|
ASIYEWEZA KUFUNGA |
| Suala 1: Nini neno (jawabu) lenu kwa yule asiyeweza kufunga saumu ya ramadhani, kwa sababu ya maradhi na kuwa mzee wa miaka, je anaweza kukodi mtu wa kumfungia ramadhani? |
|
Jawabu:
Haitakikani mtu ambae hawezi kufunga kukodi mtu mwingine
amfungie ramadhani. Lakini alishe maskini mmoja kwa kila siku ikiwa hawezi
kufunga wala kulipa baada ya kupita muda wake na wala hategemei kuwa
atapata hali itamuezesha kufunga saumu au kulipa hizo saumu zilizompita.
Na asili ya jambo hili ni maneno ya Mwenyezi Mungu : (Na
wale wasio weza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini).
(Mwenyezi
Mungu ndie mjuzi wa kila kitu)
|
|
Suala 2:Bibi mzee ametia nia ya kufunga mwezi wa Rajab wote, akafunga siku kumi za mwanzo kisha hakuweza kukamilisha. Je inamjuzia afungue(afutari), na je anayo kafara ikiwa hatakamilisha kufunga mwezi alio utilia nia kufunga? |
|
Jawabu: Ikiwa hii saumu aliyoitilia nia ni nafila haimlazimiki kukamilisha mwezi isipokuwa siku aliyoamka huku amefunga. Na likiweko lolote jingine yeye ni amira (anaijua) wa nafsi yake akitaka atafunga akitaka atafungua.
|
| Suala 3: Mtu hawezi kufunga siku kumi kwa pamoja (mfululizo), lakini anaweza kufunga siku mbili kwa pamoja kisha apumzike kisha anafunga tena siku mbili kwa pamoja. Je kuna chochote juu yake? |
|
Jawabu:
Alipe siku hizo kwa
kuzitenganisha, ikiwa hawezi kuzilipa zote kwa pamoja (mfululizo).
|
| Suala 4:Mtu ana maradhi ya figo (Kidney) na anafanyiwa matibabu ya kusafishwa figo kila wiki mara mbili, na kila kusafisha figo kunachukua masaa manne (4Hrs). Nini juu yake akiwa hawezi kufunga kwa sababu hiyo ya kusafishwa figo? |
|
Jawabu: Ikiwa kusafishwa figo kuta mfanya (kuta mbidi) afungue, basi afungue kisha azilipe siku alizofungua. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).
|
|
Suala 5:Mtu ana maradhi ya moyo akafunga siku kumi na tano za ramadhani, kisha Doctor (mganga) akamkataza asifunge. Nini afanye? |
|
Jawabu:Asifunge
katika hali hii, akiwa anategemea kupona na kuweza kufunga siku za mbele
basi azilipe hizo siku alizo fungua, na akiwa hategemei kupona na kuweza
kuzilipa basi alishe maskini mmoja kwa kila siku aliyo fungua.
(Mwenyezi Mungu ndie
mjuzi wa kila kitu).
|
| Suala 6:Mtu amekutwa na maradhi ya sukari na maradhi mengineyo, hajaweza kufunga ramadhani kwa sababu ni lazima anywe dawa mchana wa ramadhani. Nini ina mlazimikia? |
|
Jawabu:
Ikiwa hategemei kupona, basi alishe kila
siku aliyo fungua maskini mmoja.
(Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).
|
| Suala 7: Mtu alikuwa mgonjwa katika mwezi wa ramadhani baada ya kupita siku kumi ilipo anza ramadhani akafariki dunia. Nini ina mlazimikia mtoto wake katika hii hali? |
|
Jawabu: Ikiwa hakufunga siku kumi ilipoanza ramadhani kabla ya kufa kwake, na hajalisha maskini kwa kuacha kufunga hizo siku kumi. Basi mtoto wake amfungie (amlipie) baba yake hizo siku kumi au alishe maskini mmoja kwa kila siku baba yake aliyofutari(aliyo fungua), (yaani alishe maskini kumi, kwani baba yake alikuwa hakufunga siku kumi alipokuwa hai). (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).
|
| Suala 8: Mtu mzee na amelazwa Hospitali (amepata kitanda) , na hajafunga ramadhani mbili na yeye ni fakiri wa hali na mali, hawezi kulisha maskini. Nini juu yake? |
|
Jawabu:
Ikiwa hawezi
kulisha maskini na hawezi kufunga Mola ni mbora wa kusamehe, kwani nafsi
haijikalifishi ila lile inayoweza kufanya. (Mwenyezi
Mungu ndie mjuzi wa kila kitu).
|
|
Suala 9: Nini neno (jawabu) lenu kwa mtu aliyekuwa amesafiri na Doctor (mganga) muislamu akamnasihi asifunge ramadhani na wala asifunge siku nyingine zozote zile kwa sababu afya yake inadhurika kwa kufunga. Nini afanye? |
|
Jawabu:
Afungue kisha alipe pale Mwenyezi Mungu
atakapo mpa uwezo wa kuwa na afya.
(Mwenyezi Mungu ndie
mjuzi wa kila kitu).
|
|
Suala 10: Nini ina niwajibikia mimi juu ya mama yangu, ambae hajaweza kusali wala kufunga katika mwezi wa ramadhani kwa ajili ya maradhi makali, na amefariki wala haja usia, na alipoteza fahamu katika mwisho wa maisha yake? |
|
Jawabu: Ama kuwa ni wajibu si wajibu kwako kufanya lolote lile, ama kuwa ni ihsan basi inapendeza ulishe kila siku aliyo kuwa haku funga na huku ana akili yake timamu maskini mmoja. Ama siku ambazo alipoteza fahamu basi hana taklifu yeyote ile juu yake, na ina takikana pia utoe sadaka kwa ajili yake na umu ombee maghfira kwa utakavyo weza. (Mwenyezi Mungu ndie mjuzi wa kila kitu). |