Madhara ya Ukimwi
Je ni yapi madhara ya ukimwi kibinafsi, kijamii, kitaifa na
kimataifa?
Kibinafsi:
Anapokosa mtu mwenyewe kujielewa kuwa yeye kaumbwa kwa malengo gani na
ana nafasi gani katika familia yake basi ndipo hapo anapotumbukia katika
majanga mbali mbali kwa makusudi au kushawishiwa anapoingia katika haya
ya UKIMWI anaisababishia nafsi yake:-
1. Kutokuwa na afya nzuri.
2. Anakosa kujiamini.
3. Anakosa kutekeleza amri za Mola wake kikawaida.
4. Anapata khofu ya moyo na jambo hii linaweza kupelekea kifo cha hofu.
5. Huwa mvivu na hiyo humpelekea kudhoofika mwili wake kupungua nguvu.
6. Hukosa heshima.
Kifamilia:
Familia inapokosa elimu hupoteza mwelekeo wa utendaji na usimamiaji wa
majukumu yao ya kila siku.
Familia inapopata madhara haya hukosa yafuatayo:-
1.
Elimu mbadala.
2.
Hukosa ushauri.
3.
Hukosa huduma.
4.
Huwa masikini.
5.
Familia hupoteza kiongozi wake.
Kijamii:
Jamii inapogubikwa na madhara kama haya ya ukimwi, na hata mengine
yasiokuwa haya, basi jamii hiyo huingiwa na butwaa na wasiwasi kwa wana
jamii kuwa huenda watamalizika, ila kwa rehema za Mola wao.
Jamii inapoingia katika vuguvugu hili linalotishia maisha yao hupotea na
kupoteza wengine jamii hiyo huangalia yafuatayo:-
1.
Hukosa wataalamu.
2.
Hukosa wafanyakazi.
3.
Hukosa wasimamiaji wa amri za Allah na makatazo yake.
4.
Jamii hukosa jeshi la ulinzi.
5.
Jamii huingia katika umasikini.
6.
Jamii huzidisha matumizi yenyewe na kuipa mzigo serikali kwa kupiga
bajeti ya matibabu.
7.
Jamii hupata ombaomba, watoto wa mitaani na wajane.
Kitaifa na kimataifa:-
Taifa linapogubikwa na janga kama hii na jengine kama vita vya wenyewe
kwa wenyewe, basi Taifa hilo hupoteza:
1.
Hupoteza wataalamu.
2.
Hupoteza nguvu kazi.
3.
Hupata waathirika wengi.
4.
Hukosa wana siasa bora.
5.
Hukosa uwakilishi wake ndani ya mataifa.
6.
Hukosa uchumi ndani ya soko la dunia.
|