`iila wa Is-Haaqa;
Inna Rabbi Samii`u Ddu`aa. Rabbi J`alnii Muqiima S`salaati Wa Min
Dhurriyatii. Rabbanaa Taqabbal Du`aa. Rabbaanaa Ghfir Lii Wa Liwaalidayya Wa
Lil Mu`uminiina Yawmma Yaquumu L-Hisaab.
"Mola wetu ! Hakika Wewe unajuwa siri yetu
na tunavyodhihirisha. Na hapana kifichikacho Kwako, cha ardhini aw cha
mbinguni. Namshukuru Mwenye enzi Mungu kunijaaliya juu ya uzee wangu
kuwapata Ismaaiil na Is-haaq, Hakika Mola wangu ni Mwenye kusikiya du`aa.
Ewe Mola ! Nijaaliye nidumishe `Salaa na vizazi vyangu, Bwana wetu
tupokelee du`aa zetu. Mola wetu ! Nighufirie mimi na wazee wangu na Waislamu
wote siku ya Qiyama" (Ibraahiim 38-41).
ÑóÈøóäóÇ æóÇÌúÚóáúäóÇ ãõÓúáöãóíúäö áóßó æóãöäú ÐõÑøöíøóÊöäóÇ ÃõãøóÉð
ãõÓúáöãóÉð áóßó æóÃóÑöäóÇ ãóäóÇÓößóäóÇ æóÊõÈú ÚóáóíúäóÇ Åöäøóßó ÃóäúÊó
ÇáÊøóæøóÇÈõ ÇáÑøóÍöíãõ (128) ÑóÈøóäóÇ æóÇÈúÚóËú Ýöíåöãú ÑóÓõæáðÇ ãöäúåõãú
íóÊúáõæ Úóáóíúåöãú ÂíóÇÊößó æóíõÚóáøöãõåõãú ÇáúßöÊóÇÈó æóÇáúÍößúãóÉó
æóíõÒóßøöíåöãú Åöäøóßó ÃóäúÊó ÇáúÚóÒöíÒõ ÇáúÍóßöíãõ (129) (( ÇáÈÞÑå
128-129))
Rabbanaa Wa J-`Alnaa Muslamayni Laka, Wa Min
Dhurriyatinaa Ummatana Muslimatan Laka, Wa Arinaa Mnaasikanaa; Wa Tub
`Alaynaa, Innaka Anta Ttawwaabu Rra1hiim. Rabbanaa Wa B`Ath Fiihim Rasuulan
Minhum, Yatluu `Alaihim Aayaatika Wa Yu`Allimuhumul Kitaaba Wal-Hikmata Wa
Yuzakkiihim Innaka Anta L-Aziiza L-`Hakiim
"Mola wangu ! Tufanye tuwe wanyenyekevu sisi
wawili pamoja na baadhi ya vizazi vyetu,utuongoze njiya njema na utusamehe.
Ewe Mola ! Uwaletee Mtume kutokana nawo awafunze Kitabu Chako na dini Yako
na ilimu nyengine, ili wajitakase na kila baya ". (Al Baqra :
128.........129 ).
Hapakumuweka hapo ila tunamuwona kasimama,
kama aliyechagawa, kwa wingi wa zile kelele za kitoto zilizokuwa zikimkata
maini na kuwona maisha ya mwanawe yanatoweka. Hapo alijikusanya kusanya na
kusema " Sitakaa na kuwona kwa macho yangu kifo cha mwanangu na
niliyemuoneya machungu . " Ya Allah !!" Hapo mandhari hayisemeki namna
ilivyokuwa ikitisha. Kila kitu hapo kilikuwa kimesita, sauti haisikilizani,
upepo hauvumi na hata pumzi hazikuwa zikisikika. Vitu vyote vikingoja dakika
ya mwisho. Pahala hapo hapakuwa na kiumbe cho chote ila wanyama wa mwitu tu.
Labda wawo waliharakisha hii dakika ya mwisho ili wapate kunufaika.
Haajir kasema kweli :- " Mungu si mtovu "
uokovu Wake papo hapo ukaja kwa kupasuka MAJI YA ZAMZAM. Kuwona
Haajir maji haya alikuwa na nguvu za zayidi ya simba. Alijiyona sasa yeye
anaweza kuichukuwa duniya nzima kwa mkono mmoja tu. Nani kama Haajir? Mungu
kamrehemu mja Wake kwa kumteremshiya maji kutoka mbinguni. Neema ilioje hii
! Hapana tena.
Kwa nini Haajir asiwe hivyo na hali Quran
inasema wazi na kwa kinywa kipana :-
(
æÌÚáäÇ ãä ÇáãÇÁ ßá ÔÆ
Íí
)
{ Waj`alanaa mina l maai kulla shaiin
hayyi }
“Tumejaaliya uhayi wa kila kitu uwe
unatokana na maji "
Mishipa ya maisha iliyanza kidogo kidogo
kupiga pembezoni mwa Zamzam. Kama vile ujuwavyo kila msafiri kuwa dalili ya
kukurubiya pahala penye maisha ni kuwona ndege. Kwa hiyo basi, wote wale
waliyokuwa wakipita karibu na Makka waliduwaa kuwona ndege kati ya hili
jangwa.Baada ya kupagunduwa mahali patokapo hayo maji wengine walitaka
ruhusa ya kuwishi hapo . Haajir aliyapokeya maombi yawo kwa ule moyo wake
mkunjufu. Inasemekana wakaazi mwanzo walikuwa ni wa kabila ya Jurhum.
Kidogo kidogo watu wakawa wanakuja kuwishi
hata lewo ikawa Makka ina wakaazi wengi sana, na ndipo wayelekeyapo Waislamu
wa duniya nzima wakati wa Salaa. Piya kwenda mbiyo za `Safaa na Marwa ni
kazi mpaka hii lewo ifanywayo na kila Muislamu aendaye kuhidji Makka aw
kufanya Umrah kwa ajili ya kule kutekeleza nguzo ya tano ya Uislamu.
|