BARUA YA no: 3

Imeandikwa na: Khalid Nassor

                          Kutoka: U.K

Soma  barua Iliyopita

BARUA HII IMESHASOMWA NA WATU:

Web Page Hit Counter

KUHIFADHI QURAAN

Assalam alaikum warahmatullah wabaratuh

 Mwenyezi Mungu kasema katika Qur'ani:

Åöäøó ÇáøóÐöíäó íóÊúáõæäó ßöÊóÇÈó Çááøóåö æóÃóÞóÇãõæÇ ÇáÕøóáóÇÉó
æóÃóäÝóÞõæÇ ãöãøóÇ ÑóÒóÞúäóÇåõãú ÓöÑøðÇ æóÚóáóÇäöíóÉð íóÑúÌõæäó ÊöÌóÇÑóÉð
áøóä ÊóÈõæÑó.
 


Hakika wale wanao soma Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na wakashika Sala, na
wakatoa kwa siri na kwa dhaahiri katika tulivyo waruzuku, hao hutaraji
biashara isiyo bwaga. (Fatir 35:29)

Othman ibn Affan kataja kuwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu  kasema: "Alokuwa
bora miongoni mwenu ni yule anayojifunza Qur'an, halafu akaisomesha. "
[Al-Bukhari].

Haya yafuatayo ni dokezo kuhusu jinsi gani ya mmoja kujisaidiya kuhifadhi
Qur'an zilotajwa na Sh. Osama Abdul-Azeem wa Al-Azhar Cairo.

1) Kwanza, hakikisha unatubu kwa Mwenyezi Mungu kwa madhambi yako
unayofanya, kwasababu madhambi hayawachi chumba kwa maneno ya Mwenyezi
mungu.

2) Weka niyya yako tayari, na zingatia akilini ijaza ya mmoja anayopata
katika kuhifadhi Qur'an. Muombe Mwenyezi mungu kukusaidiya kutizima hii.

3) Towa masaa yako machache katika siku ya kukaa ukadurusu na kuhifadhi.
Hii iwe kipindi ambacho huna kazi nyengine, wala hapana fujo.

4) Tumiya kopi hiyo hiyo ya Qur'an kila siku. Hii kwasababu akili yako
inachukuwa ‘snapshot’ ya karatasi.

5) Anza na Surah ambao ni rahisi kwako.

6) Surah nyengine zakuanza ni zile ambazo unazipenda ukizisoma, na zile
ambazo unazisikiliza sana na ambazo pengine ushaanza kuzihifadhi baadhi ya
sehemu.

7) Kila ukiwa umri wako mdogo ndio bora zaidi. Kwa sababu kila ukiwa mkubwa
kichwa chako kinajaa na mambo mengine. Lakini kwenye kujifunza daima
hakuna kuchelewa. Ikiwa hukupata kuhifadhi Qur'an udogoni basi bado unao
muda wakuanza tena.

8) Baada yakuisha baadhi za ayah, zisome katika sala ifuatayo ya nafl
(sala za hiari). Kila muda jaribu kudurusu mbele ya familia yako au
rafiki.

Mwisho, itakuwa vyema tu kudurusu katika kikundi cha watu, hii inasaidia
kusaidiana miongoni mwenu. Ikiwa una jaribu kuwahifadhisha watoto wako
unaweza kuwafanyiya kila anayomaliza anapata zawadi yakuisha kuhifadhi
surah flani hii itawasaidiya watoto kuwa na hamu na kile kitu.

Mwenyezi Mungu Inshallah atusaidiye kutenda mema. Amin.


Khalid Nassor
 

Copyright © 2005  uislamu.net