NJIA, MBINU NA UTARATIBU WA KINGA DHIDI YA VVU:

1.      Kila mwenye ndoa kuilinda na kuheshimu mipaka na taratibu za ndoa.

2.      Kuacha kujiingiza na mambo yote yanayochochea maambukizi ya VVU.

3.      Kutumia vyombo vya habari na vya mawasiliano kwa kuelimisha.

4.      Kulinda walioathirika na VVU na kuwafariji.

5.      Kuepuka na kuacha kufanya tendo la ndoa/kujamiana kusikokuwa na usalama na uhalali.

6.      Kutumia vifaa safi na salama katika kutoa huduma kukatia (kutia  tohara) au kutobolea (kupiga sindano), kunyolea na kutia damu.

7.      Kuwashughulikia na kuwasimamia wanawake kwa kuwapatia maisha yao badala kuachiwa kuhangaika na kupelekea kufanya mambo yasiyo kuwa na faida.

8.      Vijana waelimishwe kuhusu njia bora za kupambana na maisha na kujiepusha na mambo ya anasa na kupeleka kupata maambukizo ya VVU.

9.      Mama mwenye VVU asipokee ujauzito ikibidi ili kuepusha maambukizo kwa mtoto?

10. Kuzuia uenezwaji wa VVU inawezekana pindi mikakati iliopo itatiliwa mkazo, kwa kushirikishwa jamii yote na katika ngazi zote za kifamilia na kiutawala.

                    UKIMWI bado ni tatizo, hakuna tiba wala chanjo lakini inawezekana kuzuia usambazaji wa maambukizo mapya ya VVU. Kubadilisha tabia za watu zinazohatarisha afya ni njia muhimu. Watu wote waelimishwe wajue kwa uwazi kuhusu UKIMWI bila ya kuoneana haya, lakini pia bila kuvuruga mila na heshima kwa wahusika na kukiuka sheria na mafunzo ya Allah S.W.

Copyright ©2004-2005  www.uislam.net