AINA
ZA SUMU
Vifungu vya Saumu:
Saumu imegawika vifungu
vinne:
1-Saumu iliyo wajibu (faradhi).
2-Saumu iliyo haramu.
3-Saumu iliyo himizwa.
4-Saumu iliyo makruhu.
Saumu iliyo wajibu ni:
Saumu ya Mwezi wa Ramadhani,
Saumu ya nadhiri, Saumu ya kaffara; kaffara ya kuuwa, kaffara ya “Dhihar”
(mume kumwambia mkewe: wewe kwangu ni kama mgongo wa mama yangu basi
anaharimika kwake mpaka atoe kaffara), Kaffara ya “Ilaau” yaani mwanamme
kuapa kuwa hatamwingilia mkewe basi hatoweza kumuingilia mpaka atoe
kaffara, kaffara ya kwenda kinyume na kiapo chake na Saumu ya Attamatuu
kwa yule asieweza kumiliki kuchinja na kirefu cha haya kitapatikana katika
vitabu vya Fiqhi.
Saumu iliyo Haramu:
Kufunga katika Idi mbili
(Al-Fitri na Al-Adh-haa) na kufunga kwa aliye katika hedhi na ujusi (kwa
mwanamke) na kufunga siku ya shaka nayo ni tarehe 30 thelathini shaabani
haifungiwi siku hii ili isiongezeke siku katika Ramadhani kutoka mwezi
mwengine. Kama ilivyosemwa kutokana na Ikrima R.A. na Ammar R.A. wamesema:
Aliyefunga siku inayotiliwa shaka basi amemuasi Aba Al-Qasim bali
inavyopendelewa kuwa atiye niya ya kufunga siku ile iwe mwezi mosi
Ramadhani halafu ajizuie mpaka katikati ya mchana ikaja habari ya
kuonekana mwezi aendelee na funga yake lakini juu ya hivyo hapana budi
kuilipa siku ile kwa sababu hakuiamkia siku ile naye ana hakika kamili
kuwa ni Ramadhani na katika sharti ya Saumu kuwa atiye niya ya uhakika
tokea siku.
Saumu iliyohimizwa:
Saumu ya Ashuraa (siku ya
kumi ya Muharram) na aongeze kufunga siku moja kabla yake au siku baada
yake ili kuwahalifu (kwenda kinyume) mayahudi na manasara kwa sababu wao
waitukuza siku hii kwa kuifunga, vile vile inahimizwa kufunga siku ya
Arafa kwa mujibu wa kauli ya Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) :
(صوم يوم عرفة يكفر سنتين ماضية , و مستقبلة و صوم عاشوراء
يكفر سنة ماضية )
“Saumu katika siku ya Arafa
hufuta (madhambi ya) miaka miwili uliopita na unaokuja, na Saumu katika
siku ya Aashuraa hufuta madhambi ya mwaka uliopita.”
Inapendelewa vile vile
kufunga siku tatu, “Ayyaam Beiydh” nazo ni tarehe 13, 14 na 15 katika kila
mwezi wa Hijri (mwezi wa Kiislamu) isipokuwa tarehe 13 katika mwezi Dhul
Al-Hijja kwa sababu ni katika siku za “Attashriq”. Amesema Mtume Salallahu
Alayhi Wasalam
( من صام في كل شهر ثلاثة أيام فكأنه صام
الدهر كله )
Anaefunga katika kila mwezi
siku tatu basi kama aliyefunga zama zote (milele). Na pia inapendelewa
kufunga siku sita katika Shawwaal kwa mujibu wa kauli yake Mtume Salallahu
Alayhi Wasalam:-
( من صام رمضان ثم
أتبعه بستة أيام من شوال فكأنه صام الدهر كله )
“Anaefunga Ramadhani kisha
akaifuatilia (kwa kufunga) na siku sita katika Shawwaal basi kama kwamba
amefunga milele”.
Inahimizwa kufanya Iitikaaf
mwisho wa Ramadhani na ifanywavyo ni kuingia msikiti unaosaliwa jamaa
kabla ya kutuwa jua usiku wa tarehe 21 Ramadhani afanya hivyo kwa ajili ya
radhi ya Mwenyezi Mungu Subhanahu Wa Taalah na kutarajia malipo yake bila
ya kuwa na kusudio lingine na kuwa ajifungie nafsi yake katika msikiti huo
kwa kufanya ibada na asitoke humo isipokuwa kwa kwenda kusali Sala ya Idi.
Hivi ndivyo ilivyokuwa Sunna. Anaetaka kufanya Iitikaaf chini ya muda huo
na atiye niya kabla kwa mujibu wa siku anazotaka kukaa Iitikaaf na
haitakiwi kubadilisha niya hiyo wakati yuko msikitini katika Iitikaaf wala
asijishughulishe na mambo ya kiDunia isipokuwa kwa mambo ya dharura kama
kwenda kukidhi haja au kwenda kula ikiwa hawezi kula msikitini.
Na akifanya Iitikaaf katika
wakati usiokuwa Ramadhani basi ni shuruti afunge. Na kufanya Iitikaaf
katika Ramadhani na hasa katika kumi la mwisho kuna mambo ya kheri
Mwenyezi Mungu huyaleta katika wakati huu na asa akafanikiwa kuipata
Laiylatul Al-Qadri. Mtume Salallahu Alayhi Wasalam alifanya Iitikaaf
katika mwanzo wa mwezi wa Ramadhani na katikati yake na mwisho wake na hii
ndio ilikuwa amali yake ya mwisho Salallahu Alayhi Wasalam. Na Masahaba
walikuwa wakichukuwa kwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam vitendo vyake vya
mwisho mwisho (hawachukuwi) vya zamani lakini wachukuwa vipya). Na alikuwa
Mtume Salallahu Alayhi Wasalam akifunga zaidi katika mwezi wa Shaabani (kuacha
mwezi wa Ramadhani) lakini ni lazima afungue siku mbili za mwisho wa
Shaabani asiziunganishe na Ramadhani kwa mujibu wa kukataza kwake
Salallahu Alayhi Wasalam kuiunganisha Ramadhani na mwengine.
Saumu iliyo makruhu:
Ni Saumu ya siku za
“Attashriq” nazo ni siku tatu zinazofuatia Idi Al-adh-ha (Idi kubwa) kwa
sababu hizo ni siku ambazo Mwenyezi Mungu Subhanahu Wa Taalah anawafanyia
“dhiyafa” (anawakaribisha na kuwakirimu) waja wake kwa hiyo haifai
kuikataa dhiyafa yake na sababu ya kuitwa ayyam “attashriiq” kwa sababu
huanikwa nyama katika jua siku hizo. Na vile vile ni makruhu kufunga siku
moja au mbili kabla ya Ramadhani ili zisiungane nao, na pia kufunga siku
ya Ijumaa peke yake isipokuwa kama ikitanguliwa na siku au ikifuatiliwa na
siku kwa sababu wamesema kuwa Ijumaa ni Idi na haifai kufunga siku ya Idi.
Amesema Shekhe wetu Noor
Diin Mwenyezi Mungu Amrehemu kuwa tofauti iliopo baina ya Idi na siku ya
Ijumaa kuwa imekubaliwa kwa ujumla kwamba ni haramu kufunga siku ya Idi
hata ikatanguliwa kufungwa siku moja au ikafatiliwa na siku moja ambayo ni
kingume ya siku ya Ijumaa kwani imekubaliwa kwa ujumla kwamba inaruhusiwa
kufunga siku ya Ijumaa ikiwa itatanguliwa au ikafatiliwa na kufunga siku
moja. Vile vile katika Saumu iliyo makruhu kufunga milele.
Amesema Mtume Salallahu
Alayhi Wasalam:
لا صام من صام الأبد
“Hajafunga mwenye kufunga
milele”
na kauli yake aliemwambia
Abdullah bin Omar:
صم صيام داود : كان يصوم يوما ويفـطر يوماً
ولا يفـر إذا لاقي
“Funga Saumu ya Dawood
alikuwa afunga siku na afungua siku na hakuwa akikimbia akutanapo (na adui)
na aliambiwa hivyo wakati aliposhikilia ombi lake la kutaka kufunga milele
akamnasihi Salallahu Alayhi Wasalam asifanye hivyo na akamwambia:
( صم و افطر و قم و نم , فإن لعينيك عليك حقا و إن لنفسك و
أهلك عليك حقا )
“Funga na ufungue, usimame (kwa
kufanya Ibada) na ulale kwani jicho lako lina haki juu yako na nafsi yako
na watu wako (mke na watoto wako) wana haki juu yako” na katika hadithi
nyingine “wana hadhi juu yako”.
Vile vile katika Saumu iliyo
makruhu ni Saumu ya msafiri akiwa amedhoofika hata akawa hawezi kufanya
yale yaliyomuwajibikia kuyafanya kama alivyofanya Mtume Salallahu Alayhi
Wasallam katika baadhi ya vita vyake alipoona uchofu umedhihiri kwa
masahaba zake kutokana na kufunga basi akawaamrisha wafungue kwa kuwaonea
huruma kwa hiyo msafiri amepewa ruhusa ya kufungua na hiyo ni Rehema ya
Mwenyezi Mungu Subhanahu Wa Taalah juu ya waja wake.
Saumu kwa ujumla ni kheri na
ina fadhila kubwa isipokuwa kwa zile siku zilizokatazwa kufunga kwa mujibu
wa kauli yake Salallahu Alayhi Wasalam:
لكل شيء زكاة وزكاة الجسد الصوم
Kila kitu kina Zaka na Zaka
ya kiwiliwili ni Saumu.
Na katika kauli yake
Salallahu Alayhi Wasalam:
( من صام يوماً ابتغاء وجه الله أبعده الله من جهنم كبعد غراب
طائر و هو فرخ حتى مات هرما )
“Anaefunga siku moja kwa
kutaka kumridhisha Mwenyezi Mungu (tu peke yake) basi Mola humuweka mbali
na Jahannam kama umbali wa kunguru anaeanza kupuruka yu hali ni kinda
mpaka anapokufa naye amekonga”.
Hadithi mbili hizi
zimetolewa na Abu Huraira. Na katika hadithi:
(
لكل شيء زكاة وزكاة الجسد الصوم)
Kila kitu kina Zaka na Zaka
ya kiwiliwili ni Saumu.
Na katika kauli yake
Salallahu Alayhi Wasalam:
( من صام يوماً ابتغاء وجه الله أبعده الله من جهنم كبعد غراب
طائر و هو فرخ حتى مات هرما )
“Anaefunga siku moja kwa
kutaka kumridhisha Mwenyezi Mungu (tu peke yake) basi Mola humuweka mbali
na Jahannam kama umbali wa kunguru anaeanza kupuruka yu hali ni kinda
mpaka anapokufa naye amekonga”.
Hadithi mbili hizi
zimetolewa na Abu Huraira. Na katika hadithi:
(الشتاء ربيع المؤمن طال ليله فقام وقصر نهاره
فصام)
Siku za baridi ni faida kwa
mwenye kuamini usiku wakni mrefu kwa hiyo hupata kusimama (usiku kufanya
ibada) na mchana wake ni mfupi na hufunga.