Utangulizi:
Kila Desemba Mosi ya kila mwaka Tanzania hujiunga na nchi nyingine
duniani kuadhimisha siku ya Ukimwi duniani. Lengo kuu la siku hii ni
kuwakumbuka waliokufa kutokana na UKIMWI na pia kuwaunga mkono
walioathirika na ugonjwa huu ili waendelee kuishi kwa matumaini.
Kwa mujibu ya Ripoti ya Hali Watu Duniani ya 2000, UKIMWI unaongoza kama
chanzo cha vifo barani Afrika wakati unachukua nafasi ya 4 ya sababu ya
vifo duniani. Inasadikika kwamba zaidi ya watu 35 milioni, wakiwemo watu
wazima na watoto, wanaishi na UKIMWI au na virusi vya UKIMWI. Maambukizo
mapya yanakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 5.4 kila mwaka. Bara la Afrika
ndilo lina ongoza kwa kasi za maambukizo ya UKIMWI.
Hali ya ukimwi Zanzibar:
Zanzibar ikiwa ni visiwa vilivyopo katika mgongo wa dunia, pia inakutana
na vikwazo katika kupambana na maambukizo ya maradhi ya UKIMWI.
Maambukizo ya VVU hupelekea kupunguwa kwa maisha ya watu na kupunguza
nguvu za kazi hasa kwa vijana wa kike na kiume ambao ni tegemeo la
taifa.
Baada ya kugundulika kwa wagonjwa watatu katia mwaka 1986, idadi hiyo
imeongezeka siku hadi siku na kuvifanya visiwa vya Unguja na Pemba mpaka
2002 kuwa na watu 3,287 waliogundulika kuwa na VVU na wakati kasi ya
maambukizo ni asilimia 0.6% idadi inaonesha kuwa wanaambukizika zaidi
kwa mara 4-6 kulingana na wanaume. Kuna idadi ya watu 600
wamesharipotiwa kufa kutokana na UKIMWI na familia hizo zimeacha
mayatima 500 walosajiliwa na kuna idadi ya watu 6000 wanaoishi na VVU
hapa Zanzibar.
|