|
Neno AIDS maana yake nini?
AIDS
ni kifupi cha maeneo manne ya Kiingereza: Acquired Immune Deficiency
Syndrome.
Sydrome:
Maana yake ni matokeo, au kikundi cha dalili, au kikundi cha mambo
yanayojitokeza pamoja.
Acquired:
Maana yake ni kukumbwa na au kupatikana na
Immune:
Maana yake ni uwezo wa mwili wa kujihami dhidi ya magonjwa.
Deficiency:
Maana yake ni upungufu, au dosari, au kuwa duni.
Tafsiri ya Kiswahili ya maneno hayo ya Kiigereza "The Syndrome of
Acquired Immune Deficiency" ni: Dalili au Matokeo ya Kukumbwa
na Upungufu wa Kujihami Mwilini. Kama tunavyofahamu kujihami
kunahitaji kuwa na silaha. Ndio kusema basi kwamba mwili wenye Hali Duni
ya Kujihami ni mwili ambao silaha zake za kujihami zimedhoofika. Kwa
hiyo tafsiri nyingine ya Kiswahili kilicho rahisi zaidi kuelezea maana
inayofanana na maneno hayo ya Kiingereza "The Syndrome of Acquired
Immune Deficiency" ni Matokeo ya Hali ya Kuporomoka Silaha za mwili,
na kifupi chake kinaweza kutupatia neno UKIMWI.
U
= Upungufu wa
KI = Kinga.
MWI
= Mwilini.
Neno hili UKIMWI licha ya kuwa tafsiri ya AIDS, linasaidia sana kutoa
picha sahihi ya mtu mwenye ugonjwa huo. Kama tutakavyoona hivi punde,
mtu mwenye UKIMWI (AIDS) ni sawa na askari ambaye amenyang'anywa silaha,
hawezi kujitetea.
|