بِسْمِ اللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1. Aya tukufu:
﴿وَٱتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ ٱبْنَىْ ءادَمَ بِٱلْحَقّ إِذْ قَرَّبَا قُرْبَـٰناً فَتُقُبّلَ مِن أَحَدِهِمَا وَلَمْ يُتَقَبَّلْ مِنَ ٱلآخَرِ قَالَ لاَقْتُلَنَّكَ قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ ٱللَّهُ مِنَ ٱلْمُتَّقِينَ﴾
﴾Na soma juu yao habari ya watoto wawili wa Adam; wakati walipopeleka sadaka zao; basi ilikubaliwa kwa mmoja wao na haikukubaliwa kwa mwengine. Akasema: Hakika nitakuua". Akasema: Hakika yalivyo ni kua anakubali Allah kwa Wachamungu﴿
[Maidah 27]
2. Hadithi ya wiki:
وَرُوِيَ أَنَّ سَائِلاً سَأَلَ فَقَالَ: يَا رَسُوْلَ اللهِ أَيُّ الْمُؤْمِنِيْنَ أَكْيَسُ؟ فَقَالَ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَكْثَرُهُمْ لِلْمَوْتِ ذِكْراً، وَأَحْسَنُهُمْ لَهُ اسْتِعْدَاداً. أُولَئِكَ الأَكْيَاسُ ذَهَبُوْا بِشَرَفِ الدُّنْيَا وَكَرَامَةِ اْلآخِرَةِ"
"Imepokewa kua mwenye kuuliza aliuliza: Ewe Mjumbe wa Allah hivi ni nani Katika Waumini mwenye busara zaidi? Basi Mtume (s.a.w) alisema: Ni yule aliyekua ni mwingi zaidi wa kukumbuka mauti, na mwenye kujitayarisha vizuri zaidi kwa ajili ya hayo mauti. Hao ndio wenye busara; wameondoka pamoja na Utukufu wa Dunia na Cheo cha Akhera"
3. Hekima ya wiki:
"Ubora wa Uislamu wa mtu ni kuacha lisilomuhusu"
4. Dua ya wiki:
Inapokaribia Magharibi sema hivi:
اللَّهُمَّ بِكَ أَمْسَيْتُ، وَبِكَ أَصْبَحْتُ، وَبِكَ أَحْيَا، وَبِكَ، أَمُوْتُ وَإِلَيْكَ الْمَصِيْرُ
"Allahumma bika amsaytu, wabika asbahtu, wabika ahyaa, wabika amuutu, wailayka lmaswiir"
"Ewe Mola wangu; kwa kutaka wewe nimeingia jioni, na kwa kutaka wewe ninaing asubuhi, na kwa kutaka wewe niko hai, na kwa kutaka wewe nitakufa, na kwako wewe ndio Marejeo"
Wassalamu alaykum
Msikiti wa Ibadhi Bujumbura
20/08/1426H



