MAMBO MENGINE YANAYO SABABISHA UKIMWI

1.      Utumiaji wa ulevi na madawa ya kulevya.

2.      Kufanya biashara ya kuuzwa mwili.

3.      Kufanya matendo ya kujamiana yasiyokuwa salama na halali.

4.      Kutafuta maisha ya kupelekea kuondoka nyumbani muda mrefu kwa wafanyakazi wa biashara, majeshi, wasafirishaji mizigo kwa njia za magari makubwa, wavuvi kwenda kulala dago n.k.

  Kwa nini ugonjwa wa UKIMWI unatisha sana?

Ugonjwa huu unatisha sana kutokana na sababu nyingi mbalimbali, baadhi yake zikiwa ni hizo tatu zifuatazo:

    1. Unafyeka watu kama Majani:

        Mpaka sasa takwimu zilizopo zinaonyesha kwamba katika kila watu 100 wanaopata ugonjwa huu 60%  - 70%  huwa ni wale wenye UKIMWI Baridi, 23 - 26% huwa ni wale wenye UKIMWI Vuguvugu; 2%  - 15% huwa ni wale wenye UKIMWI Moto; na katika kipindi cha miaka miwili hadi mitano hao wenye UKIMWI Moto wanaweza kupoteza maisha.

    2. Hautibiki:

       Mpaka sasa wataalam hawajafaulu kugundua dawa za kuchanja ama njia nyingine za kuzindika watu ili wasiugue UKIMWI.

    3. Hauna Kinga:

      Ijapokuwa ugonjwa umelipuka katika miaka ya hivi karibuni tu lakini tayari umeshaenea sehemu nyingi sana duniani. Kutokana na kuambukizana, takwimu zinaonyesha kwamba idadi ya watu wenye UKIMWI imekuwa ikiongezeka mara mbili kila baada ya miezi sita hadi mwaka mmoja.

    4. Unaambukiza:

Ijapokuwa wataalam katika sehemu nyingi duniani wanaendelea kujitahidi sana kutafuta dawa za kuponyesha UKIMWI, lakini mpaka sasa hayajapatikana mafanikio yenye matumaini makubwa.

    5. Ni ugonjwa wa maisha:

        UKIMWI hauimaliziki mwilini. Ukishaambukizwa utabaki nao mpaka ufe. Viini (virus) vya ugonjwa huu vikishaingia mwilini mwako vitaendelea kubana humo na kuzaana humo katika maisha yako yote; na kwa vile mpaka sasa haijagunduliwa dawa ya kuweza kuviua basi ni dhahiri kwamba ukiambukizwa ugonjwa huu utakuwa ni mtu mwenye wasiwasi maisha yako yote kwani japo UKIMWI wako uwe ni wa baridi hujui ni lini utaweza kubadilika na kuwa wa vuguvugu au wamoto.

        Isitoshe licha ya kuwa ni ugonjwa wa maisha, kama wewe ni msichana, ugonjwa huu utaweza kuendelea kuonekana kwa baadhi ya watoto wako kwa miaka mingi baada ya wewe mwenyewe kutoweka.

 

Copyright ©2004-2005  www.uislam.net